Bongo hapo zamani: Nyerere alipoongoza kikao kilichoiua TAA na kuizaa TANU

Bongo hapo zamani: Nyerere alipoongoza kikao kilichoiua TAA na kuizaa TANU

Mudir
Kwema Maalim wangu nashukuru sana kwa kazi nzito unayofanya kuweka sawa hii historia yetu ya Tanganyika, vizazi vijavyo viweze kujua nchi yao.
 
Mudir
Kwema Maalim wangu nashukuru sana kwa kazi nzito unayofanya kuweka sawa hii historia yetu ya Tanganyika, vizazi vijavyo viweze kujua nchi yao.
Ritz,
Ahsante sana kaka.
 
huyu Abdul Sykes ilikuwaje akawa financier wa TANU wakati alikuwa Market Master tu wa sokoni, pesa za kufadhili TANU alitoa wapi?
 
huyu Abdul Sykes ilikuwaje akawa financier wa TANU wakati alikuwa Market Master tu wa sokoni, pesa za kufadhili TANU alitoa wapi?
Laki...
Ili kukufahamisha hali ya Dar es Salaam na siasa zake zilivyokuwa inabidi nikurejeshe nyuma katika miaka ya 1900 Wajerumani wameshaituliza nchi na hakuna vita tena baada ya kuwashinda Absushiri bin Salim Al Harith na Mtwa Mkwawa na kumaliza upinzani wote.

Vita Maji Vya Maji vimekuja mwaka wa 1905 na baada ya kuwanyonga majemadari 62 waliokuwa wakipiganisha vita hivyo maarufu katika hawa majemadari akiwa Abdulrauf Songea Mbano baadhi wakishindwa kutamka ''Rauf,'' wakimwita ''Wawufu,'' nchi ikawa imetulia.

Wajerumani waliituliza nchi kwa msaada mkubwa sana wa majeshi ya mamluki Waafrika wenzetu kutoka Sudan ya Kusini Daafur Wanubi na Wazulu kutoka Mozambique waliochukuliwa katika kijiji kinaitwa Kwa Likunyi, Imhambane.

Maarufu katika watoto wa hawa mamluki wa Kizulu na Kinubi walikuwa Kleist Sykes na Ibrahim Hamisi hawa walikuja kuunda African Association mwaka wa 1929 chama kilichokuja kuzaa TANU mwaka wa 1954 chama kilichopigania uhuru wa Tanganyika.

Alikuwapo pia Hassan Machakaomo baba yake alikuwa katika lile jeshi la Wazulu lakini mwanae Hassan Machakaomo alifahamika za zaidi katika uongozi wa Young Africans Football Club miaka ya 1940.

Walikuwapo pia na mamluki wa Kimanyema kutoka Belgian Congo, babu yangu mkuu Abdallah Mwekapopo Samitungo Muyukwa akiwa mmojawapo.

Wajerumani kwa kuonyesha shukurani yao kwa jeshi hili la mamluki walitengeneza jeshi lililowaunganisha hawa wote na jeshi hili likaitwa Germany Constabulary na Mkuu wa Jeshi hili alikuwa Chifu wa Kizulu jina la kwao lilikuwa Mohosh, lakini Tanganyika akajulikana kama Affande Plantan.

Jeshi hili likawekwa ndani ya kambi hapa Dar es Salaam na walikuwa na ardhi yao waliopewa kama makaburi yao ya kuzikana sehemu za Pugu Road.

Wajerumani wakajenga shule pale ilipo Ocean Road Hospital kwa ajili ya watoto wa hawa wanajeshi na wakawa kila akizaliwa mtoto wao wanamsajili na kumpa jina la Kijerumani ndiyo maana leo bado tunao akina Sykes na Plantan kizazi cha tano kuzaliwa katika ardhi ya Tanganyika.

Lakini kwa kuwa hawa Wazulu walikuwa Waislam mtoto akifikishwa nyumbani baba na yeye anatoa jina lake na ndiyo wakapatikana Kleist Abdallah Sykes na Schneider Abdillahi Plantan.

Watoto hawa wakapata elimu ambayo kwa miaka ile ilikuwa kubwa wakisomeshwa Kijerumani na wakikizungumza kama maji, wakafundishwa kupiga taipu, kuweka mahesabu na wakatiwa katika jeshi lile lile walilotumikia baba zao - Germany Constabulary.

Katika jeshi hili wakawafunza mbinu za vita, utumiaji wa silaha na mambo ya ''signals,'' na kupiga ''morse.''

Babu yangu alisomeshwa ''foundry,'' yaani ufuaji chuma na kutengeneza vipuli (spare parts).

Hawa wakawa ''professionals,'' wa wakati wao na wakawa juu ya raia wengine wa kawaida kwa hali zao kwa ajili ya elimu na upendeleo waliopewa na Wajerumani.

Ilikuwa rahisi sana kwa wao kupata ajira na hata kujiajiri kwani walifunzwa ujenzi, useremala na kazi nyinginezo.

Wagawe uwatawale ndiyo ilikuwa sera ya wakoloni.

Hapa Dar es Salaam Wazaramo, Wangindo, Warufiji, Wandengereko na makabila mengine yakawa wao wako chini wakijifananisha na Wazulu, Wanubi na Wamanyema.

Kujihami wakawaita hili kundi lililotoka nje ya mipaka ya Tanganyika ''Wakuja.''

Juu ya hali hii hawa ''Wakuja,'' ndiyo wakawa waasisi wa taasisi muhimu sana katika jamii ya Kiafrika wakimiliki majumba kadhaa na biashara ndogo ndogo na wakawa na maisha bora katika hali ile ya kikoloni.

