LGE2024 Boniface Jacob: CHADEMA tumesimamisha wagombea katika Mitaa 547 kati ya 564, iliyobaki tumewaachia vyama vingine

LGE2024 Boniface Jacob: CHADEMA tumesimamisha wagombea katika Mitaa 547 kati ya 564, iliyobaki tumewaachia vyama vingine

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
uchaguzi wa serikali za mitaa, hafla iliyofanyika leo, Alhamisi Novemba 07.2024 amesema kuwa wamefanikiwa kusimamishawagombea katika Mitaa 547 kati ya 564
Kama taarifa hii ni kweli, pongezi sana kwa juhudi hiyo, na ingependeza sana hali iwe hivyo hivyo na kwenye kanda nyingine nchi nzima.
Lakini nafasi zilizo achwa ni 17, na siyo 23.

Hebu Lema na yeye atoe mrejesho wake huko Kandani kwake.
 
Hotuba aliyotoa kamanda Boniface Jacob imetia chachu na hasama siyo kwa wanachadema wote bali hata huku mitaani wananchi wanasema mwisho wa chama dola kongwe umetimia, kura zote kwa CHADEMA

WIMBO WA HAMASA, KANYAGA KANYAGA ...

View: https://m.youtube.com/watch?v=dJo_96hjF6Y

Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Pwani kamanda Boniface Jacob almaarufu BoniYai, leo 07 November 2024 ametoa hotuba nzito inayokwenda kuandika ukurasa mpya wa mabadiliko ya kisiasa na kiutawala nchini Tanzania baada ya miongo hiyo kutawaliwa na chama dola kongwe ambacho sasa kimeishiwa pumzi.

Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani Boniface Jacob amesema kuwa wao kama chama CHADEMA, wapo tayari kwa uchaguzi kwani mpaka sasa wamesimamisha wagombea kwa zaidi ya asilimia 95 kwa mkoa wa Dar es Salaam na wapo tayari kufanya kampeni za kistaarabu.

“Kwanza, tupo tayari kwa uchaguzi, na pili tupo tayari kwa kampeni za kistaarabu sisi CHADEMA ustaraabu ndio jadi yetu, ndio maana huwezi kusikia kwenye kura za maoni kuna wizi au vurugu”

“Lakini tatu kama wao wakiamua kusiwe na uchaguzi, wakaamua kuhujumu uchaguzi CHADEMA Dar es Salaam ipo tayari kwa lolote, waamue tunyoe au wasuke kwa hiyo hatma ya uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa mkoa wa Dar es Salaam ipo mikononi mwa Tume yenyewe, wasimamizi wa uchaguzi na chama tawala cha CCM.” Boniface Jacob
 
Mama Samia amesema Uchaguzi utakuwa Huru na Haki. Washindi watatangazwa kwa Haki.
 
MBONA MITAA YOTE HAKUNA WAGOMBEA WA CHADEMA HAO ANAOWASEMA WAKO MITAA IPI LABDA MBONA ANACHEKESHA HUYU BONI MAYAI
Wewe unajua mitaa mingapi uliyoitembelea na usipelewe takwimu?
 
9 November 2024
Mlandizi, Pwani
Tanzania

Boniface Jacob Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani


View: https://m.youtube.com/watch?v=nxEWtJhSnyw

Mnataka viongozi tutoe tamko, sasa natoa tamko, hakuna mtu kuenguliwa au kukubali kuenguliwa tuoneshe tumechukia, kukasilishwa na tuoneshe kwa vitendo kwamba uhuni na hujuma hii hatuko tayari kuivumilia" Boniface Jacob, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani akizungumza na viongozi wa kanda hiyo wa mkoa wa Pwani Tanzania.
 
Back
Top Bottom