Boniface Jacob apata dhamana baada ya kushikiliwa mahabusu kwa takriban siku 19

Hakimu mkazi Mkuu Franco Kiswaga wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam anayesikiliza kesi hiyo anatarajiwa kusoma hukumu ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Boniface Jacob (Boni Yai).

Ingawa mashtaka yanayomkabili yana dhamana, lakini tangu aliposomewa mashtakata yanayomkabili, Septemba 19, 2024, dhamana yake imekuwa kizungumkuti kutokana na maombi yaliyotolewa na Serikali ya kuzuia dhamana yake.

Boni Yai anakabiliwa na kesi ya uchapishaji taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii ambayo upelelezi wake bado haujakamilika.

UPDATE

MAHAKAMA ya Hakimu mkazi Kisutu leo Jumatatu Oktoba 07/2024 imekubaliana na hoja za utetezi kuhusu pingamizi la kutopatiwa dhamana lililokuwa limewekwa na Jamhuri dhidi ya aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni na baadaye Ubungo, Dar es Salaam Boniface Jacob (Boni Yai), hivyo Mwanasiasa huyo amepatiwa dhamana inayoendana na masharti yatakayowekwa kwenye shauri la msingi, ambalo sasa linaendelea.

Maamuzi hayo madogo ndani ya kesi ya msingi yametangazwa Mahakamani hapo na Hakimu mkazi Mkuu Franco Kiswaga wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam ambapo shauri hilo lililetwa Mahakamani hapo kwa ajili ya kusomwa hukumu ya kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi.

Soma Pia

Awe makini , watataka kumteka tena hao majamaa wa mama Abdul
 
Sheria inatamka wazi polisi wanatakiwa wamshikilie masaa ishirini na nne kama siyo kosa la uhaini na uhujumu uchumi aachiwe lakini Kwa kuwa mahakama zetu hupigiwa simu zimeamua kuvunja hiyo Sheria Kwa sababu ya simu ya kizimkazi aliyowapigia. Bora mahakama zetu zifutwe na tujiunge na marekani ili mtu akikosea tunaenda kumshitaki marekani.
 
Huyu shatani namba moja (Boni) anastahili adhabu kali ili iwe fundisha kwa wapuuzi wa mitandaoni kuandika wanachojisikia tu.
Matoto ya stand ni laana,Siku imepita nawee kwa upuuzi huu.
 
Sena ndio furaha yako kuona hayo yakitendeka kwa wenyemtazamo tofauti na wako
wahalifu makaidi na wenye kiburi katika kutii sheria bila shuruti ni lazima wanyoroshwe kwa mujibu wa sheria :pedroP:
 
Katoka Sasa,ni habari Dunia nzima Dw,BBC,voice of America,duh mwamba kala Dona week tatu,si maguvu ya misuli katoka nayo!
kwahiyo sasa inasaidia nini hiyo ? :pedroP:

kutafuta huruma ni kazi sana dah
 
Hakimu mkazi Mkuu Franco Kiswaga wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam anayesikiliza kesi hiyo anatarajiwa kusoma hukumu ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Boniface Jacob (Boni Yai).

Ingawa mashtaka yanayomkabili yana dhamana, lakini tangu aliposomewa mashtakata yanayomkabili, Septemba 19, 2024, dhamana yake imekuwa kizungumkuti kutokana na maombi yaliyotolewa na Serikali ya kuzuia dhamana yake.

Boni Yai anakabiliwa na kesi ya uchapishaji taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii ambayo upelelezi wake bado haujakamilika.

UPDATE

MAHAKAMA ya Hakimu mkazi Kisutu leo Jumatatu Oktoba 07/2024 imekubaliana na hoja za utetezi kuhusu pingamizi la kutopatiwa dhamana lililokuwa limewekwa na Jamhuri dhidi ya aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni na baadaye Ubungo, Dar es Salaam Boniface Jacob (Boni Yai), hivyo Mwanasiasa huyo amepatiwa dhamana inayoendana na masharti yatakayowekwa kwenye shauri la msingi, ambalo sasa linaendelea.

Maamuzi hayo madogo ndani ya kesi ya msingi yametangazwa Mahakamani hapo na Hakimu mkazi Mkuu Franco Kiswaga wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam ambapo shauri hilo lililetwa Mahakamani hapo kwa ajili ya kusomwa hukumu ya kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi.

Soma Pia

Mbona siku ni chache si angakaa tuu kama kina Mbowe miezi ya kutosha?
 
Back
Top Bottom