Bonge la Nyau atafuta mwonekano, amponda Diamond kwa mtandao

Bonge la Nyau atafuta mwonekano, amponda Diamond kwa mtandao

Awa watoto Diamond ana hasira nao sana,uyu Kiba ana dharau sana halifikiri domo hatotoka kumzidi anaombwa kolabo anamzungusha mpaka anafuta sauti kuona dogo kachomoka...uyo bonge la pussy mziki ajui katumwa tu na kina bob maana maloser wote wameungana kupambana na domo..Kiba kafuria wajanja wametengeneza pesa kwa mgongo wake akae atulie amalizie mziki wake kwa kusifiwa sijui ana sauti nzuri sijui anajiheshimu,wapiiii na kafuria pale alipo show hapati...

NB: hii bif haijaanza leo
 
hili ni tatizo kubwa sana kwa wasanii wetu wa bongo si mziki,filamu wala mpira wengi hawachagui maneno sahihi ya kuongea wakipata umaarufu kidogo tu wanaropoka nakumbuka tegete alivyokuwa anaropoka kuhusu alivyokuwa anamfunga kaseja wakati yupo simba ajabu saa wapo wote yanga maisha hayatabiriki hiki ndo kitu wasanii wabongo hawaelewi.

Kweli.....haya maisha tuuu....mchezo unaweza kubadilika at any time...
 
Hivi kirefu cha H.O.D ni nini?
Maana nikiwa school, ilikua H.O.D ni Head of Department, ila hapa sijui ni nini?
 
Awa watoto Diamond ana hasira nao sana,uyu Kiba ana dharau sana halifikiri domo hatotoka kumzidi anaombwa kolabo anamzungusha mpaka anafuta sauti kuona dogo kachomoka...uyo bonge la pussy mziki ajui katumwa tu na kina bob maana maloser wote wameungana kupambana na domo..Kiba kafuria wajanja wametengeneza pesa kwa mgongo wake akae atulie amalizie mziki wake kwa kusifiwa sijui ana sauti nzuri sijui anajiheshimu,wapiiii na kafuria pale alipo show hapati...

NB: hii bif haijaanza leo

we ndio pimbi kabisa na nina asilimia mia ujui mziki. mziki autaki dharau ata kidogo mfano mzuri ni preezo na jaguer uyo pimbi preezo yuko wap mwenzake anapeta yeye yuko nyuma kama mkia wa mbuzi
 
Sasa kama Ally kiba alihojiwa na shabiki kwenye twitter na akajibu kosa lake likwapi.?
Kwanini diamond haishi kumtaja kiba kwenye interview zake.?
Sio mara ya kwanza kusikia lakin kiba hajawahi kumtaja..
Kimuziki Kiba na Diamond ...Kiba yuko juu sana anamzidi kila kitu huyo domo ...yaani hamsogelei kwa kitu chochote...ki domo kina bahati lakini najua Kiba akijifua atarudi kwenye game soon..
 
Mkubwa hajambi!

Hahaaa,analiza makalio tu...
Ila kiukweli hiyo tweet ya kiba tusisahau kuwa ni maandishi yale..wakati mtu anaandika huwezi kuona wala kuhisi hisia zake tofauti na alichofanya diamond kuongea live.Sisi wasomaji kila mmoja atasoma kwa hisia zake tofauti.
By the way,sikuwahi kumsikia kiba akimtaja ama kumdiss diamond live iwe kwenye radio ama tv (labda kwa kuwa mimi sio mpenzi sana wa kusikiliza radio wala kutizama tv) ila kwa maoni yangu namuona kiba ni mfano wa super star anavyotakiwa kuwa,hata mr.blue pia.

"Nlikuwepo":bolt:
 
Hakuna dharau lakini kajibu kibifu hata kama source ya bifu inafahamika! kwani angesema tu kwa lugha ya kawaida asingeeleweka hadi anaapiza never and ever? Hakuna ubishi kwamba Ally Kiba muziki anaujua but now-a-days there's something wrong; ni kama anapototea taratibu taratibu! Ngoma pekee ambayo kwa sasa inampa kick ni ile aliyoshirikishwa na mdogo wake.

Never ever sio maneno ya dharau labda angesema kwamba hana hadhi ya kufanya kazi na mimi hapo sawa

Diamond ajiangalie sana huu ndo mziki wa bongo atakuja juta siku moja
 
Hivi kirefu cha H.O.D ni nini?
Maana nikiwa school, ilikua H.O.D ni Head of Department, ila hapa sijui ni nini?

