Mkuu,
Suala hapa siyo kufanya jino kwa jino bali kusahihishana.
Mimi niipoanza kuiangalia tu nilihisi kukosekana kwa umakini katika kutunga hadithi na hata script.Nikawasamehe maana wengi wa hao vijana viwango vyao vya elimu ni vya chini sana kulinganisha na maendeleo ya kidunia.Nilishangaa nilipoona toka sinema inaanza Kanumba kakariri akina Plato, Shakespeare na wengineo ili ati kuipa makali hoja yake anayotaa kuijenga! Hapo ndio nikaona ujinga zaidi wa yule aliyetunga mchezo ...kwamba kama aliweza kuingiza dhana za philosophers hao katika kujenga hoja za "Moses" kudhalilisha wanawake ...basi kuna disconnect somehow..ama kwenye ubongo wake na uelewa au katika malezi yake na hali ya maendeleo ya sasa ya kujenga taswira nzuri ya maelewano, upendo, amani nk. Ila pia nilidhani huenda kadiri sinema itakavyoendelea basi ataelekea kuonyesha kurekebisha hali hiyo.... ila sikuwa na uvumilivu kuangalia mpaka mwisho maana ilini bore sana.
Ushauri kwa watunzi wa michezo na movies kama hii ya Moses, basi muwage mnatafuta watu wa kuwafanyieni review ya hizo hadithi zenu ili hata kama unataka kuonyesha taswira ya unyanyasaji isiwe kijinga kama ilivyo kwenye "Moses".
Pia waepuke kukariri sana maneno ya kiingereza kutoka kwenye vitabu..bali wakariri scripts za mchezo.Kwa msomaji wa vitabu hivyo vya kiingereza au mtu aliye fluent katika kiingereza kwa kweli hizi sinema za akina Kanumba wanaojikakamua kutema "ung'eng'e" kwa kukariri vitabuni unatia kichefuchefu badala ya kuwapa heshima! Wanatakiwa "wasizidishe"- wana overdo hadi inaondoa ladha.
La mwisho , basi sub titles nazo mtafute mtu makini awasaidie kunyoosha kiingereza maana nazo zinatia aibu.Mjue sinema zinaonyeshwa hadi nje ya nchi thanks to MNET. Itafanya watu wazidi kuamini kuwa Watanzania ni vilaza kumbe kuna watu waliotulia sana kwenye kila kitu.