Bongo movie waache utapeli, nani kawagawia majukumu ya kumsomesha mtoto wa Masogange?

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2016
Posts
8,658
Reaction score
15,793
Nyie Bongo movie, acheni utapeli. Mlichangisha rambi rambi kwa ajili ya kuwapoza wafiwa ili kipindi hichi cha majonzi ambacho hawawezi kutafuta hizo pesa ziwasaidie kusukuma siku.
Sasa nyie mmegeuza michango ya rambi rambi eti kuwa ada ya kusomesha mtoto akianza mwakani form one!
Hayo majukumu nani kawagawia? Nyie ndio baba wa mtoto?
Hizo pesa mkabidhini mzazi wa marehemu.
Hayo mambo ya kusomesha ikihitajika msaada wenu mtachangishwa na wenye nia watachanga.
Acheni kula rambi rambi za watu kijanja.
Basi kama kweli mngekuwa na mpango wa kusomesha mtoto, hizo pesa mngeshaziweka kwenye akaunti ya mtoto. Mnakaa nazo mpaka sasa hivi ili iweje? Au ndio mmejikopesha ili watu wakisahau mzitafune kimya kimya?
Najua vyuma vimekaza, ila sio kwa staili hii aisee!
Michango ya Masogange haipewi familia - Steve | East Africa Television
 
Huyo mtoto si alipewa ofa ya kusomeshwa bure hadi form four na tajiri mmoja hivi mmiliki wa shule daaah bongo movie kwa upigaji bana
 
Boss wa atlas aliahidi kumsomesha bure kwenye shule zake hadi form six, akasema akifaulu vizuri hadi chuo kikuu..... BONGO MOVIE WANATAKA KUPIGA DILI...
 
Hivi ni masogange yupi huyu anaongelewa mbona mm sielewi?
 
kwani baba ya mutoto nayo kwisha fariki?
 
Nyie Bongo movie, acheni utapeli. Mlichangisha rambi rambi kwa ajili ya kuwapoza wafiwa ili kipindi hichi cha majonzi ambacho hawawezi kutafuta hizo pesa ziwasaidie kusukuma siku.
Sasa nyie mmegeuza michango ya rambi rambi eti kuwa ada ya kusomesha mtoto akianza mwakani form one!
Hayo majukumu nani kawagawia? Nyie ndio baba wa mtoto?
Hizo pesa mkabidhini mzazi wa marehemu.
Hayo mambo ya kusomesha ikihitajika msaada wenu mtachangishwa na wenye nia watachanga.
Acheni kula rambi rambi za watu kijanja.
Basi kama kweli mngekuwa na mpango wa kusomesha mtoto, hizo pesa mngeshaziweka kwenye akaunti ya mtoto. Mnakaa nazo mpaka sasa hivi ili iweje? Au ndio mmejikopesha ili watu wakisahau mzitafune kimya kimya?
Najua vyuma vimekaza, ila sio kwa staili hii aisee!
Michango ya Masogange haipewi familia - Steve | East Africa Television
Steve, mrushie dingi wake jamaa wametushitukia, mpaka data wanazo! Tukubali yaishe.
 
Back
Top Bottom