Kwa humu jukwaani kirefu chake ni Heaven On Desert...jamaa mmoja hivi anafanya kazi kwenye ofisi ya Diamond,akili yake anaijua mwenyewe

Asante
 
chuki ya nnn sote tupo chini ya jua.. DOMO umekosea.. unaona umemaliza mwenyewe.. na kusuhu bonge la nyau kukomment bot hii issue ana haki zote , kwan tuna uhuru wa kusema chochote .. ye n nani asisemwe bwana! aende zake huko
 
Mi ni shabiki mkubwa wa Ally k but jibu alilotoa sio zuri,angetafuta namna nyingine ya kujibu ambayo haikeri.Mfano angejibu "Hapana,siko tayari kwa hilo collabo".Ila the way alivyojibu imekaa kibifu sana,hata mi ningekuwa Diamond ningechukizwa kwa jibu hilo.Pia na Diamond naye ndo kakosea zaid,kashindwa kucontrol hasira had anaanza kuhusisha na maisha binafsi ya mtu,sasa hayo mambo ya kukopa Pride ameyaongea yanini?Hata hivyo mi sitak kuamini kwamba Alikiba amefulia kimuzik,kwa kipaji alichonacho sio wa kufulia Leo yule.Kwa mtazamo wangu Alikiba anauwezo mkubwa kimuzik kuliko Diamond ingawa hajamzid sana
 
"upepo ni KIMBUNGA,mchawi ni KIMBUNGA/oyaa,anakupungia jamaa na wewe PUNGA!-yote sawa by niki mbishi
njiwa ana makinda,spika wa bunge ana makinda na yeye bado bado ni spika so anasikika anapoimba_yote sawa baba malcom
 
Kweli.....haya maisha tuuu....mchezo unaweza kubadilika at any time...
tatizo elimu ndogo watu wanashindwa kupangilia hoja zao vizuri,yaani ukiangalia interview za watotot wa mbele wadogo kiumri lakini wanajua kujibu interview accoringky,ukishakuwa superstar sio kila kitu cha kukitolea maelezo mengine unaweza sema tu sitaki kuongelea swala hilo basi coz kuongea sana mara nyingine ndo hupelekea bifu na mara nyingine kujipotezea thamnai kwa mafans wako
 
Never ever sio maneno ya dharau labda angesema kwamba hana hadhi ya kufanya kazi na mimi hapo sawa

Diamond ajiangalie sana huu ndo mziki wa bongo atakuja juta siku moja
sijasema dharau mzazi, nimesema ameongea kibifu bifu...design kama anaapiza hivi! Kwanza ukiangalia bifu kati ya Diamond na Ally Kiba ni mambo ya kijinga tu, am very certain ipo cku watakuja kuelewana tu! So, kulikuwa na sababu gani ya kuapiza kwamba ever never? That's one. Lakini hoja yako kwamba Diamond hajiangalie sana, huu muziki cku moja atakuja juta mi sidhani kama ni issue sana. Kwanza sielewi unamaanisha atakuja kujuta nini. Kama suala kwamba ipo siku ata-drop, ni kawaida sana hiyo kwenye sanaa ya aina yoyote; sio muziki tu! Na ndio maana hata Michael Jackson wa 1980's si yule wa 1990's and 2000's...! By the way, mbona jamaa kawaida tu! Yeye kuwa na bifu na Kiba wala haina maana yoyote kumwapizia kwamba atajuta tu...kwa level yake, suala la bifu ni inevitable kwake coz' lazima tu kutakuwa wanajitokeza mahasimu wa hapa na pale. Na mie naamini kama mchizi angekuwa ni mtu wa ku-entertain mabifu, basi angekuwa ni mtu wa mabifu kila leo lakini jamaa inaelekea anapotezea!
 