African Association walikuwapo Kleist Sykes na Ibrahim Hamisi na wanachama wengi wakiwa ni hao hao jamaa zao.

Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika walikuwa pia ni viongozi hawa hawa kama waasisi, Kleist Sykes, Mzee bin Sudi na Ibrahim Hamisi - Mzulu, Mmanyema na Mnubi.

Ukija katika Maulid Committtee ni hao hao ndiyo viongozi na jamii ya Kiarabu na Kihindi.

Nimetanguliza huu mkadama mrefu ili msomaji apate picha ya hali ilivyokuwa wakati ule.

Laki...
Umetumia maneno Abdul Sykes alikuwa Market Master tu.

Hii ilikuwa kazi kubwa sana.

Abdul Sykes katoka jeshini KAR Burma Infantry akiwa na cheo kikubwa ambacho Mwafrika angeweza kupata katika jeshi lile la Waingereza - Quarter Master Sergeant.

Baba yake katika jeshi la Wajerumani katika WW I alikuwa "Aide de Camp" wa Paul von Lettow Vorbeck.

Wakoloni wakiheshimu sana vyeo katika majeshi na Abdul alipewa kazi ile ya pili na Waingereza kwa ajili ya "rank" yake katika jeshi la Waingereza.

Kabla ya hii nafasi Waingereza walimteua kama Secretary General wa Dockworkers Union mwaka wa 1947 na hii ilikuwa nafasi kubwa sana wakati ule.

Hii Waingereza walikuwa wakichukulia kama ''continuation of service'' kutoka jeshini.

(Nimeandika historia kamili ya Dar es Salaam Dockworkers Union kwa msaada mkubwa wa Mzee Islam Barakat aliyekuwa Labour Inspector wakati wa ukoloni na pia askari wa KAR WW II).


Kwa hiyo toa fikra kuwa Market Master ilikuwa nafasi ndogo.

Tuache haya mambo ya kuajiriwa serikalini.

Abdul alikuwa mmoja katika wakurugenzi wa kampuni ya baba yake Sykes and Sons pamoja na baba yake mwenyewe na ndugu zake wawili iliyokuwa na machimbo ya chokaa Kigamboni.

Hii biashara ilikuwa kubwa sana kwani chokaa yote iliyokuwa ikitumika katika majengo ya Tanganyika Railways Tanganyika nzima katika kupaka ofisi hadi nyumba za wafanyakazi, kupaka madaraja na alama katika njia za reli ''supplier,'' ilikuwa kampuni hii.

Siku zile matumizi ya rangi yalikuwa madogo sana.

Bwana Ally alipata kuniambia kuwa kila mwisho wa mwaka baba yao akifunga vitabu vya kampuni alikuwa akigawa ''dividends,'' sawa kwa sawa kwa wakurugenzi wote kiasi Ally Sykes aliweza kununua gari akiwa kijana mdogo sana na Wazungu wakichukia kumuona Mwafrika anaegesha gari kwenye sehemu ambayo walidhani yataegeshwa magari ya Waingereza peke yao.

Hizi dividends walianza kupewa 1942 wakiwa Burma baada ya baba yao kubadili umiliki wa kampuni.

Wamerudi vitani 1945 wamekuta kila mtu ana fedha benki ambazo hawakuzitegemea.

1950 Abdul Sykes alifungua Filling Station yake Ilala Boma na hii ilikuwa biashara kubwa ikimuingizia fedha nyingi sana.

Fedha hizi ndizo zilizokuwa zikienda TANU HQ kila mwisho wa mwezi na ikafikia mahali biashara hii ikaanguka na ikabidi ifufuliwe upya kwa mkopo kutoka kwa rafiki zake katika jumuia ya Ismailia.

Soko la Kariakoo kwa Market Master lilikuwa sawa na shamba lisilokuwa na msimu wa mavuno.

Muhudumu wa ofisi ya Market Master Mzee Abdallah ambae baadae alikuja kufanya kazi bandarini na ndipo tulipofahamiana alipata kunieleza kuwa yeye alikuwa anachinja hadi kuku 20 anapeleka nyumbani kwa Abdul Sykes kwa ajili ya wageni wake.

Takrima nyingi ambazo Abdul akiwafanyia wageni wake na viongozi wa TANU nyumbani kwake pale Stanley Street chakula kilikuwa kinatoka hapo sokoni.

Naamini msomaji umeweza kupata picha ya hali ilivyokuwa wakati ule.

Hii Petrol Station ipo hapo hadi leo inaelekezana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ilala.

Iko siku nitakuhadithieni historia ya ''sanduku la fedha la Abdul Sykes na watu wa TANU,'' kama alivyonieleza mkewe, mama yangu Bi. Mwamvua maarufu kwa jina la Mama Daisy.

Wakati ule kati ya hawa ndugu watatu na mama yao Bi. Mruguru bint Mussa walikuwa wanamiliki nyumba saba zaidi au pungufu kidogo maana zipo walizokuja kujenga au kununua baada ya uhuru mwaka wa 1961.

Huyo hapo chini anaezungumza Kijerumani ni Thomas Plantan katika Kumbukumbu ya Paul von Vorbeck mwaka wa 1964.

Kwa Abdul kuwa na uwezo wa kufadhili harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika fedha hazikuwa tatizo kilichokuwa muhimu kwake ni ule moyo wa kujitolea na ukarimu.

Si ajabu kuwa rafiki zake walimpa jina wakimwita, ''The Sweet Abdulwahid Sykes.''

 

Attachments

  • 1573040457869.png
    1573040457869.png
    527.7 KB · Views: 2
  • 1573040467538.png
    1573040467538.png
    527.7 KB · Views: 2
  • 1573041042665.png
    1573041042665.png
    161.3 KB · Views: 2
Back
Top Bottom