Bongo kunakera!


Sasa hizo shopping malls za nini bongo kama mambo yenyewe ndio kama haya!?
 
Mr. Price Nguo ya 150,000 yaani zaidi ya Rand 1000 (tena ya kike) du labda bongo, lakini in SA sidhani kama kuna nguo ya bei hiyo kwa Mr Price

Nafikiri huja soma vizuri hapo.....kwenye kapu alikuwa na zaidi ya nguo moja! Read this ''kwenye kapu nina nguo ya thamani ya 150,000 na hii top moja mnayotaka kuninunulisha ni 22,000 tu sasa nilipie hizi zilizonisha nah ii niache au niziache hizi za laki na nusu''[/COLOR ...ni vidole tu viliteleza sentensi ya kwanza!
 
Mimi nawashangaa watu mnao ng'ang'ania kwenda sehemu hizo zenye ubaguzi wa khali ya juu wkt unaweza hata kwenda hapo Manzese,K/Koo,Ilala au mchikichini ukakaribishwa kama mfalme nakupigiwa magoti ununue mzigo kwa bei poa.
Aache kushangaa alicho taka ndo hicho.
 
Sasa hizo shopping malls za nini bongo kama mambo yenyewe ndio kama haya!?

Hizi ni exceptional cases jamani....si kila mahali utaenda ukumbane na adhaa hii, though nakubali customer care bongo iko chini hata ukicompare na jirani zetu wa Kenya!
 
Unajuwa pia Elimu inasaidia sana tena sana ndio maana maana angekuwa mtu aliyesoma asingeweza kufanya hivyo kabisaaaaaa....Pia pole sana
 
Hivi wadau niambieni kwanza ukiwa na card ya VISA mfano kutoka U.K na hiyo card yako ndani inahela unaweza kuitumia hata bongo kuchukua hela zako kama kawaida????au inakuwaje hapo????
 
Hivi wadau niambieni kwanza ukiwa na card ya VISA mfano kutoka U.K na hiyo card yako ndani inahela unaweza kuitumia hata bongo kuchukua hela zako kama kawaida????au inakuwaje hapo????

Unaweza kuitumia kama debit card yako yenye logo ya VISA na ku withdraw hela kutoka kwenye ATM nyingi tu nchini sasa hivi. Nafikiri sasa hivi most Banks zote zina networks ambazo zinaruhusu transactions za accounts za nje. Mwaka jana ilikuwa ni benki za kigeni (Barclays, Stanbic, na Standard Chartered) among others. Kuna limit ya kiasi gani uta withdraw kwa siku. Mimi nilichargiwa fees za aina mbili. Moja ya Barclays, kwa kutumia machine yao, na ya pili, Wells Fargo wakani charge kwa ku transfer hela lakini ilikuwa ni very minimal. Na fedha utazipata in Tanzanian shilling. I hope this information helps kiasi.
 
Sasa hizo shopping malls za nini bongo kama mambo yenyewe ndio kama haya!?
ndugu yangu,
culture ya Malls mbona ni mpya sana bongo? Hizo super markest na convinient stores bado ni novel idea.Hao wauzaji bado wanaona mauzauza.Wakizoea wataacha!
 
Hivi wadau niambieni kwanza ukiwa na card ya VISA mfano kutoka U.K na hiyo card yako ndani inahela unaweza kuitumia hata bongo kuchukua hela zako kama kawaida????au inakuwaje hapo????
Kama alivyokwambia Capitol, mimi hutoa shilingi mara zote nikienda nyumbani kwenye cash point yoyote ile kutumia Visa debit card yangu, huwa benki yangu (Barclays UK) wananikata £2.50 kwa kwa kila transaction, ila kwa kutumia kadi dukani Bongo sijawahi.
 

Basi watanitambua,

Nitaweka marapurapu kwenye nguo zangu upande wa tumbo ili nionekane nina kitambi. Halafu nitajipaka unga wa ngano usoni nionekane mweupe. Halafu nitakuwa ninafoka kiingereza kile che Shakespeare tu.

Je kwa hatua hizo nitapewa heshima hapo Mlimani City?
 



Yap mkuu nimekupata nashukuru sana kwa wazo lako zuri zaidi......Maana sikujua kama card yangu naweza kutumia hata bongo nashukuru mkuu kwa mawazo yako na maelezo yako mazuri!!
 


Yap mkuu nashukuru pia na wewe kwa maelezo yako pamoja na mkuu Capitol asante sana na nadhani tupo pamoja!!
 


