Boniface Jacob: Abdul Nondo kapatikana, yupo Mahututi hajiwezi kwa lolote, hata kuongea ni shida

Boniface Jacob: Abdul Nondo kapatikana, yupo Mahututi hajiwezi kwa lolote, hata kuongea ni shida

Hatimaye kijana Nondo kapatikana muda huu,akiwa ametupwa nje ya Makao Makuu ya Ofisi za ACT.

Taarifa za awali zinasema yupo Mahututi hajiwezi kwa lolote ,hata kuongea ni shida.
===============
Kwa upande mwingine Malisa ametoa maelezo mengine kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram

Wasamaria wema" waliomuokota Nondo Coco Beach kwanini wamempeleka ofisini badala ya hospitali? Inaelezwa Nondo amejeruhiwa vibaya na hawezi kutembea wala kuongea.

"Sasa wamempeleka ofisi za chama akafanye nini? Anyway, its a good thing kama chama kimechukua initiatives za kimkimbiza Aghakhan kwa matibabu. Kwa sasa kipaumbele kiwe afya yake kwanza, Hayo mengine tutayajua vizuri akishapona".

Soma Pia: Dar: Abdul Nondo amechukuliwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

Source
Boniphace Jacob
Ex mayor.

View attachment 3166864
Utekaji halisi haufai, unaumiza, unasikitisha. Naona wanahangahika sana,..... Leo mara kuteka, mara uchunguzi, mara kile, wanajaribu kuwasaulisha watu mambo ya msingi ila now a days watu wanatambua, zama hizi si kama zile.
 
Tanganyika mauaji na utekaji, umekuwa mkubwa,ila Zanzibar hukuna kitu kama hicho.

Zanzibar Kuna jeshi la polisi tofauti na Tanganyika?
 
Huu utekaji hadi lini ndugu zangu? Ni nani mkubwa anaratibu utekaji ambaye anaogopwa na wote? Wapi wazee wa nchi? Wapi viongozi wa dini? Wapi wana harakati?
 
Ndugu acha masikhara kwenye roho za watu sisi sote tunakipenda chama lakini ukweli lazima usemwe kwa mwendo wa sasa wa jeshi la Polisi unaogopesha kwa kweli Jeshi letu la Polisi kwa sasa haliaminiki na linaogopwa na Wananchi si Jeshi rafiki tena
imani yako au ya mwingine kwa kitu chochote kile unachokiamini au usichokiamini, inanihusu nini mimi gentleman?

kwahiyo sasa mpaka sasa unaamini taarifa ya polisi au hao vibwengo wengine, hata uwe na huruma ya kinafiki kiasi hicho?🐒
 
At least huyu kapatikana haraka tena akiwa bado anapumua
Zitto siyo Mbowe ilikuwa lazima apatikane .

Zitto amewapa tahathari kwa vitisho polisi wa Gogoni .

Kama asingepatikana lazima Polisi kama 5 wangekiona .Wameogopa refer case ya yule waziri
 
Mkuu uko Tanzania kweli?Mbona unauliza maswali yaliyoko0 wazi

George alikuwa mgombea Mwenyekiti wa Kitongoji kwa tiketi ya CHADEMA wilaya ya Manyoni mkoa wa Singida.

Alipigwa risasi tarehe 26/11/2024 usiku na askari Magereza.
Asante ɓroo,
Hiyo habari ilinipita
 
Hivi mbona wananchi wamewaachia uchaguzi washinde hata kwa asilimia 100, kwanini bado wanatesa wapinzani
Wenyewe wanajua kuwa hawajashinda.

Mtaa una wakazi 100 lakini waliojiandikisha kupiga kura ni 19 na waliopiga kura ni 9, Sasa hapo si wanajua kabisa kuwa hawajashinda?
 
Mwanzo 4:8
Mungu akamwambia Khaini akasema, "Umefanya nini?sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.
Basi sasa umelaaniwa wewe katika ardhi iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako"
 
acha upotoshaji gentleman dah h🐒
CCM bila ushirikina haiendi. Kwa ushirikina wenu mnajenga majengo ya Hospitali bila ya kuweka matabibu, vifaa tiba wala madawa. Kama si ushirikina ni ni Sasa?

Yaani wagonjwa wataponaje kama hakuna matabibu, madawa na vifaa tiba? Huo ndiyo ushirikina ambao CCM mnaupenda.
 
Back
Top Bottom