Shukran mtoa mada!
Binafsi napenda usomaji wa vitabu sana.
Hapa chini ni baadhi ya vichache nilivyopata kuvisoma:
1.Green book by Muammar gadafi.
2.Think and grow rich.
3.How to win friends and influences people by dare Carnegie.
4.The manipulated man by Esther vilar.
5.Who will cry when you die by robin sharma.
6.Harakati za ukandamizaji fikra huru vyuo vikuu nchini by Alphonce lusako.
Nadhani hiki kitabu kilipata msukosuko wakati wa uzinduzi wake na hatimaye kupigwa marufuku,lusako kaelezea mambo mengi changamoto zinazowakabili wanafunzi wanaotetea na kupinga unyonyaji wa baadhi ya masuala ndani ya vyuo.
Wanazuoni wengi bado waoga hasa kutetea haki zao wapo kama kondoo wapelekwao machinjioni,lakini wanapojitokeza watu kama Lusaka wanapandikiza mbegu ya kujiamini na kutetea haki zako kwa wanazuoni waoga hili ni jambo jema.
Huwa najiuliza kwanini uwe muoga kudai haki yako..? msomi unakuwa muoga kutetea haki yako..?
Wanazuoni tuamuke Elimu itukomboe na itusaidie kupambana katika unyonyaji wa kila namna.Tuwaandalie mazingira mazuri vizazi
Vinavyokuja.
7.No Excuses! By Brian Tracy.
Kitabu kizuri sana,kinaelezea Mambo mazuri kubwa hasa kutokuwa mtu wa visingizio na sababu lukuki baada ya kushindwa kutekeleza jambo,kubali makosa yako na usiwe mtu wa kulalamika punguza ulalamishi tafuta njia sahihi kushughulikia changamoto...kubali wajibu wako, maisha yako yako mikononi mwako.
8.The 5 love language by Gary Chapman.
Haya Sasa kwa wale wapenda Mambo ya malavidavi hiki kitabu Safi sana,walio katika ndoa hiki pia kunawafaa vyema huku pia kikielezea malezi pia ya watoto.
Moja ya vitu alivyoelezea Mr.Chapman vya muhimu ni love language a)words of affirmation.b)receiving gift c)acts of service d)physical touch e)Quality time.
Kwa mfano Mimi hapa ukiniuliza love language yako ni ipi nitakutajia "word's of affirmation" japo wanaume wengi hudai "physical touch-tendo la ndoa,n.k"
Nashauri vijana na wanandoa wapate kukisoma kitabu hiki.
9.Act like a lady think like a man by Steve Harvey..kitabu pia kizuri hebu kajipatie nakala yako kama u-mpenzi wa vitabu.Moja ya vitu alivyopata kuvieleza ni kuhusu wanaume,anadai wanaume waliowengi wanapomutongoza kitu kikubwa na cha kwanza katika bongo zao ni kumvua nguo ya ndani mwanamke/kulala naye kisha Mambo mengine hufuata.
10.101 ways to make money in Africa by John Paul & wiuoha hernet bokrezion PhD.
Kitabu poa sana Africa ni bara ambalo tuna rasilimali nyingi sana na fursa nyingi sana za kutengeza pesa,vijana tuamuke tushughulishe ubongo tuthubutu,pamoja na changamoto za uongozi wa nchi za africa kuwa mbovu,rushwa,ukabila n.k lakini bado tunaweza kufanya Mambo makubwa tu na kusaidia jamii inayotuzunguka.
Kubwa zaiidi katika kitabu hiki unapata idea's mbali mbali za biashara,kilimo na njisi kuzikabili baadhi ya changamoto,vyema kuangalia kutazama mazingira gani upo na jambo gani ufanye ili kujipatia pesa na kutoa huduma kwa jamii inayokuzunguka laweza kuwa jipya au lakuboreshwa.
Wakati Ndio huu Africa, Africa tunaweza!!!
Tujitahidi jamii yetu
Watanzania tuwe na utamaduni wa kusoma vitabu japo kunachangamoto nyingi mfano;Ukata,upatikanaji wa vitabu na aina gani ya vitabu na malezi lakini bado tunaweza tukiwa na nia Elimu ni gharama Ujinga ni mzigo.
Shukran Jamii forum na wote wenye utamaduni wa kusoma vitabu...by Alisina.