Bondia wa Tanzania atwaa mkanda wa dunia wa uzito wa kati chini Ujerumani

Bondia wa Tanzania atwaa mkanda wa dunia wa uzito wa kati chini Ujerumani

Kaka

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
745
Reaction score
372
Bondia Ibrahim Class Mgendera (26) almaarufu “King Class Mawe” amefanikiwa kutwaa mkanda wa ubingwa wa wa uzito wa kati (lightweight) unaotolewa na Baraza la Ngumi Duniani (Global Boxing Council) kwa kumpiga bondia Jose Forero almaarufu kama “chui” kutoka katika pambano la mizunguko 12.

Pambano hilo lilichezwa siku ya Jumamosi, tarehe 1 Julai, 2017 katika ukumbi wa Müggelspree, Hangelsberg, Brandenburg nchini Ujerumani na kushuhudiwa na zaidi ya mashabiki mia tano wengi wao wakiwa ni raia wa nchi mbalimbali za ulaya na wachache kutoka nchi za Afrika. Ibrahim kabla ya kupanda ulingoni na huku akijiamini sana aliwahakikishia Watanzania kwamba ataibuka na ushindi na kunyakua mkanda huo na kwa mikono yake angependa kumkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa John Joseph Pombe Magufuli mara atakaporejea nyumbani.

Mchezo ulianza kwa Ibrahim kurusha makonde mfulululizo kwa mpinzani wake ambaye naye alijitahidi kuwa imara zaidi huku akipata kuungwa mkono zaidi na mashabiki wengi wa waliohudhuria pambano hilo. Hali hiyo haimkumkatisha tamaa Ibrahim kuendelea kupamba zaidi ambapo mpaka pambano linafikia mzunguko wa 12 ambao ndio wa mwisho Ibrahim alionekana bado ana nguvu ya kuendelea na pambano hilo. Majaji wote watatu katika pambano hilo walimpa Ibrahim ushindi wa 120-108, 119-109 na 118-110 dhidi ya mpinzani wake na hivyo kukabidhiwa mkanda huo wa ubingwa.

Ushindi huo umemuwezesha Ibrahim kuongoza orodha ya mabondia bora katika uzito wake nchini huku akiwa nafasi ya tisa kwa bara la Afrika na 114 kwa dunia nzima kwa mujibu wa tovuti ya Boxrec wakati huo huo Baraza la ngumi duniani (GBC) likimpa nafasi ya tatu na kabla ya ushindi huo hakutambuliwa katika orodha yake ya mabondia bora.

Meneja wa Ibrahim Bi. Victoria Joseph ambaye pia aliambatana naye huko Ujerumani pamoja na kiongozi wa Kamisheni ya Ngumi za KUlipwa Tanzania (TPBC) ndugu Joe Joseph, aliupokea ushindi huo kwa furaha sana na kuahidi kuendelea na hatua inayofuata katika kumuandaa bondia wake kwa ajili ya kuutetea mkanda huo ambapo GBC walitoa fursa kwa Tanzania kupewa kipaumbele cha kuwa mwenyeji wa pambano hilo la marudiano huku Panama na Marekani zikipendekezwa pia endapo Tanzania haitoweza kuandaa pambano hilo.

Kaka ...

Attachments

  • 20170701-IMG_7642-1024x683.jpg
    20170701-IMG_7642-1024x683.jpg
    64 KB · Views: 118
  • GBC TITLE.jpg
    GBC TITLE.jpg
    28.3 KB · Views: 79
  • IC TITLE.jpg
    IC TITLE.jpg
    25.2 KB · Views: 69
  • Victoria Joseph (meneja), Ibrahim Class na Joe Joseph (Kiongozi wa TPBC).jpg
    Victoria Joseph (meneja), Ibrahim Class na Joe Joseph (Kiongozi wa TPBC).jpg
    119.7 KB · Views: 148
Yuko vizuri

Sent from my Halotel H8401 using JamiiForums mobile app
 
akithubutu tu kumpa hio belt Mh.Rais imekula kwa Morombo n'gooo hatouona tena.
 
Yuko vizuri ila asilewe sifa au kujihusisha na mapromota uchwara

Ni kweli mkuu, kwa sasa kijana yuko chini ya timu ya menejimenti ya Joe's Gym na wanatimiza wajibu wao kimkataba na zaidi katika kuhakikisha kijana anafikia ndoto zake na kuliletea sifa taifa.

Safi sana. Tunasubiri mafanikio yake kwa hamu kubwa sana. Huu mchezo ni fursa nzuri ya kujikimu kimaisha iwapo bondia mwenye kipaji chake atapata uangalizi mzuri. Na mafanikio yake itakuwa ni chachu ya vijana wengine kujitokeza na kutumia hiyo fursa ili kujikimu kimaisha.
 
Mzee yani fursa ya kuchezea mkong'oto?
 
Mzee yani fursa ya kuchezea mkong'oto?
Huu ni mchezo na sio mkong'oto. Watu wenye nguvu zao na vipaji vyao wanaonyesha umahiri wao sie wanyonge tunawatizama jinsi wanavyocheza. Mwisho wa siku wanapeana mikono na kupongezana. Kwenye ile michezo yetu ya undava haina sheria na ukipewa mkong'oto unaishia kusonya!
 
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom