Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Hakimu mkazi Mkuu Franco Kiswaga wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam anayesikiliza kesi hiyo anatarajiwa kusoma hukumu ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Boniface Jacob (Boni Yai).
Ingawa mashtaka yanayomkabili yana dhamana, lakini tangu aliposomewa mashtakata yanayomkabili, Septemba 19, 2024, dhamana yake imekuwa kizungumkuti kutokana na maombi yaliyotolewa na Serikali ya kuzuia dhamana yake.
Boni Yai anakabiliwa na kesi ya uchapishaji taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii ambayo upelelezi wake bado haujakamilika.
UPDATE
MAHAKAMA ya Hakimu mkazi Kisutu leo Jumatatu Oktoba 07/2024 imekubaliana na hoja za utetezi kuhusu pingamizi la kutopatiwa dhamana lililokuwa limewekwa na Jamhuri dhidi ya aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni na baadaye Ubungo, Dar es Salaam Boniface Jacob (Boni Yai), hivyo Mwanasiasa huyo amepatiwa dhamana inayoendana na masharti yatakayowekwa kwenye shauri la msingi, ambalo sasa linaendelea.
Maamuzi hayo madogo ndani ya kesi ya msingi yametangazwa Mahakamani hapo na Hakimu mkazi Mkuu Franco Kiswaga wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam ambapo shauri hilo lililetwa Mahakamani hapo kwa ajili ya kusomwa hukumu ya kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi.
Soma Pia