Hotuba aliyotoa kamanda Boniface Jacob imetia chachu na hasama siyo kwa wanachadema wote bali hata huku mitaani wananchi wanasema mwisho wa chama dola kongwe umetimia, kura zote kwa CHADEMA
WIMBO WA HAMASA, KANYAGA KANYAGA ...
View: https://m.youtube.com/watch?v=dJo_96hjF6Y
Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Pwani kamanda Boniface Jacob almaarufu BoniYai, leo 07 November 2024 ametoa hotuba nzito inayokwenda kuandika ukurasa mpya wa mabadiliko ya kisiasa na kiutawala nchini Tanzania baada ya miongo hiyo kutawaliwa na chama dola kongwe ambacho sasa kimeishiwa pumzi.
Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani Boniface Jacob amesema kuwa wao kama chama CHADEMA, wapo tayari kwa uchaguzi kwani mpaka sasa wamesimamisha wagombea kwa zaidi ya asilimia 95 kwa mkoa wa Dar es Salaam na wapo tayari kufanya kampeni za kistaarabu.
“Kwanza, tupo tayari kwa uchaguzi, na pili tupo tayari kwa kampeni za kistaarabu sisi CHADEMA ustaraabu ndio jadi yetu, ndio maana huwezi kusikia kwenye kura za maoni kuna wizi au vurugu”
“Lakini tatu kama wao wakiamua kusiwe na uchaguzi, wakaamua kuhujumu uchaguzi
CHADEMA Dar es Salaam ipo tayari kwa lolote, waamue tunyoe au wasuke kwa hiyo hatma ya uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa mkoa wa Dar es Salaam ipo mikononi mwa Tume yenyewe, wasimamizi wa uchaguzi na chama tawala cha CCM.” Boniface Jacob