Kimuziki Kiba na Diamond ...Kiba yuko juu sana anamzidi kila kitu huyo domo ...yaani hamsogelei kwa kitu chochote...ki domo kina bahati lakini najua Kiba akijifua atarudi kwenye game soon..
Mauza uza, angalau kwa sasa mwache Diamond aitwe Diamond; bahati inakuja mara moja tu! Hakuna anayebisha kwamba Kiba muziki anaujua lakini for time being muziki ni biashara kwahiyo ni zaidi ya kuujua kwa maana ya kutunga mashairi na kuimba kwa sauti ya kuvutia!Diamond sio kwamba ana bahati bali anaifahamu biashara ya muziki kitu ambacho inaonekana kwamba Ally Kiba kuna kitu ame-miss katika hilo! Ally Kiba alipata bahati ya kufanya kazi na R-Kelly lakini akashindwa kuitumia nafasi hiyo kufanya biashara ya muziki wake...ingekuwa ndo Domo pale; wangemkoma! So, this's not all about having a very beautiful voice than anybody under the sun but it's all about how you're gonna emit it to audience! Waimbaji wazuri wasiotumia soko wanatakiwa kuwamo Kanisani wakiimba kwaya, ambao kwa bahati mbaya hata wao wakishaona "they've something" lazima watakuja sokoni! So, kubaki tu kwamba Kiba ni mkali haitoshi; hata Muumini Mwinjuma, Banza Stone, Ally Choki, and in fact; hata Mr. Paul, wote hawa nao ni wakali! There's something missing about Kiba, cjui ni wapi anateleza...inawezekana hana management inayoeleweka and competent in the industry. Kila nikiikumbuka nyimbo yake ya Single Boy, napata uchungu kuona huyu vp; mbona kimya! Haidhuru, si ajabu ukimuuliza atakujibu "nina nyimbo kibao nasubiri wakati muafaka!"
 
Last edited by a moderator:
we ndio pimbi kabisa na nina asilimia mia ujui mziki. mziki autaki dharau ata kidogo mfano mzuri ni preezo na jaguer uyo pimbi preezo yuko wap mwenzake anapeta yeye yuko nyuma kama mkia wa mbuzi


Ujui chochote kipapa wewe..kuna mtoto mwenye dharau km kiba? au bob junia?uyo bonge la pussy ni mick tu iyo katumwa..mara wamtungie ngoma ilimradi kumchokonoa tu domo...Ss ivi hadi ile sharobalo halisi imejikuta imefufuka automatically kupambana na domo..Wakubali dogo ndio wakati wake km ni kufulia mbona kiba ashafuria kila msanii dunia hii ana wakati wake inategemea unaitumiaje,ss wenyewe walitumia vibaya watulie warudi ata kucheza boli tutawaombea namba ata ashanti pale..Diamond hawamueezi na bado ana muda mrefu watajiua ata kujiua kwa wivu..
 
Hata hivyo mi sitak kuamini kwamba Alikiba amefulia kimuzik,kwa kipaji alichonacho sio wa kufulia Leo yule.Kwa mtazamo wangu Alikiba anauwezo mkubwa kimuzik kuliko Diamond ingawa hajamzid sana
Ali k yupp vizuri sana kiuimbaji,ana sauti balaa..ni kama walivyokuwa kina Qchilla..na atabaki kuwa na sifa izo milele hakuna wakumnyanganya ilo ata domo...Ila linapokuja swala la muziki Diamond mzk anaujua,anajua wabongo wanataka nini,anajua kutengeneza muziki mzuri unaofanya vema sokoni ata km hana sauti ya ivyo na ana discipline ya kazi yake,,anajua kumaintain kick zake..anajua soko lake lipo wapi na hajivungi kulifata,,,vitu ambavyo kiba hana..kiba anajiona ni staa kiasi kwamba kila mtu kwake ni mdogo ata asante hazijui..
 
Hivi kirefu cha H.O.D ni nini?
Maana nikiwa school, ilikua H.O.D ni Head of Department, ila hapa sijui ni nini?
Huyo hapo mtu mwenyewe!Anatumika na mwanamme mwenzake
 

Attachments

  • 1390841121484.jpg
    1390841121484.jpg
    129.9 KB · Views: 67
Jumapili ya jana ilikua jumapili mbaya sana kwa msanii Diamond kwani ni kama vile karibu watu wote waliojiunga instagram walimuona mtu mbaya kwake. Ishu ilianza ivi, kupitia akaunti moja huko Instagram inayotumia jina la TeamKiba iliandika ujumbe unaosemekana umeandikwa na Diammond ukisema "Unajua kua kuna watu hawataki kabisa kukubali kua mimi ni zaidi yao kuanzia mziki wangu mpaka maisha yangu, mtu anaulizwa twitter hivi mkiamua kufanya nyimbo na Diamond hamuoni kwamba itapendeza sanaa. Et never eve haiwezi kutokea mimi kuimba na Diamond, badala angekubali apate kick nimrudishe katika mziki analeta dharau wakati anipati kimziki wala kipesa. Muziki wake hauna tena soko nasikia sasa hivi kajiunga na taasisi ya mkopo inaitwa FAIDIKA NA PRIDE kakopeshwa kujenga nyumba. Sitaki kua mnafiki ni Ali Kiba"

