Elias Msuya
Platinum Member
- Dec 23, 2011
- 267
- 1,014
Mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu nchini Kenya, Boniface Mwangi ameachiliwa kwa dhamana baada ya kufunguliwa mashtaka ya kumiliki risasi kinyume cha sheria kuhusiana na madai ya kuhusika kwake katika maandamano hatari dhidi ya serikali yaliyofanyika Juni mwaka huu.
Mashitaka hayo yametajwa leo Julai 21 wakati ukumbi wa mahakama ukiwa umejaa mamia ya wanaharakati, wakiwa wamevaa bendera za Kenya.
“Hawana ushahidi,” Mwangi aliwaambia waandishi wa habari, akielezea mashtaka dhidi yake kama “aibu kubwa”.
Wakili wake aliambia shirika la habari la Reuters kuwa wanashukuru mahakama kwa kukubali kumuachia Mwangi kwa dhamana.
Kenya imekuwa ikikumbwa na maandamano makubwa ya kupinga serikali kote nchini tangu mwaka jana – awali kupinga ongezeko la kodi katika muswada wa fedha, na baadaye kudai kujiuzulu kwa Rais William Ruto.
Tangu maandamano hayo yalipoanza, polisi wamekuwa wakishtumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu, ikiwemo madai ya wakosoaji wa serikali na wanaharakati kutekwa na kuteswa.
Boniface Mwangi alishtakiwa na polisi siku ya Jumatatu, siku mbili baada ya kukamatwa na kushutumiwa kwa kumiliki mitungi ya gesi ya machozi ambayo haijatumiwa, risasi ya mfano ya milimita 7.62, simu mbili za mkononi, kompyuta mpakato na daftari.
Muda mfupi kabla ya kufikishwa mahakamani kwa mashtaka yanayohusiana na ugaidi, Boniface Mwangi aliyekuwa na msimamo thabiti, akiwa ameandamana na mawakili wake, familia, na wanaharakati wenzake, alisimama katika Mahakama ya Kahawa.
Katika onyesho la hisia na mshikamano, umati huo uliimba kwa pamoja, na kugeuza ngazi za mahakama kuwa jukwaa la maandamano.
Mwangi, aliyekamatwa kwa tuhuma za kuhusika na vurugu za maandamano, alitumia fursa hiyo kuikosoa hadharani serikali.
Chanzo: Aljazeera