Bongo Movie mnakera, kwanini hambadiliki?

Bongo Movie mnakera, kwanini hambadiliki?

Habar wapendwa,
Muda kidogo nimekuwa nafatilia kwa karibu sana kazi za wasanii wetu wa bongo,
Kiukweli zinachosha sana na mnatuchosha sisi watazamaji maan kazi za saiv hazina tofauti sana na za zaman maan zamani ilikuwa ukisoma maelezo ya Movie utakuwa ushaangalia film yote.

Tatizo langu kwenu ni kwamba mnashindwa kufanya mantaining ya Vocal na Background songs and effects kitu ambacho si sahihi kwani watazamaji wanahitaji kusikiliza maneno na cyo wimbo au background zenu kwa kuwa wanazo kwenye simu, flash, Pc, hard disk nk.

Kama haitoshi 95% ya actors wanaokuwa walinz wanakuwa wajinga wajinga au walemavu wa mikono nk hivi hamuoni hata kwa wenzenu wa Nigeria?

Suala wa wahusika kuvaa uhusika pia mnashindwa yaan mtu anapigwa rusasi anakufa alafu baada ya kudondoka chini anavuta nguo ili kitovu kisibaki wazi hiyo inakera sana.

Unakuta jambazi amevaa miwani myeusi na jaketi kubwa jeusi anavuta sigara au bangi na amekunja sura acheni kukalili maisha.

Nyie mshakariri kwamba siku zote watu ili wafanikiwe lazima waende mjini huo ni ushamba na nikupotosha jamii na kukatisha vjana walio vijijini tamaa kwani watajua ili wafanikiwe lazima waende mjini, huo ni upuuzi.

Unakuta mtu ana amka ile asubuhi amepaka make up, wanja, lipstick nk huo ni ushamba na haipo badilikeni na kama mkishindwa tutaendelea kuangalia film za nje hata kama ni ghari.

Akafu kwa mwendo mnataka mtusue hiyo haiwezekeni.

Ongeza kingine kinacho kukera.
umenikera wewe,badala ya kuwafundisha cha kufanya wewe unawasimanga mkuu!
 
Nimekumbuka yule jambazi msafi kavaa mask na risasi sasa yupo ndani kavua viati nje asichafue sakafu haya maigizo ata siyaangaliagi tena mara ya mwisho niliangaliaga movie ya YOLANDA
Asee mimi ya mwisho kuangalia ilikuwa ni "FAKE PASTORS"na sidhani kama wamewahi kutengeneza movie nyingine ya kiwango kile.
 
Bora kuangalia mizengwe,vituko show na jambo na vijambo ili uongeze siku za kuishi lakin co hao wasiojua nn wanakifanya, mwisho wa siku wanabana [emoji103]eti sanaa yetu haitulipii!!! nyie badiliken
 
Wewe utakuwa bongo movie
acha kuongea utumbo,mimi sio wa huko mkuu,naweza kuwa msaada wa vitu vizuri kwako coz nipo deep sana,siwezi kuangalia wala kuwa mshabiki wa bongo muvi,never in my life...
 
acha kuongea utumbo,mimi sio wa huko mkuu,naweza kuwa msaada wa vitu vizuri kwako coz nipo deep sana,siwezi kuangalia wala kuwa mshabiki wa bongo muvi,never in my life...
Kweli uko deep, hongera
 
Tatizo Lao wanafanya kazi kwa kulipua,
Filamu wanashoot wiki moja, inayofuatia sokoni tayari!
Hollywood kuna filamu zinatengenezwa mwaka mzima, ikija kutoka, huko Box Office Ni balaa!
 
Kwa wenzetu, mfano mzuri Marekani, ukiachana Na vipaji, asilimia kubwa ya waigizaji Ni mazao ya shule za sanaa,
Hapa kwetu Wolper ataigiza filamu mbili, baada ya hapo anatangaza kufungua kampuni ya filamu halafu yeye ndio director[emoji23][emoji23]
 
Ivi bado kuna wabongo magreat thinker wanakaa kitako kuangalia bongo movie tangu trailer hadi maandishi yanapanda.
Walahi hata kwenye basi siangalii, nautafuta usingizi hadi naupata.
 
Huyo anayesema tuwashauri, labda hutujui sisi wabongo, ukimshauri anakuona ni adui yake unataka kurudisha maendeleo yake nyuma
 
Tatizo Lao wanafanya kazi kwa kulipua,
Filamu wanashoot wiki moja, inayofuatia sokoni tayari!
Hollywood kuna filamu zinatengenezwa mwaka mzima, ikija kutoka, huko Box Office Ni balaa!
Wanakwambia hawana bajeti kubwa ya kutengeneza movie mnazotaka na kwa muda mrefu.
 
Alafu mtindo wa kuwaweka walinzi getini wanakuwa kama wachekeshaji unazingua sana
 
acha kuongea utumbo,mimi sio wa huko mkuu,naweza kuwa msaada wa vitu vizuri kwako coz nipo deep sana,siwezi kuangalia wala kuwa mshabiki wa bongo muvi,never in my life...
Unajuaje kuwa upo "deep sana" na unaweza kuwa msaada kwa wengine ambao baadhi yao wanskuzidi? Unapima IQ ya mtu kwa kuangalia comments?
 
Back
Top Bottom