Bongo fleva boresheni Mziki wenu Video Mnajitahidi

Jana nilikua namsikiliza mchizi mox. alitolea mfano wimbo wa weusi unaitwa tatizo bei ya mkaa.
Ukisikiliza mashairi na kiitikio hakuna uhusino wowote.
mashairi ya wimbo na kiitikio nimendika hapo chini.

Inabidi waka onge promo na kaligi haka si ndio somo wanawivu mpaka umezidi kikomo, dhidi ya,
weusi wale ni watu wa media.....

kiitikio

tatizo ni bei ya mkaa, bei ya mkaa.

Nyimbo zenye kasoro kama hizo, ni nyingi sana.
 
Reactions: prs
Na ule Hesabu je wa Nikki?
 
video gan hizo ambazo wanajitahidi..? zile za ma-director n kutoka S.A na Naija au za hanscana na ivan n.k ?
 
Reactions: prs
video gan hizo ambazo wanajitahidi..? zile za ma-director n kutoka S.A na Naija au za hanscana na ivan n.k ?
Nimelinganisha Miaka 10 iliyopita na Sasa wamepiga hatua..Ila Bado wanahitaji kuongeza Bidii..
 
Ni tatizo Mkuu..inatakiwa Waingie gharama Studio..na wapunguze kutumia auto-tune Maana hata Mashairi hayasikiki.

Na hii ni shida kubwa. Matumiz ya out tune yamezid
 
Reactions: prs
Sasa hiyo ni kazi ya producer kumpanga na kumpika msanii asiimbie utumbo...

Wasanii wengi wa bongo flavour hayo mambo uliyoyataja hawayajui...

MJ records na Bongo records wamejitahidi sana...

Cc: mahondaw
 
Reactions: prs
hahaha sasa inakuaje mtu ambaye yupo kwenye field hiyo halafu asijue uwepo wa hayo maneno kwenye field yake? Ni sawa na mwalimu asijue kitu kinaitwa curriculum
 
Ni Kweli Mkuu kwa Wasanii ambao wana mikataba na Studio Producer anaweza Kulaumiwa kiasi..Ila Wasanii Wanatakiwa kutunga nyimbo zao makwao ,Mashairi pamoja na Chords ,Walimu wapo..Siyo kutungia nyimbo Studio.
 
Siku hizi muziki umekua biashara... kwa kua unapesa ya kulipia studio basi unarekodiwa ili mradi... enzi ya Mastet J na Majani...

Walikua hawakurekodii kama unachowaletea ni upuuzi na walikua wanakushauri kabisa hii ungemuweka fulani hapa, badilisha hiki hapana, hii fanya hivi, hii sitaki...

Siku hizi wasanii hawaumizi vichwa kabisa, pesa yako tuu...

Cc: mahondaw
 
Reactions: prs
hahaha sasa inakuaje mtu ambaye yupo kwenye field hiyo halafu asijue uwepo wa hayo maneno kwenye field yake? Ni sawa na mwalimu asijue kitu kinaitwa curriculum
Wapo Mkuu Maana Vyombo vya Studio si gharama sana.
 
siku hizi wengi wanashindana kutoa matusi yatakoyobamba
 
Reactions: prs
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…