Boniface Jacob: Polisi walioua Mlinzi wa Bar ya Boardroom Sinza wadaiwa kutumwa na RC Chalamila kukamata Wanaojiuza

1. Polisi wawili waua kwa risasi mlinzi wa Bar maarufu ya Boardroom iliyopo Sinza Jijini Dar es Salaam.

2. Mlinzi waliyeuwawa kwa risasi anaitwa Razak Anan mwenye umri wa miaka 29 muajiriwa wa Bar ya Boardroom, Sinza

3. Polisi kutoka kituo cha Polisi Mabatini walifika na gari na kupaki nje ya Bar ya Board room na kuanza msako wa Dada poa kwa kusema ni agizo la Mkuu wa Mkoa.

4. Lakini Polisi hao walikuwa wakiwatoa nje wahudumu na wateja katika Bar hiyo ambao walikuwa na min skirt (sketi fupi) kwa kusema kuwa watu hao kwa mavazi yao walikuwa wanajiuza katika Bar hiyo ya usiku (night Club)

5. Wateja wengine walipona udhalilishaji na manyanyaso hayo walianza kuondoka katika Bar hiyo ya Boardroom na waliobakia waligoma kutolewaa nje ya Bar kwa muonekano wa mavazi yao.

5. CCTV za Bar ya Board room inayonyesha Polisi hao walipoona wadada wanakata kufananishwa na machangudoa walienda katika gari na kuchujua silaha aina ya bunduki (SMG) na kuanza kutishia wateja na kuelekezea katika meza za wateja waliokuwa wanakunywa katika Bar hiyo.

6. Polisi hao ambao walikuwa wanaonekana wametumia kilevi walifyatua risasi kadhaa kisha kuondoka na gari yao kutoka eneo hilo la Bar ya Boardroom na baada ya kuondoka wateja walirejea na kukuta mlinzi mmoja wapo akiwa amelala chini akiwa amepigwa risasi na kuvuja damu nyingi (video inaonyesha damu ya marehemu)

7. Mlinzi wa Board room alifariki njiani akiwa katika Bajaji anakimbizwa hospitali.

8. Matukio ya polisi kuvamia sehemu za starehe na nyumba za watu binafsi ni maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye anaendesha zoezi la kutafuta madanguro na kusaka madada poa.

9. Leo Mkuu wa Mkoa amesisitiza mauaji kufanywa na polisi ni Jambo la kawaida "Mtu akifia kituo cha polisi tunasema Polisi wameua, Mtu akifia hospitali tunasema ni Mapenzi ya Mungu" RC-DSM, Chalamila

10. Nawakumbusha kulaani tukio lolote la Polisi kuua raia kwa kisingizio chochote kile, Leo kwa huyu kesho kwake.

#Polisi waliua baunsa kwa utashi wao na si RC kama ambavyo wengi wanafikiri.


Video za chini zikionyesha polisi hao wanafyatulia watu risasi.
 
9. Leo Mkuu wa Mkoa amesisitiza mauaji kufanywa na polisi ni Jambo la kawaida "Mtu akifia kituo cha polisi tunasema Polisi wameua, Mtu akifia hospitali tunasema ni Mapenzi ya Mungu" RC-DSM, Chalamila
Hii nchi ngunu saana.
 
Badilisha kichwa cha habari sema wameua kwa maagizo ya RC.

Maana yeye ndo ndo kamrisha polisi wasake wanaojiuza sasa sijui wana alama gani? Siku ikitokea makahaba wenye akili wakaishtaki selikal ndio siku watakayo tajirika kwa fidia za udhalilishwaji.
 
Jukumu kuu la polis ni kulinda raia na mali zake. Nadhani Mh RC nae hajui kabisa majukumu take na hajui majukumu ya polisi pia
 
Jukumu kuu la polis ni kulinda raia na mali zake. Nadhani Mh RC nae hajui kabisa majukumu take na hajui majukumu ya polisi pia
Watanganyika so far wannaamini kazi ya RC ni kujenga chama chake.
 
9. Leo Mkuu wa Mkoa amesisitiza mauaji kufanywa na polisi ni Jambo la kawaida "Mtu akifia kituo cha polisi tunasema Polisi wameua, Mtu akifia hospitali tunasema ni Mapenzi ya Mungu" RC-DSM, Chalamila
Hii ni kauli ya leo au ya siku za nyuma? kama ameirudia leo tena, basi kuna siku ATANYONGWA.
 
Kichwa na utumbo wa habari havisomani mkuu. Rekebisha kimoja wapo
 
Huyu Chalamila kuua mtu kwake sio kitu cha kushangaza. Mara nyingi huwa anajigamba tena mbele ya waandishi wa habari kuwa anaweza kumtwanga mtu na risasi. Marumizi ya bastora kwake ndio kipa umbele kwa maamuzi atayoshindwa kuamua kwa busara.
 
8. Matukio ya polisi kuvamia sehemu za starehe na nyumba za watu binafsi ni maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye anaendesha zoezi la kutafuta madanguro na kusaka madada poa.
by ncessary implication, kauli ya kuwa mtu akifia kituoni, POLISI WAMAEUA, AKIFIA HOSPITAL MUNGU KAPENDA ..kauli kama hizi indirectly unawaruhusu polisi kuua kwa defense hiyo. SAMIA UTABEBA DHAMBI HIZI ZA MAUAJI KWA KUMPA MADARKA KICHAA AMBAYE ULISHASEMA HUYU HAJAKUA!
 
Umeeleweka kaka!
 
Hivi?
Kuna cheo cha Ex Mayor nchini?
Au ni ili misifa , niliwahi kuwa mkubwa mimi, usinione hivi!
 
Badala Serikal Itafute Viongozi Wanaowachomekea Raia Vyupa Vya Matako Inang'ang'ana Na Madada Poa.NONSENSE
 
Haya yote ni kutaka kuendesha mambo kama Iran kwa Ayatollah au Afghanistan kwa Taliban walipo na polisi wa maadili.
Kwa hiyo nchi ambazo hazina sheria kama za Iran na Afghanistan polisi wake hawauwi raia kimakosa?
 
And so the police expected to find people with hijabs at the boardroom bar hall?
What a wicked police jeshi?
The police in Tz is a legally organized and trained group of gangtsers under the ruling group of balded heads called sisi ni em. I pity them.
Rais Samia if you get to read this, pls do us a favour by restructuring the whole police system in Tz au mpaka usikie tunakamata mmoja mmoja tunaua huku mitaani? Tunaishi nao huku.
 
Huu ni muendelezo wa ubwege nataka munijibu

1. Je mtu anayedaiwa kujiuza alitaka kujiuza kwa nani ?

2.Hiyo complaint waliipata lini na jalada la uchunguzi lilifunguliwa lini?

3.Je hiyo Bar si ina Meneja? Hiyo si biashara ya Mtu? Je mulizungumza na muajiri wa huyo anaye jiuza?

4.Huyo mteja aliyetaja kuuziwa yuko wapi? Au ndio huyo Mlinzi binafsi muliyemuuwa

5.Je mulikuwa na Uongozi wa Serikali ya Mtaa ? Na huo upuuzi unao onekana kwenye video ndiyo taratibu za ukamataji?

Hakuna aliyesalama TUDAI KATIBA MPYA

1.Wafanyakazi Kikokotoo
2.Walevi risasi na kifo
3.wakosoaji bambika kesi weka mahabusu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…