Pre GE2025 Boni Yai: Mbowe utabakia kuwa Jenerali na kiongozi wangu siku zote, Nitakuwa tayari siku yoyote kupokea majukumu kutoka kwako hata nje ya siasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wachumia tumbo matumbo joto
 
Tatizo waliamini wanashinda ndio maana bado wanaweweseka. Hata tweet ya leo ya mbowe inaonyesha huyu mzee ana maumivu.
 
Unamsujudu mtu halafu unaishia na nukuu kwamba humsujudu mtu.

Contradiction.
Ndio tatizo la mtu mzima kuwa Chawa!! Hana tofauti na Mwijaku; yote hiyo sababu ya njaa. Huyu anajifanya mnyakyusa lakini nadhani ni Kabila moja na chawa Mwashambwa . Wanyakyusa ni watu imara sana a’ la Mwabukusi 😳😳
 
We protect the Purpose and not a person"πŸ’ͺπŸΏπŸ‘ŒπŸΏ
 
Kama kamanda wa anga asingekuwa kiongozi Bora na SI Bora kiongozi chama chetu cha CHADEMA kisingukuwa tishio kubwa Hadi Leo kwa CCM kiasi cha kuifanya CCM nserikali yake kuiba uchaguzi wote mara mbili 2019 to 2020 na 2024 to 2025.
 
Anaandika Boniface Jacob kupitia X.

Freeman Aikaeli Mbowe

Kwangu umekuwa siyo tu kiongozi wangu wa chama bali ni mwalimu, mwanafalsafa,mkufunzi,mzazi,mlezi na rafiki wa kweli. Wewe ni mfano wa kuigwa

Nashukuru kwa kuniamini na kunipa jukumu la kuwa Mwenyekiti wa kampeni zako katika uchaguzi mkuu wa chama January 2025.

Unajua,umeona, umesikia na umeshuhudia hadi sekunde ya mwisho nilivyo simama na wewe na nilivyojitoa kwa hali na mali kufanya jukumu lile zito lililokuwa mbele yetu lakini bahati haikuwa upande wetu.

Sikuwahi kufikiri au kudhani ipo siku mwalimu wangu wa siasa atanipa mimi mwanafunzi wake kazi ya kusimamia kazi yake ya siasa

Hata hivyo nachezwa na machale, ninavyokufahamu itakuwa ulikuwa kuna kitu ulitaka nijifunze kwenye majukumu yangu ya kusimamia kampeni zako.

Moja ya funzo kubwa na la ajabu nitalikumbuka daima katika uchaguzi huu ni pale uliponieleza

"Watu wako rasmi uliowapa jukumu la kufanya kampeni wasifanye Jambo lolote bila idhini yako, na pia katika kila jambo tutakalofanya tusikiumize chama kwa namna yoyote ile au kwa kisingizio chochote kile"

Mapenzi yako kwa CHADEMA na wanachama wa CHADEMA ndiyo yalinifanya nikubali kubeba Jukumu hili zito,ulistahili "support" yangu hata kama Dunia nzima ingekusaliti kisiasa na kukugeuka bado mimi ningebakia peke yangu kuwa pembeni yako.

Ndiyo maana nilipoona kura zetu hazijatosha sikuhitaji ruhusa yako kusaini fomu ya matokeo kuwa Mheshimiwa Tundu Lissu ni mshindi

Na nilipokujulisha matokeo ya uchaguzi kuwa wajumbe 482 walihitaji uwe Mwenyekiti wao na wajumbe 513 wameamua ukapumzike, watu wengine uliokuwa nao chumba cha VIP wakiwa wanalia wewe ulinyanyuka ukanikumbatia kisha ukachukua simu yako ili kupongeza na kukubali matokeo kupitia ukurasa wako wa X na kuanza kujadili swala la kurudi ukumbini tayari kupokea matokeo rasmi.

Soma Pia: Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA 2025: Tundu Lissu ashinda nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa kwa Kura 513 sawa na 51.5%

Hili ni somo kubwa sana kwangu.

Wewe utabakia kuwa Jenerali wangu wa kweli na kiongozi wangu siku zote. Nitakuwa tayari siku yoyote na mahala popote kutumwa au kupokea majukumu kutoka kwako hata nje ya siasa.

Nakutakia maisha mapya nje ya majukumu makubwa ya kisiasa.

"We protect the Purpose and not a person"

Boniface Jacob (Boni Yai)
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani
Thursaday, Jan 23, 2025.

 
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ Kumbe kuna watu walilia Mbowe kushindwa?

Watakuwa kina John Mrema hao.

Ila mwamba inaonekana alikuwa anawapa mshiko sana wapambe wake
Mbowe mtu safi saana roho ya kizungu.

Mtu mwenye choyo kama Lissu hawanaga utu kabisa.

Mbowe alivyosalitiwa kama unaipenda chadema na Tanzania lazima usikie maumivu.
 
Huyu ndio chawa Sasa,anatambua nafasi ya bosi wake sio unasapoti kibaraka na mtu asiyeaminika kama Lisu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…