Wapo christians waaminifu piaHii mada nlikuwa naijadili jana na jamaa yangu mmoja,alikuwa anatetea unachokisema mimi nilikuwa napinga.Wewe ni mkristo na muaminifu kwa mujibu wa maandishi yako,mimi ni mkristo na muaminifu kwa jinsi navyojijua.
Ni story TU sio wote wanasoma albadiri dhulma ni dhambi kubwa Sanaa ukiswali TU na ukaomba Dua aliyekudhulumu analipa au ht ukinung'unikaKwaiyo albadili huwa Ni story za kufikirika au vipi?
sio kweli, Waislamu wanafundishwa wazi wazi bila kupindisha maneno kuwa Ipo siku ya mwisho (siku ya hukumu) ambayo itakuwa ngumu sana kuliko binadamu yeyote anavyoweza kufikiria!Sio kwamba ni waaminifu Ila wanajua Kuna gharama kubwa italipwa ukienda nje ya mstari.
Kila shekhe anajua madhara ya Albadri.
Baba la baba mzee Mohamed hawezi kupita na hela za mama lao Faiza la sivyo kesho ataanza kuokota makopo hapo gerezani
Wapo ambao sio waaminifu ila wasioshika dini na wasiomjua MunguAlafu kuna waislam sisi hapa..
Wee jichanganye tuu [emoji851][emoji851][emoji851]
Rafiki yangu alidhulumiwa kiwanja na mchungaji wake Wa kanisani daahh...aliumia Sanaa na hakutegemea Kwa kweli ..Mpk Leo almost 7yrs hajamaliza deniJe hauoni wakufanana na sheikh ni mchungaji? Je ushawahi kufanya biashara na mchungaji?
Sheikh alikula hela za mauzo ya kiwanja cha marehemu ndugu yake akamdhulumu mjane yule milion 13Rafiki yangu alidhulumiwa kiwanja na mchungaji wake Wa kanisani daahh...aliumia Sanaa na hakutegemea Kwa kweli ..Mpk Leo almost 7yrs hajamaliza deni
Aisee[emoji848]Usiwasifie sana. Ni mafunzo ya dini yao yanawafanya wawe hivyo na hasa kwenye biashara.Kuna Muislam mmoja alikuja kwangu Kununua kitu kwenye duka langu kapungukiwa Shillingi 500.Nikamwambia aende ataniletea kesho yake akakubali lakini hapohao akampigia simu mtoto wake akaja pale dukani ana umri kama miaka 21 hivi. Nilishangaa sana alipomfahamisha kuwa anadiwa 500 ataileta kesho yake lakini kama amri ya Mwenyezi Mungu itapita na akatwaliwa kabla ya hiyo kesho kufika,basi mtoto abebe hilo deni.Wakakubaliana wakaondoka.
Kwa bahati nzuri kesho yake ilifika na Mzee mwenyewe aliileta ile fedha.
Sikuami kama ni mambo ambayo yanapatikana katika dunia hii lakini katika kuuliza nikaambiwa ni waoga sana linapokuja swala la klumwogopa Mungu.
Hayo yapo na hakuna aliyebisha ila wengi waaminifuSheikh alikula hela za mauzo ya kiwanja cha marehemu ndugu yake akamdhulumu mjane yule milion 13
Binafsi Ni mkristo mkatoliki na Niko kwny biashara Zaid ya miaka 18 sasa
Ila kiukweli jamii ya waislamu hasa wa Zanzibar, somali au bara wale wazee wa swala 5 Ni waaminifu sijapata kuona.
1. Kuna msomali mmoja mwaka 2008 ile bado mchanga biashara, hanijui simjui ndo mara ya kwanza nanunua mzigo kwake, ila aliniamini akanikopesha mzigo wa pesa ndefu kwamba nikishauza ntamtumia pesa zake. Kweli nikamrejeshea kwa uaminifu na tunafanya biashara vizur Hadi leo. Hatujawai dhurumiana hata Senti.
2. Kuna mpemba mmoja ni nafanya nae biashara yuko nje ya nchi mwaka wa 4 huu, simjui hanijui, Zaid ya calls na chats kupitia wasap, nilitumiwa TU namba kupitia mtu baki, ila uwa namtumia pesa ananitumia mzigo na mizigo mingine ananikopesha. Tunafanya biashara Safi kwa upendo wa Hali ya juu utadhani mtu na ndugu Yake.
3. Kuna ustadh mmoja msambaa anamiliki mpesa matawi kibao Hapa k'koo mengine kibaha na mbezi . Ila matawi yote mengine yanayosoma till za jina lake, kaweka mashehe wenzie waliokutana na kufahamiana mskitini na wanayamiliki na kuendesha 100% ili kutunza familia zao. Ustadh yeye kabaki na matawi 2 tu anayoyamiliki 100%.
4. Kuna mfanyabiashara mwenzangu Ni mrangi wa dodoma ila Ni shehe swala 5. Yeye tangu nimjue hajawahi kukopa pesa ya riba benki yoyote Hapa nchini, kwake riba Ni haramu.
Akiwa na shida na pesa au mtaji umeyumba anaazima kwa mashehe wenzie uko mskitini na kurejesha Kama zilivyo.
5. Kuna mwislam mmoja mrangi Yuko Moro, nmemtumia sana kipind flan nafanya biashara ya nafaka. Huyu Tumejuana TU barabarani Tena kijiwe Cha draft, nikawa namtumia pesa ananikusanyia nafaka na kupakia kwny fuso na kunitumia dar. Ila mpaka naacha ile biashara, hajawahi nidhurumu hata Senti moja. Tuna maelewano mazur Hadi Leo.
6. Mwingine Ni shehe mmoja msomali agent binafs wa magari used yuko japan, ila ana wateja wengi Tanzania ,Zambia Hadi Uganda na Congo. Mteja analipia,gari inasafirishwa Hadi Uganda,Zambia kwa uaminifu mkubwa.
Anasifiwa Sana uaminifu kule kwny uzi wa magari used japan.
7. Mwingine Ni mpemba mmoja shehe anajiita Abdulwahid Yuko zanzibar anauza tv Toka Dubai, anasifiwa Sana kwa uaminifu kule Uzi wa wauza tv. Nami pia nishafanya nae biashara,hanijui simjui, Nikamtumia pesa ndefu akanitumia mzigo wangu Safi kabisa nikaupata Bila longolongo.
Mifano Ni mingi Sana,
Ila nikiri waislamu wako mbali Sana kwenye suala zima la uaminifu.
Nawasilisha[emoji1431]
Kweli kabisaWapo ambao sio waaminifu ila wasioshika dini na wasiomjua Mungu
Tunapoongelea dhulma mpk kumzini mke wa mtu ni dhulma piaIlo kwa muislam mwenye dini kwenye pesa ondoa shaka ila nikutahadhirishe usije ukaamini same kwenye kumwachia mkeo huko wengi hua wadhaifu sana ila kwenye pesa dhurma hua tunaogopa kupita maelezo.
Inamaana umetumia kipimo gani kusema wengi ni waaminifu au ushafanya sensa ya nchi yote ?Hayo yapo na hakuna aliyebisha ila wengi waaminifu