Bongo Record Vs Mj-Record:Kati ya P-Funk Majani na Master Jay nani alitengeneza ngoma kali zaidi?

Jaribu kuzunguka mabara barani hapa Tanzania ulinganishe wingi wa Gari kabila la Toyota v/s Makabila Mengine kama Nissan, Suzuki, Isuzu, etc. Hivi ndivyo ilivyokua wingi wa ngoma za Majani kwenye Top 10 v/s ngoma za ma producers wengine.

MJ ni mzuri pia, ila hakumfikia Majani.
 
P Funk ni ishu nyingine. Binafsi huwa nikiskilizaga tuu lile beat la 'nini mnataka mazee' huwa sithubutu kumfananisha P Funk wa kipindi kile na producer mwingine yoyote

the Legend☆
 
Pfunk yule mjinga moto wa kifuu, ile ada ya milioni 40 kwa mwaka pale International schhool of Tanganyika ilibidi tu wamfungulie studio Marekani maana alikuwa level za kina dre kabisa...Tukumbushane maajabu ya P funk majani
1.She got agwain @ngwea
2.kama unataka demu
3.nitoke vp-bwana misosi
4.Nikusaidiaje: professor jay
5.Mikasi
6.Nipo bize:Jaffarai

Hadi sasa hivi huyu mjinga hakuna wa kumpambanisha nae,Respect kwa master J na Mikamwamba pia kwa kulifanya game Liwe na ushindani.
 
Unajua gharama ya kufungua bongo records au unaropoka tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumshindanisha P na MasterJ ni kumkosea adabu...

Huyu jamaa ni hatari...

Umesikiliza

Party flan-Geez
Maisha ya madem-wandago
Usipime-Black rhyno
Birthday ya HK
Ratiba zetu-Snaa lee
Mida mibovu
Ndani ya club na Yote ni maisha??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina hakika kama Mtoto wa Geti kali ni ya Majani. All in all Majani hana mpinzani, labda MJ tungempambanisha na Mika Mwamba, kwa Majani tunamuonea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rekebisha namba moja, mtoto wa geti producer ni Mika Mwamba.
 
Anayesema mJ ni zaidi ya P Funk aje na vielelezo maana Afrika mashariki na kati yote inajua PFunk ni zaidi ya MJ.

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Bro usiseme hawa watu wawili.. Pa1 na kina bizman and like... Wanahitaji heshima kubwa kuliko tunavyowashindanisha hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…