Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,422
- 5,659
Nimekwazwa na kilichotokea kwa wasanii kufurumushwa uwanjani pasipo kutumbuiza na pia kuonekana kama watu waliokuwa wamevamia shughuli licha ya kuwavalisheni mavazi yenye uwiano wa rangi na jeshi lenu pendwa halikuwa jambo la kupendeza wala kupongezwa.
Ni kweli tulipaswa kuenzi utamaduni wetu leo na kuupa kipaumbele kama kucheza ngoma n.k, lakini tulipaswa kutambua kuwa bongofleva pia ni fahari tuliyonayo na tulipaswa kujivunia hilo mbele ya mataifa yote badala ya kuwapa nafasi sijuhi wachekeshaji tuliowaokota wapi ambao walizungumza pumba za kuchefua bongo za kila aliyewasikiliza.
Watu hawa ambao walionekana wahuni mwanzo, wakastruggle mpaka kukubalika mbele ya jamii, hatimaye leo wamefanya mziki uwe biashara na kitambulisho chetu nje ya nchi ukiachilia mbali michango yao mbalimbali wanayoitoa kwa jamii ni watu wa kukosa nafasi kweli hata ya kuwasilisha wimbo wao kwa jamii katika siku muhimu kama hii.
Kijana mnayemzungumzia mtamuinua ni yupi hasa? Ikiwa leo hii kijana mdogo kupitia sanaa ya muziki anatoa kodi ya mpaka bilioni 1 na ajira juu kwa vijana wenzake bado amtambui thamani ya sanaa yake na hamuwapi nafasi kuwainsipire new generation kuwa na wao ipo siku michango yao itathaminiwa mbele ya macho ya wazawa watasimama kupitia bongofleva kuimba mbele ya shughuli muhimu za kitaifa na kimataifa.
Tumekuwa tukiwatumia vijana hawa kuimba nyimbo za uzalendo kupamba TV zetu za taifa na kutupigia kampeni lakini moyoni bado hatujawapa hadhi yaani tunawachukulia wakutumika for purpose na influence tu, kiukweli kilichotokea leo niwape pole wasanii wote wa nchi hii najua wamevunjika moyo ila hawana pa kusemea na wanaishia kubaki kinyonge.
Naomba wimbo wenu mliokuwa mmeutunga msiufute nakuusahau vichwani maana ipo siku mtautumia tena, amini mwakani wakiona shughuli si ya muhimu sana mtatafutwa kwa mbwembwe na promise kibao kuhusu bongofleva yenu huku mkihamasishwa muandae wimbo bora wa shughuli hii hii (hili umati usiwakimbie uwanjani) ambayo leo hii mmekosa nafasi kisa mtawaaibisha mbele ya kadamnasi muhimu kwao.