Babu Kijiwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2010
- 4,830
- 4,729
Habari zenu wakuu, Sheria za mtandao nchini zinawataka watengeneza maudhui wote kusajili channels zao TCRA bila kujali ni maudhui gani wanatoa, jambo hili limefanya baadhi ya watu walioendelea kutoa maudhui bila kusajili kujikuta mikononi mwa vyombo vya ulinzi na usalama, mfano yupo kijana anaitwa MC Warioba ambaye channel yake iliweka videos za sherehe mbalimbali alizo hudumu lakini alikamatwa kwakuwa hakusajili, pia MC pilipili alishawahi kukumbana na mkono wa sheria kwa kosa la kuendesha channel bila kusajili.
Nimeona channel ya Bongo Zozo kule Youtube na nilipo angalia orodha ya channel zilizo sajiliwa na TCRA nchini Tanzania, sikuona channel ya Bongo Zozo, swali ni je Serikali inaruhusu baadhi ya watu kuendesha shughuli zao bila kusajili? Kama jibu ni hapana kwanini wanawafumbia macho baadhi ya watu?