Uchambuzi wangu:
Payne ni mzuri katika kuimba (sauti) lakini ki saana vile. Uchaguzi wake wa nyimbo ulikuwa mzuri sana. Kucheza na beats nina mrank wa mwisho (kky).
Kweli ushabiki wa kumpenda Payne ni psychological zaidi kuliko the intrinsic talents in him. Yaani ulichangiwa na 'mtu mgeni' asiye tegemewa kuimba kiswahili kilichonyooka kwa usanifu. Mfano ni mtu kutoa Afrika akianza kufanya maajabu katika say Ice / figure-skaters' dance, watu wanaweza kukupenda sana maana si kawaida sana.
Juu ya shindano la BSS kwa ujumla. Mshindi kwa kwanza yaweza kuwa sawa, pengine kwangu ningemweka wa pili lakini huyo mshindi wa pili I doubt kabisa! Ana sauti moja nzito tu hawezi kupanda juu na pia hata nyimbo zake si zinazogusa sana ukilinganisha na wengine.Yaani kuna waliokuwa wazuri sana kuliko yeye akina Chiby na Salum.
Majaji (ukiondoa Mzungu kichaa) wameonyesha upupu mkubwa kwa kutoa comments za kishabiki kuliko ile kazi ya ufundi ambayo kwayo imewaweka hapo. Wameshindwa kuficha pia feelings zao na kuonyesha waziwazi yule walitaka ashinde eti oh huyu ana mvuto na lazima ashinde oh mimi huyu ndiye wangu namba moja n.k , oh nitajiua huyu aki.......... . Hakika sikuamini kuwa maneno kama hayo yanaweza kutamkwa na Jaji aliyepewa dhamana na shughuli iliyodhaminiwa na makampuni mamilioni ya fedha.
Kibaya kuliko vyooote ni kumuruhusu Payne kushiriki toka mwanzo maana baadaye kawa na washabiki wengi na niseme kuwa performance yake ya mwisho ilikuwa kiboko sasa baadaye mkishasoma alama za nyakati eti mnajifanya kumweka kuwa wa tatu! lo aibu sana! yaani mlichemsha kabisa. Huyu hakustahili kufanya kazi hii bila work permit inayomruhusu kufanya kazi hii. hata kuna yule msichana pia aliyepewa zawadi ya moza Kiili house naye wakati anashiriki Master J alikuwa anamnyanyepaa kuwa anafaa akaimbe hizo nyimbo zake huko kwao ( Yaani naye Kiswahili kilikuwa mgogoro). Ninachosema ni kuwa hamna haja ya kuwaruhusu wageni kushiriki halafu mnawaponda kutoknana na uraia au matamshi yao au lugha zao!
BSS rudini kwenye meza mkae chini mjiulize kusudi la BSS ni nini? Sidhani kama mnakusudia kutufurahisha watazamaji au kunyanyua vipaji vya watu wowote duniani au ndivyo? Kama ni vkwa ajili ya vijana wa kitanzania basi: mdefine umri wa kushiriki na pia mtu awe raia wa Tanzania full stop.
Halafu next time 2011, fanyeni kweli. Rita wewe kaa pembeni kama Mkurugezi na Mratibu Mkuu, acha kabisa kuwa jaji. Jopo la majaji liwe na:
Producer mwingine mmoja (si master J tena) , Mtaalamu wa maonesho ya Sanaa mmoja, na waalimu wawili waliobobea katika Muziki acheni blabla ndiyo maana mtu akijaribu kuwasahihisha washiki kwa kutaja terminologies za music ninyi akina Salama mnambeza! Haya ni mashindano ya kutafuta mkali wa KUIMBA si kuuza tu sura wala kukata ma...... waka hata kucheza na vyombo ingawa hivyo vinatakiwa kuwa vikolombwezo kwenye kipawa cha msingi cha uwezo wa kuimba!
BTW Kwenye shindano lolote malalamishi hayakosekani lakini mnaweza kuyapunguza kama mtafaya kazi hiyo strategically na kwa kuwa wakweli!
Rita, make your mind and your project shall be of a success and of benefits to the Tanzanian youth!