I like this Naima..hii ndio dawa ya watu wenye dharau ambao wana-judge kitabu kwa kuangalia jalada itabidi niige huu mfano wako unafaa sana kuwakomesha wafanyabiashara wa Bongo wenye cutomer service zero.
Nimesoma hii mifano mbalimbali ya kero za Bongo jasho linanitoka manake nyumbani ni nyumbani ijapokuwa pangoni ila mambo mengine yanatia hasira!
 

Kufuatana na habari hiyo ya da Chemi....mimi sina haja ya kashfa, kwa hiyo sitonunua chochote hapo Mr. Price. Na nitawadokezea marafiki zangu kwamba kama wataenda duka hilo basi wajitayarishe na kashfa.
 

Watakufukuza....lolol
 


Sasa hii tuiiteje....maana sio Racism wala Tribalism....!!!!
 
Hizi ni exceptional cases jamani....si kila mahali utaenda ukumbane na adhaa hii, though nakubali customer care bongo iko chini hata ukicompare na jirani zetu wa Kenya!

Ni ukweli Next Level: Nikiwa nyumbani, kama naenda kula nyama choma, au naenda kuwapa offer washkaji kwenye baa ya mtaani, nakuwa treated like a King. Na sehemu nyingine nyingine. Tatizo ni pale inapokuja katika kuhitaji au kutumia huduma ambazo wa Tanzania tumezoeshwa ama tunadhani ziko pale kwa ajili ya raia wa nje tu especially kutoka mataifa ya magharibi. Mifano waliyotoa wadau hapa mingi inaonyesha hivyo...kuanzia Slipway, airport, clothing store zinazo offer high end products, na hii ya kwangu ya ATM. Ukiangalia huduma zote hizi utaona kutokana na hako ka trend na labda owners na wahudumu wa hizi biashara wana wa consider "westerners" kama target market yao na sisi wengine tunaonekana kama vibaka once we show up at these places. Ila kuna mkuu mmoja hapa ndani nafikiri ni Naima ameongelea kuhusu kudharauliwa na mfanya biashara wa kawaida tu tena sokoni kwa sababu ya item "zabibu" ambayo the merchant thought clients could not afford. Kwa hiyo nafikiri tatizo kubwa hapa ni lack of education na exposure. Kuna siku itafika Tanzana hizi biashara zitakuwa hazina wateja kwa sababu ya nguvu ya mteja na nguvu ya mawasiliano "internet". Kwenye nchi za magharibi, kama mtu anataka product fulani ama huduma fulani...hahitaji tena kwenda physically kwenye ile biashara...what they do, wana GOOGLE..reviews za ile biashara online. Wakishaona customers zaidi ya mmoja wanalalamika kwamba don't go there...then its a "Red Light" they go somewhere else. Hii imetokea kwenye biashara kama za maduka ya vitabu, apartments, uuzaji wa magari, na hata kwenye huduma za ndege. Wafanya biashara wengi wanasahau kwamba reputation za ubaya zinavuma zaidi kuliko reputation za uzuri, na siku zote..never underestimate anybody. Kwa wale wakazi wa Arusha...mnakumbuka enzi zile lile duka la LAST IMAGE lilivyokuwa...ulikuwa ukienda mswahili pale hawaongei na wewe, ngozi nyeusi pale tulikuwa tunaonekana kama "nyanya mbichi vile", they looked down on us. Leo hii I wish those bastards were sound in business ili niwaonyeshe kwamba sio watu wenye light skin pekee wanaoweza ku freaking afford Nike shoe ya $200.
We need to put a stop to this type of XPLOITATION. Raise your voice when you can. Believe me...it will change things.
 
Kila kitu ni kukijulia ,mtu hunyakanyaga bongo miaka kibao,ukifika unavamia na kuwaona watu bado ni wale wale uliowawacha kumbe inawezekana kabisa wapo mbele kimaendeleo kwani miaka yote uliyoondoka tayari wameshafika wageni wengi kutoka kila pembe ya Dunia ,aisee wewe umeishia hapo UK tu ,huku wanakuja watu kutoka mataifa mbali mbali na wanajumuika na wenyeji hivyo inawezekana kabisa wakakushangaa ,maana nchi imejaa vibaka na wewe unafanana navyo ,kwani vibaka mavazi yao ni ya bei mbaya ,hapo ndipo wanapokuchanganya na kukuona mwizi tu ,lazima wakuekee ubavu ,ili kama yapo mazungumzo yaishe ,si unajua tena nchi imekauka lazima utilie maji ili mimea ije juu,iyo lugha ulipoondoka ilikuwa haipo.
 
Bongo kunakeraa ukitaka heshima

1:Kuwa na Kitambi

2:Ongea kingereza

3:Kuwa mweupe(white man)

Ole wako uwe na sifa hizi, huku mfukoni kumenuna, halafu umuulize Mmachinga bei ya bidhaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…