Bongo Star Search Wapewa mwezi mmoja kumlipa mshindi wa BSS 2019

Robidinyo

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
4,043
Reaction score
8,686
Naibu Waziri Mhe.Juliana Shonza ametoa mwezi mmoja kwa uongozi wa Kampuni ya Benchmark Production inayoendesha mashindano ya kusaka vipaji kwa wasanii wa muziki maarufu kama Bongo Star Search (BSS) kuhakikisha wamemlipa mshindi wa kwanza wa mwaka 2019 zawadi yake ya milion 50.

==========


Na Shamimu Nyaki – WHUSM.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Juliana Shonza ametoa mwezi mmoja kuanzia Aprili 08, 2020 kwa Kampuni ya Benchmark Production inayoendesha mashindano ya Bongo Star Search chini ya Mkurugenzi wake Madam Ritha Paulsen kumlipa kiasi cha Shilingi milioni 50 mshindi wa kwanza wa mashindano hayo kwa mwaka 2019, Bw.Meshack Fukuta.

Naibu Waziri ametoa maelekezo hayo leo Jijini Dodoma baada ya kupokea barua kutoka kwa familia ya mshindi huyo iliyoeleza kutokutekelezwa kwa ahadi hiyo kwa takriban miezi minne sasa ilioanisha utaratibu wa malipo hayo kuwa milioni 30 ni kwa ajili kutengeneza kazi za muziki na matangazo kwa kipindi cha mwaka mmoja na milioni 20 ni ya kukabidhiwa mkononi ambapo Mhe. Naibu Waziri amesisitiza makubaliano yote yalioanishwa kufanyiwa kazi.

“Mimi kama mlezi wa tasnia ya Sanaa ambaye pia nilikua mgeni rasmi siku ya fainali nimesikitishwa sana na malalamiko haya, hivyo naitaka kampuni ya Benchmark kutekeleza ahadi hiyo na wasipofanya hivyo ndani ya muda huo, Serikali haitasita kufungia mashindano hayo”, alisema Mhe.Shonza.

Mhe. Naibu Waziri ameongeza kuwa Wizara iliwasiliana na uongozi wa Benchmark kuhusu malalamiko hayo mbapo Kampuni hiyo ilieleza kuwa imeshindwa kumlipa msanii huyo kutokana na viongozi wa Kampuni iliyodhamini shindano hilo ya Startimes kuwepo nchini China na kushindwa kusafiri kuja nchini kutokana na uwepo wa ugonjwa wa Corona.

Hata hivyo Mhe.Naibu Waziri ameleeza kuwa Wizara iliwasiliana na uongozi wa Startimes ambao umekiri kuwa umeshalipa fedha kwa Kampuni ya Benchmark tangu mwezi Januari 2020.

Aidha, Mhe.Shonza ameitaka kampuni hiyo kuhakikisha inamtengenezea msanii huyo wimbo bora pamoja na kuufanyia matangazo ya kutosha katika kipindi cha miezi miwili kuanzia leo pamoja na kuwasilisha nakala ya mkataba wa washiriki waliofikia hatua ya kumi bora ndani ya wiki moja kuanzia leo machi 08,2020.

Katia hatua nyingine Mhe.Shonza ameliagiza Baraza la Sanaa na Taifa (BASATA) kusimamia utaratibu wa uaandaji wa mashindano mbalimbali ikiwemo kuwepo kwa mikataba kati ya wasanii na wanaondesha mashindano au shughuli yoyote ya sanaa na wasanii pamoja na kuhakikisha ahadi wanazopewa washindi ikiwemo zawadi zinakuwepo na zinakabidhiwa kwa wahusika mara baada ya mashindano.

Kwa upande wake Bw.Meshack Fukuta mshindi wa shindano hilo kwa mwaka 2019 ameishukuru Serikali kwa namna ambavyo imechukua hatua katika malalamiko yake ambapo ameahidi kufanya juhudi katika Sanaa yake ili kuitangaza nchi vizuri ndani na nje ya nchi pamoja na kujipatia kipato kupitia kipaji hicho.
 
Kitambo sana hapo wamepushana na mshindi ndio maana yanajulikana sasa... Muulize Kala Jeremiah aliambulia nini

Jr[emoji769]
Huu ni uhuni kama vipi serikali ihakikishe dogo anapewe hela yake,ikishindikana BSS ifutwe.

Ila Madam Rita kampuni yake ya Benchmark nayo inatembelea rim,lile deni lake na TRA sijui wameshamalizana.
 
Hakuna hata siku moja mshindi wa BSS aliwahi kulipwa kamili.. Na mbaya zaidi wanahakikisha wanambana mshindi kwa mwaka mzima na kumdhibiti kwenye chochote anachopanga kufanya
Huu ni uhuni kama vipi serikali ihakikishe dogo anapewe hela yake,ikishindikana BSS ifutwe.

Ila Madam Rita kampuni yake ya Benchmark nayo inatembelea rim,lile deni lake na TRA sijui wameshamalizana.

Jr[emoji769]
 
Niliwahi sikia hili sema enzi zile si hakuna mitandao kama sasa hivi na Shonza huyu ni wa kwao Mbeya!Madam pole sana punguza huzuni za msiba mlipe deni kaka wa watu
Hakuna hata siku moja mshindi wa BSS aliwahi kulipwa kamili.. Na mbaya zaidi wanahakikisha wanambana mshindi kwa mwaka mzima na kumdhibiti kwenye chochote anachopanga kufanya

Jr[emoji769]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna hata siku moja mshindi wa BSS aliwahi kulipwa kamili.. Na mbaya zaidi wanahakikisha wanambana mshindi kwa mwaka mzima na kumdhibiti kwenye chochote anachopanga kufanya

Jr[emoji769]
Kwenye mkataba kuna kipengele cha kumzuia mshindi kuzungumza na media yoyote kwa kipindi cha mwaka mzima baada ya kushinda... Kuna mtu aliwahi niambia hili
 
Naskia walikua hawalipwagi zote mtu akipewa kidogo anaridhika plus umaarufu baasi!sasa huyu naona hajapewa hata 100.
Inabidi mana kama alizowea kuwahadaa vijana kwa vipesa mbuzi akijua akitoka hapo inabaki siri safari hii wamebugi.

Na usawa huu Milioni 50 si pesa ya kitoto. Au ndio anazo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…