Tangu mlipowaacha waafrica wenzenu walipokua wanauliwa na wazungu kusini mwa Africa, ninyi mkawakumbatia wazungu kwa sababu za kiuchumi, hakuna nchi yoyote ya kiafrica itakayoiamini Kenya.
Mlipopata Uhuru mkawasaliti waafrica ambao walikua hawajajitawala sio?. Mozambique walipigana, walipopata Uhuru tu, siku hiyo hiyo wakaanza kuwasaidia Zimbabwe, Zimbabwe ilipopata Uhuru wakawasaidia Namibia, ninyi mlipopata Uhuru mkakaa meza moja na wazungu kuwakandamiza waafrica wengine.