Kwa nini wanatumia nguvu zote hizo kuonyesha kuwa wanamkubali Mbowe? Wanachopaswa kufanya ni:
1. Lissu, Heche na Mnyika kukiri kuwa Mbowe binafsi alichafuliwa sana wakati wa uchaguzi hususan kwenye suala la kulamba asali.
2. Kukiri kuwa kuna walio muunga mkono Mbowe ambao hawakutendewa haki baada ya uchaguzi. Wanapaswa kuwaomba msamaha watu kama Sigrada. Kusema kuwa madai yao sio ya kweli kwa sababu yeye hayajampata ni upuuzi. Avaae kiatu ndie anaejua wapi kina mbana.
3. Watambue mchango wa G-55 kwa Chadema hata kama baadhi yao wamehamia chama kingine cha siasa.
4. Kuacha na kuwasihi wafuasi wao kuacha kutumia kejeli na matusi dhidi ya wasio unga mkono uongozi uliopo na muelekeo wa chama chao. Kama vile Boni mwenyewe asivyotaka kuitwa msaliti kwa kumuunga mkono Lissu, wao nao wasiitwe wasaliti kwa kutofautiana na Lissu.
Boni asipofanya hivi, yote anayofanya yataonekana kuwa ni unafik na kujikomba kwa utawala mpya. Amuige Sugu ambae hatujamsikia akiwasemea ovyo G-55 ingawa anaunga mkono uongozi uliopo na sera zake.
Chadema inatakiwa kuwa na platform ndani yake ambayo itasikiliza na kushughulikia malalamiko ya wanachama wao. Watu kama Aisha wamesema wazi kuwa waliwasiliana na Heche na Mnyika kuwaelezea concerns zao lakini walipuuzwa. Wanatakiwa kubadilika na kuonyesha unyenyekevu kwa wanachama wao bila kujali tofauti zao.
Amandla...