Bookworms of JF, what's your favorite book (s) and why?

Kitabu kikubwa na cha wakati wote ni mwili wako. Ukiweza kuufahamu, huna sababu ya mavitabu yasiyoisha kutungwa
 
Between The World and Me by Ta-Ne
hisi Coates.

Black consciousness that reminds me of Alex Haley's "The Autobiography of Malcolm X".
 
Poa tu, vipi za siku?
Poa-poa aisee..

Juzi nilikuona Ulimtaja Ben Shapiro...

Ikibadidi niingie kumtazama Jamaa huyo..

Aiseee Kweli ni "Mhafidhina" Haswa..

Nilipitia vitabu vyake -Porn Generation & Brain Washed.

Nikaingia quora walau nipate Machache yake..


Nilichonivutia kwake na Uandishi wa vitabu akiwa bado kijana mdogo..

Nadhani kama nipo sahihi kaanza kuandika vitabu yupo Na Miaka 19/20....


Asante kwa Mfahamu..


Swali kwako...Vipi Ushawahi kuaandika kitabu chochote kile...?
 
Kitabu kikubwa na cha wakati wote ni mwili wako. Ukiweza kuufahamu, huna sababu ya mavitabu yasiyoisha kutungwa
Hahaha!!


Jana TBC ARIDHIO...Walikuwa na Mjadala kuhusu Usomaji Wa vitabu Kwa WaTanzania.
 
The 11th commandment by Jeffrey Archer, kama umeshaona series ya 24 basi hiki kitabu utakiona kitamu kama ubwabwa kambale
"Series" ni vitu Mpaka sasa vinanipa wakati mgumu kivitazama.

Huku Mtaani Wadau wanapenda hizo Mambo.

Nilipata kiutazama Series ya "Jumong" Tena baada ya kuona Wanafunzi Nikiwa O-level Wenzangu wanaishabikia sana hasa Weekend.

Kuna Mabrother kama watatu Walikuwa A-level nilikuwa nakaao nao wao pia walikuwa Wanaipenda,

Nakiona hapo sasa labda nakosa burudani,ndiposa nikaenda kuitazama.. Ilinishinda niliwaacha waendelea na series yao.


Mwaka Jana kuna "series" Moja ya Unyoya unapepea Angani Ya Wachina hii ndio niliimaliza na hii ni baada ya kunikuta nimemaliza kusoma kitabu cha NOTHING TO ENVY BY BArbara Deminick.

Nothing To Envy kinaelezea Maisha ya korea kaskazini na Utawala Wake,

Kitabu kizuri sana...Kwa kiasi flani wale Waliopata kuishi na kuona Utawala wa Jk Nyerere kuna mambo kadhaa utayapata kuyaona yanafanana...Socialism/Communist.


"Unyoya unapepea angani" inaonyesha pia njisi china ilivyofanya mabadiliko ya kiuchumi Kuzibaziba Mashimo/Mapungufu ya mfumo wa Awali...bila kusahau kupambana na Bidhaa feki sokoni.

Mfano Daktati feki,Maabara feki,Dawa Feki (Ukajanja) & Nguo,Vifaa vya Electronic n.k
 
Mambo ya Kim Hyuck
 
The 11th commandment by Jeffrey Archer, kama umeshaona series ya 24 basi hiki kitabu utakiona kitamu kama ubwabwa kambale
Nilivyoona Jina la Jeffrey linataka kufanana na Jeffrey Sachs..

Mchumi Jeffrey Sachs - The End Of Poverty.


Juzi Jumamosi Idhaa ya Kiswahili Dw Meza ya Duara Maada ilikuwa Tanzania Kuingia Uchumi wa kati mizani ya chini..


Waalikwa Mmoja wao alikuwa Mchumi Bravius Kahyoza...

Kwa bongo ikiweka itikadi za vyama pembeni anauwezo mzuri sana wa uchambuzi na ufafanuzi,anaonekana pia ni msomaji mzuri wa vitabu..

Alimtaja mchumi Jeffrey Sachs na mavitabu yake..


Sasa niliyvoona Jeffrey Nikiona vipi jamaa yupo kotekote kumbe ni majina tu yanafanana tena ya mwanzo.
 
