Book reading: Unasoma au Umesoma kitabu gani ungependa wengine wakisome?

Book reading: Unasoma au Umesoma kitabu gani ungependa wengine wakisome?

Mkuu tafadhali naomba namm hizo contacts ili nipate hiyo collection ya "jitambue" ya Munga Tehenan MUNGU amrehemu sana,.magazeti yake ya jitambue na mshauri wako ninayo mpka leo(baadhi)kwa kumbukizi zake zisizochosha na kuisha hamu alikuwa na vitu adimu saana..
Jaribu kucheki na wauza vitabu wa dar, mimi nilikinunua kariakoo kwa muuza vitabu aliye karibu na Club ya Simba. Jaribu kwa wauza vitabu mbalimbali mkuu. Mi kuna mtu nimemuazima, naona anagoma kunirudishia.
Vinginevyo, ningekuazima pia.
 
Napendekeza viongozi tajwa hapo juu wawe na tabia ya kuorodhesha vitabu walivyosoma kwa mwaka au miezi sita ili kuongeza maarifa kuhusu mambo mbalimbali ya dunia kiuchumi,kisiasa na kijamii

Hii itavutia watanzania nao kujenga culture ya kujisomea kuongeza maarifa
 
Si kusoma tu, na kuandika pia. Ila utamaduni huo unatakiwa uanzie kwa viongozi wa vyama kabla hawajafika kwenye ngazi ulizotaja maana kama mtu hakuwa na utamaduni huo toka mwazo hawezi akawa nao katika level za juu.
 
hahahaa..............................😎😎😎😎😎😎😎😎😎
 
Kama sisi wana jf tu hatuwezi kujadiliana kwa hoja za maana humu sembuse siku tikiwa marais ndio tusome na kuandika vitabu!?
 
Mimi sio "ngwini" hay ni maneno yalisikika kutoka kwa the so called "mwanasayansi". Hivi kuna hata mmoja ameabdika short stories za inspiration for the present and future generation.
 
Mimi sio ngwini hay ni maneno yalisikika kutoka kwa the so called "mwanasayansi". Hivi Kuna hata mmoja ameabdika short stories za inspiration.
Wewe mwenyewe ushawahi kuandika au huna cha kuandika!?
 
Wewe mwenyewe ushawahi kuandika au huna cha kuandika!?
Achana na mimi katafute likes kwenye Uzi wako.
Frankly I have two papers in accredited journal concerning on Science and Engineering.How about you dude?Unabahati natumia anonymous name ningekupa link google scholar.
 
Achana na mimi katafute likes kwenye Uzi wako.
Frankly I have two papers in accredited journal concerning on Science and Engineering.How about you dude?Unabahati natumia anonymous name ningekupa link google scholar.
Yaani wewe ni scholar! Dah sasa mbona kule umeongea vitu ambavyo hata darasa la saba hawezi kuachangia! Mungu atusaidie kwa kweli.
 
Yaani wewe ni scholar! Dah sasa mbona kule umeongea vitu ambavyo hata darasa la saba hawezi kuachangia! Mungu atusaidie kwa kweli.
Kumbe nabishana na zuzu.Hujui hata "Google Scholar". Mwanzo Na mwisho don't quote me in your nonsense.
 
Wale wenzangu na mie tunaokaa na kazi siku nenda siku rudi haiishi, tunaosubiri kazi zipungue ndo tufanye vitu fulani, tunaotaka Mungu aongeze siku iwe na saa 33 - wale wa ".... nitafanya kesho, nitafanya baadae, hii ngumu sana nitafanya nikimaliza hiki au kile, hii inachusha labda nibadilishe mazingira ndo nifanye, hii natupilia mbali kama ni kazi na nifukuzwe...." tusome "Eat That frog: 21 Great ways to stop procrastinating and get more done in less time" by Brian Tracy.
 
wiki hii nimesoma kitabu maarufu sana kwa sasa, kiitwacho NDOA YANGU, NINGEJUA. Nimekipenda sana kwa sababu kinaeleza kwa kinagaubaga kwa nini ndoa nyingi hazina amani. Kwa kweli kimenigusa kwa sababu kuna sehemu mtunzi ameeleza historia ya ndoa yangu utadhani ananijua, na hasa zaidi maswali aliyouliza: 1. KAMA UNGEJUA MKEO AMA MUMEO ATAKUWA NA TABIA ALIYO NAYO SASA, JE UNGEKUBALI KUOANA? swali hili ni zuri kwa sababu kwangu mimi nisingekubali, na hata mke wangu alipojibu swali hili, nae akasema asingekubali. Ukweli kitabu hiki ni kiboko, na ingawa nimekiazima, kwa kweli sitamrudishia mwenyewe, nataka nikisome zaidi na zaidi nitambue makosa yangu na huenda kikanisaidia pia katika kuwashauri wenzangu.
Kitabu cha pili nilichosoma kinaitwa MY DEAR BOTTLE, ukianza kukisoma andaa mbavu zako, maana kinaonyesha jinsi ambavyo pombe kumfanya mtu akapoteza utu wake na thamani kwa wengine

Watu kama nyie ndo mliotufundisha uchoyo wa vitabu. Unakuta mtu anapitia wakati mgumu au anahangaika na jambo fulani na unaona una kitabu unachofikiri kitamsaidia unaamua kumpa asome kisha akurudishie. Ukija kuhesabu vitabu ulivyorushwa na thamani yake unakoma kiherehere. Siku hizi simpi mtu kitabu hata nisukumwe vipi moyoni. Namwelekeza jinsi ya kukipata au namnunulia chake kama zawadi ili kupunguzia moyo takataka.

Kama wewe kimekusaidia na unatamani kukisoma tena na tena ili uweze kuwashauri na wengine kwa nini upange kutokukirudisha badala ya kupanga kukirudisha na kununua cha kwako? Huoni kama ni dhuluma na kukosa shukrani? Aliyekupa unadhani hataki kukisoma tena na tena kama wewe au unadhani hana ndugu na marafiki anaotamani wapone kama wewe? Tunapowaazima vitabu si kwamba tunakuwa hatuvihitaji tena ila tunakuwa tumeamua kutanguliza mahitaji yenu mbele na kuweka ya kwetu nyuma. Samahani bwana. Ni kwamba comment yako imeamsha kumbukumbu ya vitabu vyangu nilivyodhulumiwa. Mrudishie mhusika kitabu chake na umuombe radhi kwa kukichelewesha. Vinginevyo unamkatisha tamaa asiweze kuhudumia wengine kama alivyokuhudumia wewe. Dhuluma ni dhuluma hata kama si fedha.
 
Back
Top Bottom