- Source #1
- View Source #1
Ndugu zangu Watanzania,
Unaweza kusema ya kuwa Mheshimiwa Boniface Jacob ameamua kujiweka pembeni ya ulingo na masuala mazima ya siasa za CHADEMA na kuamua kujikita kwenye shughuli zake binafsi za kijasiriamali.
Ambapo Mheshimiwa Jacob ambaye ni Mayor wa zamani wa Ubungo ameonekana akiwa katika chumba au ukumbi wenye Trei za mayai Mengi sana. ambayo ni biashara amekuwa akiifanya kwa muda mrefu sana na ambayo imeonekana kumpatia matokeo chanya na faida kubwa sana.
Amepongezwa sana mitandaoni na watu mbalimbali na wa vyama tofauti tofauti kwa juhudi zake kubwa na kuwa mfano wa Kuigwa katika mapambano ya kukabiliana na umaskini na kujikwamua kiuchumi.
Wengi wamemsifu na kusema kwa hakika anapaswa kupewa sapoti na kuungwa mkono sana katika biashara yake hiyo .kwa sababu kupitia yeye bila shaka kuna vijana hata kama siyo wengi wataweza kupata ajira, ujuzi wa biashara hiyo pamoja na kusaidia wengine kuwapa ujasiri wa kuinuka na kuanza biashara.
Hata Mimi Lucas Mwashambwa ninamuunga Mkono Mheshimiwa Boniface Jacob nakuomba Mungu amsaidie sana kufanikiwa kibiashara na kiuchumi. Mimi sinaga wivu kwa mtu anayepambana na kufanikiwa kwa jasho lake mwenyewe. Mimi sina roho ya kwanini wala wivu wa kimasikini. Mimi napenda sana kuona mtu akifanikiwa kwa sababu najua anasaidia kuwapa moyo na hamasa watu wengine.
Lakini mwisho naomba nimkaribishe sana kujiunga ndani ya CCM. mahali ambapo anaweza kutimiza ndoto zake za kufanya siasa zenye matokeo chanya Kwa Taifa letu. Kwa sasa CHADEMA imeshatekwa nyara na wanaharakati uchwara na watu wasioelewa wala kujua misingi ya CHADEMA na wala hawajui gharama iliyotumika ya jasho na Damu kuifikisha hapo ilipo.
Mwenyekiti wa chama ndio huyo lissu haeleweki wala hana mbele wala nyuma wala haelewi afanye nini zaidi ya kuropoka ropoka tu na kutoa kauli za hovyo Hovyo tu zenye kutaka kuivuruga Nchi yetu. Karibu sana CCM Mheshimiwa Boniface Jacob. CCM ni mahali salama sana na mahali tulivu. wewe utafanya siasa na biashara zako zitafanya vizuri sana maana utakutana na akili kubwa huku ambazo zitakupa njia,kukuongezea maarifa na muongozo wa namna ya kukuza biashara yako zaidi na zaidi na hata kuipeleka hata nje ya mipaka ya Tanzania kwa mafanikio zaidi na makubwa.
Utafurahi sana na utakuja kunishukuru hapa jukwaani. Utapewa tenda kubwa kubwa ya kusambaza bizaa zako na utapewa njia ya kuliteka soko kubwa zaidi . Njoo CCM acha kujichelewesha huko Kaka yangu. acha kuishi mahali ambapo watu hawathamini mchango na thamani yako na hawatambui umuhimu wako. Njoo CCM Kaka na wala hutajutia.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

- Tunachokijua
- Bila shaka umewahi kusikia jina la Boniface Jacob likitajwa mahali, au pengine umewahi kukutana na jina hili mtandaoni wakati ukiperuzi vitu vyako.
Kwa wasiomfahamu kabisa, Boniface Jacob, au maarufu kama Boni yai ni kada maarufu wa CHADEMA na Meya wa zamani wa Ubungo.
Siku za hivi karibuni zimekuwapo taarifa zinazomhusu, zikisema ameanza ufugaji wa kuku na kwamba kaachana na CHADEMA. Tupate undani wake.
Uhalisia wa Taarifa
Ufuatiliaji wa Kimtandao iliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa taarifa hii si ya sasa, imekuwepo Mtandaoni kwa kipindi kirefu. Aidha, Boniface Jacob hajawa active mtandaoni kwa muda mrefu sasa tangu kuisha kwa Uchaguzi wa CHADEMA uliomuweka madarakani Tundu Lissu baada ya kumshinda Freeman Mbowe mapema mwezi Januari, 2025.
Mathalani, kwa kutumia nyenzo ya Google Lens, imeonekana kuwa picha hii ilichapishwa Mtandaoni kwa mara ya kwanza Machi 28, 2023 na Boniface Jacob mwenyewe baada ya kupokea mayai hayo kutoka shambani kwake.
Aliandika “Boniyai Company Ltd tumeshusha Mzigo kutoka Shambani leo Asubuhi, ili kuhakikisha Kipindi hiki cha Kwaresma na Ramadhani Mayai hayakosekani.
Karibuni wote Ubungo External tuwahudumie.”
Chapisho hilo unaweza kulipata hapa.
Hata hivyo, habari za Boni yai kuanza ufugaji wa kuku hazijaanza kuvuma mwaka 2025, na wala hajaanza kufanya kazi hiyo hivi sasa bali amekuwa akifanya hivyo tangu zamani.
JamiiCheck inawakumbusha watu kuwa baadhi ya upotoshaji hutokea kwa kutumia Picha, hivyo ni muhimu kujiridhisha kwanza juu ya uhalisia wa picha husika kabla ya kuamini kile kilichoandikwa.