Komitet Gorstivenoy Bezopasnost a.k.a KGB
The whole Russian intelligence lies in this novel
 
The 11th commandment by Jeffrey Archer, kama umeshaona series ya 24 basi hiki kitabu utakiona kitamu kama ubwabwa kambale

Mkuu kama unayo soft copy ya hicho kitabu irushe hapa tafadhali.

Sijaona pia hiyo series lakini nitaitafuta.

Amri ya 11 ninaifahamu vizuri na naipendekeza kwa wadau wote.

Inasema “Thou shalt not be found out”!
 
Mkuu nashukuru sana kwa ufuatiliaji wako. Unanipa sababu ya kuandika zaidi.

Ben Shapiro nimemsoma kitabu chake kimoja cha hivi karibuni nafikiri.

Huwa napenda kuji challenge kwa kusoma watu ambao niko tofauti nao kimawazo, nisije kuwa katika "echo chamber" na watu tunaokubaliana nao tu.

Basi nikajikita kusoma kitabu chake "The Right Side of History: How Reason and Moral Purpose Made the West Great".

Basi Shapiro kajishaua sana humo, kimepanda, kimeshuka.Mimi namu enjoy sana kwa sababu ananikumbusha mengi katika historia, hata kama sikubaliani na anavyoitafsiri historia kwa mrengo wake wa kihafidhina, kwa hiyo huyu ni mhafidhina ambaye ninaweza kumsoma.

Basi kaandika kaandika, namsoma namsoma, naona arguments zake shallow, ila ana data nzuri sana. Mwisho kabisa wa kitabu akamaliza na bonge la anti climax, kimsingi alimaliza kwa kukubali kwamba hata yeye hana majibu anafake tu.

Akanikumbusha tangazo moja la biashara la Marekani.

Jamaa anajisifia kayapatia maisha, ana nyumba nzuri ina swimming pool, ana familia nzuri, ana mali nyiingi.

Halafu anajiuliza swali, kawezaje kupata vyote hivi?

Akasema ana madeni yamemjaa kuanzia mguuni mpaka kwenye macho, karibu anataka kuzama kwenye madeni.

Shapiro naye alijenga kitabu kizima kama mtu anayejisifia sana kuwa na falsafa sahihi, halafu mwisho wa kitabu akakubali kwamba yote ni mambo ya kulazimisha tu.

 
Mkuu, kwa heshima na taadhima, nakuomba ufafanue zaidi
Sina ufafanuzi ninaodhani unaoweza kukusaidia

Ila ninachofahamu kwa uhakika ni kwamba unaoitwa mwili ni mkusanyo wa taarifa nyingi za watu waliopata kuishi miaka mingi huko nyuma

Waliopata kushughulika na changamoto nyingi na kuzipatia utatuzi iwe mahusiano, kiafya, kiuchumi, kiutawala n.k

Lakini vyote kwa ujumla vimekusanywa kwenye mwili mpya mmoja ambao ni wewe..!

Kwa ufupi ni kwamba hujawahi kufa na wewe ni majibu ya wale waliokutangulia.. kila changamoto na majibu yake vipo ndani yako

Sisi wengine kwako ni ukumbusho tu na si lolote, tungependa sana kuelewa pia ulimwengu ulio ndani yako tunapopata mda na sisi tupate kukumbuka mengi

Lakini cha kusikitisha dunia sasa hairusu hilo tumekuwa ni wakulishwa kila aina ya chakula na kuamuliwa namna ya kufikiri.!
 
I am flattered, Nowonmai.
Kindly suggest me a must read book that you highly recommend.
I missed you too.

I am in the process of writing a book Paula.

When I am through I will send a copy to you and I am confident you will find it a must read.

I am very serious about this so please don’t take it as just an instance of online bantering.

In the meantime there are two terrific psychological thrillers that I would like to recommend for leisure reading though you are likely to be a bit haunted by them especially if you have kids:

1. We Need to Talk About Kevin,
by Lionel Shriver.

2. Defending Jacob, by William
Landay.

Of course you might have already gone through them,been the bookhound that you are, in which case you might give me an insight.

I have kids and I confess to be terrified by the doings of Kevin and Jacob, who though in fiction, mirrors some terrible things which have really occurred in our modern society.

Have you also thought about writing a book, or actually written one Paula?

I would very much like to discuss this with you.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…