Habar wapendwa,
Muda kidogo nimekuwa nafatilia kwa karibu sana kazi za wasanii wetu wa bongo,
Kiukweli zinachosha sana na mnatuchosha sisi watazamaji maan kazi za saiv hazina tofauti sana na za zaman maan zamani ilikuwa ukisoma maelezo ya Movie utakuwa ushaangalia film yote.
Tatizo langu kwenu ni kwamba mnashindwa kufanya mantaining ya Vocal na Background songs and effects kitu ambacho si sahihi kwani watazamaji wanahitaji kusikiliza maneno na cyo wimbo au background zenu kwa kuwa wanazo kwenye simu, flash, Pc, hard disk nk.
Kama haitoshi 95% ya actors wanaokuwa walinz wanakuwa wajinga wajinga au walemavu wa mikono nk hivi hamuoni hata kwa wenzenu wa Nigeria?
Suala wa wahusika kuvaa uhusika pia mnashindwa yaan mtu anapigwa rusasi anakufa alafu baada ya kudondoka chini anavuta nguo ili kitovu kisibaki wazi hiyo inakera sana.
Unakuta jambazi amevaa miwani myeusi na jaketi kubwa jeusi anavuta sigara au bangi na amekunja sura acheni kukalili maisha.
Nyie mshakariri kwamba siku zote watu ili wafanikiwe lazima waende mjini huo ni ushamba na nikupotosha jamii na kukatisha vjana walio vijijini tamaa kwani watajua ili wafanikiwe lazima waende mjini, huo ni upuuzi.
Unakuta mtu ana amka ile asubuhi amepaka make up, wanja, lipstick nk huo ni ushamba na haipo badilikeni na kama mkishindwa tutaendelea kuangalia film za nje hata kama ni ghari.
Akafu kwa mwendo mnataka mtusue hiyo haiwezekeni.
Ongeza kingine kinacho kukera.