bongo star search

bongo star search

Iko bomba, wanajitahidi kuwa creative ila washiriki naona kama hawana viwango vya kutosha uimbaji,, waimbani bora hawakujitokeza mwaka huu
 
Mi nimeipenda ila yule mzungu alikuwa kivutio sanaa mwaka huu, bahati mbya juzi sikumuona kabisa kwenye top 20, sijui tatizo nini kama kuna mtu mwenye habari ya kutoonekana mzungu hii juzi atujuze.
 
mi naona kama ni biashara nzuri sana kufanya coz sponsors wako kibao, so naichukulia iko kibiashara zaidi, ni mtazamo wangu tuu.
 
Naona wameiga Big Brother zaidi hadi uhalisia umepotea. Ni mtazamo wangu tu jamani.:A S thumbs_up:
 
Mi nimeipenda ila yule mzungu alikuwa kivutio sanaa mwaka huu, bahati mbya juzi sikumuona kabisa kwenye top 20, sijui tatizo nini kama kuna mtu mwenye habari ya kutoonekana mzungu hii juzi atujuze.
Mzungu amerudi na yule Baby Johnshon a.k.a. Mwenye T-shirt nyekundu:biggrin1: ametoka baada ya kushindwa adhabu ya kuosha vyombo wiki nzima. so akaamua afungashe virago vyake mi nafikiri ana ugonjwa wa akili kwa sababu mambo aliyokuwa anafanya sio ya mtu mwenye akili timamu. Binafsi sikumpenda tangu siku nilipomuona amevaa T-shirt nyekundu wakati wanajadili mambo ya kazi anajidai hawezi kuosha sahani ya mtu ata-manage his only staff. nilimuona mkosefu wa adabu na haeshimu wenzake anajiona yeye ndio mwanzo mwisho.

La muhimu BSS wajitahidi wafikie anglau viwango vya tusker project fame au na kuzidi hapo maana BSS ikiisha na washiriki hatuwasikii wakivuma.
 
Dada, Rita, fanya maamuzi magumu kwa wakati.

Huyo Mzungu Mshiriki (Joseph?) kama hana work permit inayospecify categorically kuruhusiwa kufanya shughuli kama hizo (profitable business in Musical performances) afadhali mmwombe ajiondewe si kwa sababu za ubaguzi bali kwa kutii sheria za nchi. Hatuwezi kusema kuwa anajifurahisha, maana anaweza kuchaguliwa kubaki na mwishowe akishinda atatangazwa Mshindi na atakula bingo and that is doing business!
 
Yule mzungu anaimba vizuri zaidi kuliko hata watz wengi kwani inaonyesha ana ujuzi fulani wa muziki.

Mimi sioni kwamba ni tatizo kwani ndiyo kwanza imeanza na mbali na hiyo zawadi na labda future yake kuna lipi jengine ambalo ni profitable?
 
''Mi nimeipenda ila yule mzungu alikuwa kivutio sanaa mwaka huu, bahati mbya juzi sikumuona kabisa kwenye top 20, sijui tatizo nini kama kuna mtu mwenye habari ya kutoonekana mzungu hii juzi atujuze.''

Labda amekamatwa na Uhamiaji
 
Mi naona bado viwango viko chini sana kulinganisha na tusker project fame. Sioni pia kama majaji wanawasaidia kujitambua viwango vyao. Kwa muda BSS ilipoanza nilitegemea sasa hivi ingekuwa imeimarika sana lakini bado iko kama ilivyoanza au chini zaidi. kama alivyo comment m2 m1. Iko kibiashara zaidi hasa ukizingatia hizo sms za mapendekezo ambazo zinaingiza hela sana. Chap chap wameshajenga jengo la nguvu kweli kweli. By the way hilo jengo liko wapi hapa bongo
 
inachefua hasa inazidi kupoteza umaarufu imagine siku ya fainali majaji walivyolewa madamu rita alikuwa nzwii!! huyo master hata aliyokuwa akizungumza siku ile ukimuuliza leo hakumbuki!!! hawako serious hawa watu!!!!!! na hao wadhamini wao wangeleta hizo fedha kwa watoto wetu vijijini wanaokaa chini na kusoma na njaa!!!! hovyo!!!!
 
Back
Top Bottom