Kaka Pekee
JF-Expert Member
- Apr 3, 2018
- 336
- 564
Wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ukiongea nao wanadai walipunjwa malipo. Baadhi waliofariki kabla ya kulipwa, warithi wao wanakuambia hawakuambulia kitu na waliolipwa mlolongo wa malipo kwao ulikuwa mkubwa kuliko.
Upanuzi wa barabara, viwanja vya ndege. Wahanga wa mabomu Mbagala na Gongo la Mboto, wote walilipwa baada ya malalamiko mengi kuliko kiasi walichostahili. Kifupi walizinguliwa mno. Ndivyo ilivyo hata malipo ya pensheni kwa mifuko ya kijamii vilio kwa wastaafu haviishi.
Baada ya utata wa Kikokotoo.
Rais aliingilia kati na kufutilia mbali mipango ya Jenista na wenzake. Kaulize kama mtu kalipwa mpaka leo. Wastaafu wamekuwa wanyonge ndani ya taifa lao walilolitumikia kwa jasho na uzalendo mkubwa. Pengine kuliko waliokalia ofisi za malipo yao kwa sasa.
Mzee Lutusyo Mbeleka kutoka Tukuyu huko.
Ni mwaka wa 28 sasa anafuatilia mafao yake bila mafanikio. Kama alistaafu na miaka 60, leo tunaongelea miaka 88. Kina Lutusyo wangapi tusiowajua wakiwa hai au wafu bila kulipwa mafao yao? Ni shetani gani kaweka kambi kwenye fidia na mafao nchi hii?
Achana na Kikokotoo ambacho nacho ni mazingaombwe tupu. Wakulima wa Korosho huko kusini ni malalamiko tu. Hakuna lingine zaidi ya kusikia serikali inalalamika.
Wakulima wanalalamika. Wale Kagomba sijui wanalalamika. Malalamiko kila siku kiasi kwamba wengine hatuelewi lipi ni lipi. Kuna tatizo kubwa sana.
Baadhi ya viongozi wanadai kuna watu wanataka nchi isitawalike.
Tukumbushane tu kuwa pale Sudan, Rais Omar Al Bashir pamoja na ukubwa wa jeshi lake nchi haikaliki. Tatizo ni ongezeko la bei ya mkate tu, watu wapo mtaani usiku na mchana.
Suala tena siyo bei ya mkate ipungue, bali Bwana Omar aondoke madarakani.
Mafindofindo kwenye nyoyo za Wabongo ni makubwa kuliko upuuzi wa bei ya mkate. Jeshi si lolote si chochote mbele ya malimbikizi ya hasira katika nyoyo za kina Lutusyo na wengineo. Miaka 28 anasotea mafao? Wanaonyimwa stahiki za fidia au mafao ni hatari kuliko kelele za kina Tundu Lissu.
Imeandikwa na: Dk Levy