Boniface Jacob: Abdul Nondo kapatikana, yupo Mahututi hajiwezi kwa lolote, hata kuongea ni shida

Boniface Jacob: Abdul Nondo kapatikana, yupo Mahututi hajiwezi kwa lolote, hata kuongea ni shida

Hii Tanzania hujui umuamini nani? kwanza mimi napinga lolote kuhusu haya mambo siungi mkono kabisa lakini kuna maswali ya kujiuliza. Mtu akiokotwa kawaida anapelekwa Hospital sio ofisi za chama usiku na kuna sehemu nimesoma kuwa katupwa akasimamisha boda na kuomba impeleke ofisi ya chama hapa tunaambiwa mahututi hata kuongea hawezi sasa mtu mahututi kapandaje boda. Tukemee hii tabia lakini pia tukemee taarifa za kupotosha maana watu wanatumia hii kama kick za kisiasa pia. nchi hii tunasema kufa kufaana.
angewezaje kuomba bodaboda wakati mtu yupo hii bin taabani,una hokikosa ni taarifa sahihi ktk wakati sahihi,jitahidi uwe na vyanzo vya habari ambayo vinawaledi kama vyanzo yako muhimu.
 
Vyombo vya usalama vipo Madaktari wapo na Waandishi wa habari wapo kama mashuhuda wanaoweza kutufahamisha Ukweli ni upi !!
 
Kama hakuna picha za foleni za vijana, hao wapiga kura 31m+ waliojoandikisha walitokea wapi, ama nchi hii ina wazee 31m? Au mmejisahau kwa ile idadi ya kupika?
Wazee gani?!..mimi niko kwenye 40s,siwezi pigia kura chadema
 
Nani aliye nyuma ya haya?, na ni kwanini wanatekwa kwani wameongea nini kibaya,
 
angewezaje kuomba bodaboda wakati mtu yupo hii bin taabani,una hokikosa ni taarifa sahihi ktk wakati sahihi,jitahidi uwe na vyanzo vya habari ambayo vinawaledi kama vyanzo yako muhimu.
Mimi sina sababu ya kutafuta vyanzo sio kazi yangu nimesema nimesoma sehemu kama nilivyosoma hapa. wenye kazi zao watatoa tu ila kwangu mimi ndio kwanza najuwa kuna mtu anaitwa Nondo kwa kusoma tu hizi taarifa maana hata sijui ni nani haswa.
 
Hatimaye kijana Nondo kapatikana muda huu,akiwa ametupwa nje ya Makao Makuu ya Ofisi za ACT.

Taarifa za awali zinasema yupo Mahututi hajiwezi kwa lolote ,hata kuongea ni shida.
===============
Kwa upande mwingine Malisa ametoa maelezo mengine kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram

Wasamaria wema" waliomuokota Nondo Coco Beach kwanini wamempeleka ofisini badala ya hospitali? Inaelezwa Nondo amejeruhiwa vibaya na hawezi kutembea wala kuongea.

"Sasa wamempeleka ofisi za chama akafanye nini? Anyway, its a good thing kama chama kimechukua initiatives za kimkimbiza Aghakhan kwa matibabu. Kwa sasa kipaumbele kiwe afya yake kwanza, Hayo mengine tutayajua vizuri akishapona".

Soma Pia: Dar: Abdul Nondo amechukuliwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

Source
Boniphace Jacob
Ex mayor.

View attachment 3166864
Nasubiri tamko wa wazee wa Mwandiga!
 
Back
Top Bottom