Hii picha nimeitoa kule kwa Michuzi. Nimeiangalia mara kibao na kuanza kujiuliza maswali kem kem. Moja ya maswali niliyojiuliza ni nani abebe lawama za uchafu huu?
Ni viongozi wetu (wa ngazi zote)? Ni wananchi watupao takataka ovyo ovyo? Au ni Ndivyo Miafrika Tulivyo? Nimefikiria weee...nimewaza weeee...sipati jibu hadi nikaanza kuona kizunguzungu!
Nina uhakika kabisa hapo karibu na huo uchafu kunatoa harufu. Lakini hebu mwangalie huyo dogo alivyominya hap utadhani yupo bustanini akipunga upepo. Mwenzio wala haonyeshi kukerwa na huo uchafu.
Halafu mcheki huyo jamaa aliyebeba sijui ungo (labda njegere, karanga, korosho, who knows what) huo. Hapo ukimsimamisha mwenzio atakuuzia bila hata ya kuonyesha kukereka na uchafu huo...
Why us jamani? Yaani hata usafi unatushinda? Yaani kuweka mazingira unayoishi katika hali ya usafi na yenyewe yanahitaji uwe na akili kama Einstein? Good Lord!!!
Hiyo picha iko wapi?
Nilifikiri ni mimi tu nisiyeiona!? halafu kuna mwananchi ametoa thanks duuu
Utasikia tu maskini...hatuna pesa ya kigeni!
Wakati huo huo tunaagiza mashangingi 1,000 na bei ya shangingi moja ni kati ya milioni 100 na milioni 150!!!
Ingetia moyo sana katika sherehe za miaka 32 ya CCM Kikwete na uongozi wa juu wa CCM kuwahamasisha na kushiriki katika kusafisha uchafu uliokithiri katika miji yetu mbali mbali ikiwemo Dar.
utakuta kampuni iliyopewa tenda ina gari moja bovu kabisa,unajiuliza ilipataje tenda.
...bro BaK, si unakumbuka Lowassa alipoingia madarakani (u-pm) ilipita safisha safisha ya nguvu, na mabustani yakaanza kupendeza?
uchafu upo ndani ya mioyo yetu. Fikiria hata Cherrie Blair alivyoshangazwa na poor sanitation inayopelekea magonjwa ya mlipuko kama Kipindupindu, halafu mijitu inakenua meno ikitanguliza lame excuses.
Hivi kweli panahitajika mpaka aje Kikwete ndio sie wananchi tutanawa mikono kabla ya kula, au kuchemsha maji kabla ya kunywa, ama kufukua mitaro ilozibwa na mifuko ya plastiki tunayoitupa wenyewe wananchi ilhali tunajua plastiki haiozi?
Kwakweli maendeleo yatakuwa magumu sana kufikiwa iwapo tutabakia tunailaumu serikali itufanyie kila kitu, wakati tumepewa akili ya kufikiria tukichimba shimo, tunaweza zichoma hizo taka!
Hiyo picha ilipigwa siku gani?