Mwandishi wetu wa Ngama Media aliendelea kufatilia picha linaendaje na baada ya mda mfupi akaunti hiyo iliendelea kupost ujumbe mwingine kwa njia ya picha unaodaiwa kua umetolewa katika page ya Rafiki mkubwa wa AliKiba anaefahamika kwa jina la Bonge la Nyau ukisema "Hivi huyo msanii Domo Diamond anamtaka kitu gani msanii Ali kiba? Tokea juzi amekua akimzungumzia katika media kwa wale mliofatilia katika interview yake baada ya kusamehewa na kituo cha chanel ten aliropoka maneno haya kuhusu Ali Kiba kujiunga Pride akakopeshwa ndio tatizo? Kuna matajiri kibao humu mjini wana maisha mazuri kwa ajili ya mikopo. Zote chuki Diamond kama na wewe unataka mikopo si ukajiunge?? Sio kumpiga majungu mwenzio watu kibao wamejiunga na mikopo washapata inawasaidia. Kama na wewe unataka tena usisusumbuke utapatiwa mkopo na sio kumponda mwenzio.

Sasa movie linaanza hapaaaa, kupitia akaunti ya Bonge la nyau instagram, Bongo la nyau alikana kuandika ujumbe huo hapo juu na hichi ndo alichokisema " Jaman haya mambo yanayoendelea mm yanazidi kunisangaza cz napigowa simu sana na kutumiwa msg kwamba nimepost msg ya kumponda diamond kwa kusema alimponda ali kiba before... dah kweli nishai inshu iko iv iyo account hapo juu ilikuwa yangu miezi mitatu iliyopita bt kuna matapeli wa pride walinizidi ujanja wakai haki na kuchange password mpaka email ikawa chini yao wananisumbua sana cz wanapokea deal zangu zote wanawatapeli watu, watu wakijua wanawasiliana na bonge la nyau nshapokea cm ya kulaumiwa sana mpaka kutaka kupelekwa police kwaajiri ya matapeli hao cz iyo account ilikuwa kuwa kubwa sana na ina fans zangu wengi wanaojua kuwa ni mm uyo bt sio ivyo leo wamekuja na utapeli mwingine wa kuwachonganisha diamond na ali kiba ili kutangaza mambo yao ya pride sio poa kabisa cz wananiharibia mm naonekana naingilia mambo yasiyonihusu kabisa siwezi kukaa kuponda msanii mwenzangu yoyote wala kumuongelea kwa mabaya..... iyo sio peg yangu na siitumii so kama utamuitaji bonge la nyau hapatikani kwa page iyo ntwawapostia page yangu nnayatumia, hao ni matapeli wa pride wanaowaibia watu cz hata ukisoma story vizuri wameingia mambo ya kujengewa nyumba na pride akajidai eti mbona na mm bonge la nyau nimejenga kwa mkopa wa pride no no no no me sijajenga kwa pride na still niko kwa mama yangu ni uzushi tuu wa kutaka pride i kik kwa kupitia majina ya wasanii.."

Baada ya uchunguzi wetu uliofanya na mwandishi wetu kutoka Ngama Media tuligundua kweli kua akaunti ya Bonge la nyau ipo hacked na ndo ilitumiwa na matapeli kuchochea bifu hilo hapo juu.

Utapeli uliokua ukitumika katika akaunti feki kwa kutumia wasanii majina ya wasanii mbalimbalindo uliotumika na hapa katika bifu hili la Ali Kiba na Diamond. Matapeli hawa hujifanya wanatoa mikopo ya hadi zaidi ya milioni 20 kwa kujisajili kwa sh 80,000 tu. Sasa ukijidanganya ukatuma hiyo hela jua kua ndo umeshatapeliwa na hela yako haitarudi na hata ukiwapigia kwa namba uliyowatumia hela hutawapata.

Ukweli ni kwamba hakuna mikopo inayotolea mtandaoni bila ya dhamana na bila ya kuandikishiana mikataba sasa chunga sana usije ukaibiwa
 
Back
Top Bottom