- Tunachokijua
- Boniphace Jacob (Boni Yai) ni mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kanda ya Pwani lakini pia amewahi kuwa Meya wa Kinondoni.
Mnamo mwezi Mei 18, 2025 mwenyekiti huyo wa kanda ya Pwani alifanya mkutano na waandishi wa habari pamoja na viongozi wa CHADEMA wa mikoa na wilaya ambapo pamoja na mambo mengine alitumia fursa hiyo kutoa ufafanuzi wa kina dhidi ya masuala mbalimbali yanayoendelea kwenye chama hicho ikiwemo sakata la kundi la G55 wanaohama chama wakidai kubaguliwa.
Madai
Katika mtandao wa Facebook imechapishwa taarifa inayodaiwa kuchapishwa na Nipashe kuwa Boniface Jacob (Boni Yai) kupitia mkutano huo alisema msimamo wa ''No reforms, No election" kwa sasa umesitishwa.
Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (key word search) ulibaini kuwa taarifa hiyo haikuchapishwa katika kurasa rasmi za Nipashe, bali ni chapisho lililotengenezwa na wapotoshaji.
Aidha kupitia mkutano wake na waandishi wa habari alikanusha madai ya baadhi ya wanachama waliojivua uanachama wakidai ajenda ya No reforms No election walikuwa wanatania/hawamaanishi ni uongo na kumdhalilisha aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe kwani ajenda hiyo ilikuwa ni maamuzi ya Chama.