Bongo 5 mnaelekea wapi..?

mayowela

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2014
Posts
2,125
Reaction score
1,753
Mtandao wa Bongo 5 nimekuwa nikiufatilia sana na ni moja ya mitandao ya muda mrefu hapa nchini unaomilikiwa na wanandoa wawili Lucas Neghest na Nancy Sumari.Wamiliki hawa walithubutu na wakaweza.
Mtandao huu ulienda mbele zaidi na kuanzisha Tuzo za Watu ambazo zilikuwa na mashiko na zenye thamani, lakini pia ulivutia zaidi baada ya kuongeza timu ya watu fanisi na wabunifu ambao ni Fredrick Bundala (skywalker) na Sandu George( kidbwoy) walileta vitu tofauti na ikawa tishio kwa wengine,
Fredrick Bundala akiwa muhariri wa mtandao huo alifanya anachostahiri na ukawa dozi ya wasomaji haipiti siku bila kuingia huko mmojawapo ikiwa mimi mpaka siku kukiwa hakuna habari mpya nahisi hawa jamaa wako off labda, na nilipenda ikanifanya nipende kazi ya uandishi

Sasa Bongo 5, kwa muda kama sikosei mwezi sasa naona kuna mabadiliko makubwa, ni kama tena habari hazihaririwi, michapio mingi sana, habari zinajirudia, heading na habari vitu viwili tofauti, Hii inamaanisha kuondoka kwa Fredrick Bundala ambae alikuwa anahariri habari kumewafanya myumbe..? na wengineneo

Jirekebisheni wasomaji wenu bado tuna matumaini na nyinyi.. Kazi njema
 
Mkuu huenda labda mambo hayapo sawa kama ulivyosema ya huyo mhariri kutokuwepo..Tuwaoe muda watajirekebisha
 
Wanaelekea mbezi hawa uku njoo Niku assist uwaone
 
Bongo 5 ndio nini Mkuu...naomba nifahamishwe tafadhali.
 
Mmmmhhh sijapitia huko muda sionagi kipya skuizi
 
Kweli kabisa tangu aondoke Mhariri Fredrick Bundala "Skywalker" ubora na ubunifu wa Bongo5 umepungua sana.

Sikuhz wanaanza kupitwa na dizzimonline alipohamia Skywalker.

Wajipange upya watafute Mhariri na Waandishi wengine wenye "calibre" ya akina Skywalker na KidBway
 
Mkuu nashukuru sana kwa kunijulisha wamiliki wa huo mtandao,maana nilikuwa nautembelea bila kuwajua wamiliki.
 
Mkuu tafuta sehemu wameandika About us au Tuwasiliane uwape dukuduku lako
Una email 14 ikiwemo ya edomasanja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…