Bongo Movies Imekumbwa Na Msiba, Staa Mmoja Ajitoa Uhai Mwenyewe

Ibrahim300

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2010
Posts
390
Reaction score
68
MSANII Victor Peter kutoka Bongo Movie afariki dunia kwa kujinyonga katika gesti moja iliyotambulika kwa jina la SAFARI JUNIOUR ilioko maeneo ya Kisosora huko mkoani Tanga.

Hapo pichani ni mwili wa marehemu ulivyokuwa ukipakiwa katika gari kupelekwa katika hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo,

Chanzo cha habari kiliieleza kuwa msanii huyo alikuwa katika harakati zake za kushoot filamu yake mpya ambayo alicheza kama muhusika mkuu katika filamu hiyo.
Kilichowashangaza wenzake ni kwamba filamu iliisha jana Jumatatu 27/01/2014 na story ilimalizikia Vicktor kufa kwakujinyonga matokeo yake leo alfajiri Victor akakutwa amejinyonga kweli na kuiaga dunia, Mpaka sasa chanzo cha kifo chake bado hakijatambulika
====================================


Chanzo:masainyotambofu
 
Mwenye picha yake atuwekee mana wengine hatumfahamu ati
 
Huyo marehemu alikuwa anatafuta umaarufu, aya tushamjua rest in peace
 
Vifo vimefululiza sana kwa wasanii, Mungu azidi kuwatia wepesi wote walioondokewa na wapendwa wao.
 
Sio kila msanii wa bongo muvi ni msanii wa bongo muvi.
 
Kumbe nami ni bongo movie aisee rip brother
 
Huyo marehemu alikuwa anatafuta umaarufu, aya tushamjua rest in peace
Khaaa!!!
Afu nakutafuta ujue.
Ingia kwa kijiwe mshenzi ukamuone kaka yako kafumwa live na gasho
 
Huyo marehemu alikuwa anatafuta umaarufu, aya tushamjua rest in peace

Ndugu si vyema kuleta mizaha kwenye misiba.....watu wana majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao........

Uungwana ni vitendo....
 
Chanzo cha kifo chake si "kujinyonga" ama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…