Kwa wasoma vitabu, kutokana na sababu mbalimbali, wengi tunatumia zaidi softcopies badala ya hardcopies. Formats za vitabu zilizotawala ni pdf, ePub na Mobi. Mimi binafsi napendelea ePub au mobi kuliko pdf sababu ya fonts za pdf ni ndogo ndogo sana.
Hivyo kwenye kusoma, App unayotumia inaweza kukuvutia kusoma au la. Mimi binafsi ninatumia App mbili kwenye kusoma, sababu ninasoma vitabu vya namna mbili, Novels and Non-novels.
Non-Novels.
Nasoma zaidi vitabu vya Non fictions kama vya Historia, wasifu, Sayansi, Siasa n.k. Hivyo kwenye usomaji hujikuta nahitaji kutake Note na napenda zaidi Fonts ziwe kubwa na ndefu huku nikiwa na display kubwa. Hivyo baada ya Safari ndefu ya kutumia na kuacha, nimejikuta ni mlevi wa App ya ReadEra.
View attachment 1789796
Naipenda App sababu, ya Fonts zake zinavutia sana kusoma (inakupa uchaguzi wa fonts). Font hizi nimezi-custumize hivi;
View attachment 1789799
Pia inakupa mfumo mzuri wa kutengeneza folders, kama za To Be Read list, Read List, Collection (hapa unaweza tengeneza 'shelf' yako ya vitabu kutokana na mpangilio uutakao mf, History, Politics, Novels, Siasa, Tawasifu n.k. Inakupa uwezo wa kupanga kwa Authors. Sifa yake nyingine kubwa, hakuna Ads kabisa. App nyingi zinakera kwa Ads.
View attachment 1789805
View attachment 1789806
Novels.
Novels pia zinavutia ikiwa na fonts style fulani fulani. Hapa natumia App ya PrestigioReader.
View attachment 1789808View attachment 1789809View attachment 1789810
App nzuri yenye inayokupa muonekano na nyenzo sahihi za kutumia, kwenye usomaji, huvutia sana kusoma na kusoma. Hatimaye kukimaliza kitabu, kukupa urahisi wa kufanya reviews na discussions kwenye forums mbalimbali.
Tushirikishane, wewe unatumia App gani? Inakuvutia vipi?