Bonyokwa Dar - Mwenyekiti wetu wa mtaa hataki kuanzisha ulinzi shirikishi wananchi hatuna lu kumfanya

Bonyokwa Dar - Mwenyekiti wetu wa mtaa hataki kuanzisha ulinzi shirikishi wananchi hatuna lu kumfanya

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Tumepiga kelele weee kwa kutizama yanayotukia mitaa mingine ya dar, tukimsihi mwenyekiti kuanzisha ulinzi shirikishi mtaani kwa wasio na mda wa kulinda kuchangia na wasiopenda kuchangia kupangiwa zamu za kulinda wenyewe wala mwenyekiti hana habari.

Tunaomba viongozi watusaidie

kinga ni bora kuliko tiba na tunataka viongozi wanaowajibika. Tunataka tujilinde wenyewe ila kwa kuwekewa utaratibu unaotambulika kisheria na serikali ya mtaa
 
Kwa sababu mnasemaga hamumtaki naye kaamua kuwadindia. Na wale vijana wanaovuta bangi pale kwenye banda la chips la Ustadhi ndio wataanza kukaba
 
Tumepiga kelele weee kwa kutizama yanayotukia mitaa mingine ya dar, tukimsihi mwenyekiti kuanzisha ulinzi shirikishi mtaani kwa wasio na mda wa kulinda kuchangia na wasiopenda kuchangia kupangiwa zamu za kulinda wenyewe wala mwenyekiti hana habari.

Tunaomba viongozi watusaidie

kinga ni bora kuliko tiba na tunataka viongozi wanaowajibika. Tunataka tujilinde wenyewe ila kwa kuwekewa utaratibu unaotambulika kisheria na serikali ya mtaa
HATA KUMUUA MMESHINDWA?

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Sema unataka hela ya ulinz shirikishi

Kwa dsm ulinz shirikishi n mchongo wa kipigaji TU unajua panya road wanavamia kuanzia saa 10 jion had saa moja jion na nyie ulinz mnaanza saanne had saa tano usiku

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
kuna maeneo wanataka kila mtu alinde hawataki uchangie pesa
Tulikwisha anzisha huko nyuma mpango wa kila mtu alinde, wapo ambao walidai hawana mda, tukaanzisha ya kuchangia wapo ambao hawakutoa michango kulalamikia viwango.

sasa tunasema uje mpango wenye vyote na kila mtu iwe lazima kushiriki.

kuna watu kweli ratiba zao za kazi zimewabana lakini watoe michango watafutwe vijana kulinda kwa niaba yao

wapo ambao hawataki kutoa michango basi familia hizo atoke kijana au baba mwenye nyumba wapangiwe zamu za kulinda kulingana na watu waliopo.

tunataka tuwe na mpango ambao mtu haji na sababu ya kumwonea huruma, tuwe na mpango ambao ni rafiki kwa kila mtu kwa uchumi wake na mda wake
 
Sema unataka hela ya ulinz shirikishi

Kwa dsm ulinz shirikishi n mchongo wa kipigaji TU unajua panya road wanavamia kuanzia saa 10 jion had saa moja jion na nyie ulinz mnaanza saanne had saa tano usiku

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
hawa ndo panya road wenyewe wanajikita kupinga mipango ya ulinzi ili kufanikisha biashara zao
 
Back
Top Bottom