PostGE2025 Boniface Jacob: Warioba anaaminika kwenye maridhiano

PostGE2025 Boniface Jacob: Warioba anaaminika kwenye maridhiano

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani Boniface Jacob, amesema kuwa katika suala la kutafuta maridhiano ya kisiasa nchini, aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Jaji Joseph Warioba ni mojawapo kati ya watu wanaoweza kuaminiwa kusimamia au kuwa sehemu ya mchakato huo.

Boniface ameeleza kwamba Mzee Warioba ameonesha jitihada za wazi hata kabla ya uchaguzi za kutaka kuliweka taifa pamoja, na hivyo anaweza kuaminiwa kushiriki katika kutafuta suluhu ya mgawanyiko wa kisiasa kwa pande zinazotofautiana.

"Mfano tukiwa bado hatujaenda kwenye uchaguzi tukiwa na mivutano ya 'no election' na wengine wakisema Oktoba tunatiki nchi nzima nilimuona Mzee mmoja tu aliyefanya jitihada kwanza aliwatafuta tume ya uchaguzi kwa kuwabembeleza kwamba ikiwezekana uchaguzi usifanyike ili haya makundi mawili yakubaliane kwanza"

"Nilimsikia akisema kwamba pamoja na jitihada hizo tume walimkatalia kuonana nae wakamjibu kwamba kama ana jambo aandike barua, kwa kujinyenyekeza pamoja na kwamba ni mtu mkubwa Mzee mstaafu wa nchi hii akaandika barua kuwajulisha tume mtazamo wake"

"Kwamba anatamani makundi yanayosigana yakubaliane kwanza kabla ya uchaguzi ambaye Mzee huyo ni Jaji Warioba pamoja na kwamba hakufanikiwa lakini alionesha kwamba amejali"

"Mtu wa namna hiyo ukimuweka kwenye tume tayari ameonesha kujali tangu mwanzo kwahiyo angejitokeza watu wangekuwa na imani kwamba yule Mzee angeweza kuwa ni mwaminifu"-Boniface Jacob.
 
Naanza kuwa na kihali… This Warioba thing inaweza kuwa project ya National Unity na yeye mwenyewe hajui…. Him came out ranting after meeting president, now ITV is having Boniyai quotes suggesting him kwenye Maridhiano.

Wanamset huyu mzee aingie tena kwenye kumi na nane zao kisha wamtupe nje kama walivyofanya na ile rasimu yake..
 
Back
Top Bottom