Bonge la Nyau atafuta mwonekano, amponda Diamond kwa mtandao

Ibrahim300

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2010
Posts
390
Reaction score
68
Msanii wa Bongo ambaye bado ni mchanga katika sekta ya usanii kwa upate wa umaarufu ameamua kumtemea mate Diamond Platinumz kwa kumwambia aache kashfa. Katika akaunti yake ya Facebook, msanii huyu alimpa makavu Diamond kuwa anapenda kashfa za ovyo.

Tatizo limekujaje?

Katika interviews kadhaa Diamond amekuwa akimponda msanii Ali Kiba kuwa ameisha kimziki natoweza kumfikia kamwe pale alipofika yeye. Tukio la mwisho ni wakati alipohojiwa na kituo cha runinga cha Channel 10 na alikuwa na haya ya kusema:

"Unajua kuna watu hawataki kukubali kama mimi ni zaidi yao kuanzia muziki wangu mpaka maisha yangu, mtu anaulizwa Twitter hivi mkiamua kufanya nyimbo moja na Diamond hamuoni kama itapendeza sana et, anajibu never ever haiwezi kutokea mimi kuimba na Diamond.

Badala angekubali apate Kick nimrudishe katika muziki analeta dharau wakati hanipati kimuziki mpaka kipesa. Muziki wake hauna tena soko istoshe nasikia asahivi amejiunga na mfuko mpya wa kutoa mikopo PRIDE unaitwa FAIDIKA NA PRIDE kakopeshwa kajenga nyumba.

Sitaki kua mnafiki namuweka wazi ni Ali kiba"

Hivi Bonge La Nyau ana haki ya kumpa makavu ama aache muvi iendelee!!

Source: bkuHABARI
 
Sasa kama Ally kiba alihojiwa na shabiki kwenye twitter na akajibu kosa lake likwapi.?
Kwanini diamond haishi kumtaja kiba kwenye interview zake.?
Sio mara ya kwanza kusikia lakin kiba hajawahi kumtaja..

Ali kiba alijibu kimadharau so hio haikumpendea daimond so lazima aongee
 
Ali kiba alijibu kimadharau so hio haikumpendea daimond so lazima aongee

Alimjib VP kimadharau wakat hata hakua anaongea na diamond
2nd alijibu normal kwa hisia zake kwamba haitawezekana sa kosa la alikiba ni lipi hapo
 
Nashangaa hata mimi dharau ipo wapi hapo
Hakuna dharau lakini kajibu kibifu hata kama source ya bifu inafahamika! kwani angesema tu kwa lugha ya kawaida asingeeleweka hadi anaapiza never and ever? Hakuna ubishi kwamba Ally Kiba muziki anaujua but now-a-days there's something wrong; ni kama anapototea taratibu taratibu! Ngoma pekee ambayo kwa sasa inampa kick ni ile aliyoshirikishwa na mdogo wake.
 
Ibrahim,Nimesoma Hiyo Status ya Bonge La Nyau na Haina Tatizo....Ameweka Mtazamo Wake ......Na ameongea vizuri tuuu...Kusema anatafuta mwonekano/kick ni kutotendea vyema haki yake ya maoni.....
Pia,Diamond amekosea kuropoka yale maneno....amebahatika kuwa na watu 'wakubwa' wanaomuongoza na kumpa airtime ya kutosha pia nyota yake kali(Kama anasafiria za watu,mi sijui)....Ali Kiba yuko 'likable' yaani he is humble and sweet na ana 'kipaji' chaa kukubalika na watu wenye 'AKILI ZAO'......pia hatujui ile 'never ever' ya Ali imetoka wapi(lakini nina uhakika,Naseeb anajua 'Why')..Kumsema mtu sababu amekopa ilihali hata wewe Millions zako zina utata ni KUFURU...Diamond Amekosea..
 
Kiukweli alikiba alikosea kuzungumza vile profesionaly walau angesema 'ni ngumu kufanya kazi na diamond lakini chochote kinaweza kutokea' ila diamond kwa manenoaliyeongea amekosea zaidi ingawaje namkubali.
 

hili ni tatizo kubwa sana kwa wasanii wetu wa bongo si mziki,filamu wala mpira wengi hawachagui maneno sahihi ya kuongea wakipata umaarufu kidogo tu wanaropoka nakumbuka tegete alivyokuwa anaropoka kuhusu alivyokuwa anamfunga kaseja wakati yupo simba ajabu saa wapo wote yanga maisha hayatabiriki hiki ndo kitu wasanii wabongo hawaelewi.
 
Inamana huyu big pussy hajui anachotakiwa kukifanya au anajisaulisha
 
Ila Diamond nae awemakini mwenzio anapo nyolewa ww tiamaji mana akifulia atatafuta pakujificha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…