Bookworms of JF, what's your favorite book (s) and why?

J.K Nyerere alivyokuwa The University of Edinburgh , alisoma sana kazi za John Stuart Mill. Hususan kuhusu "utilitarianism". Huyu alikuwa ni kama mwanafalsafa ambaye Nyerere alimpenda kabisa wakati akiwa katika Fabian Society Edinburgh Scotland.

Utilitarianism ya John Stuart Mill ukiichanganya na falsafa za udugu za Kiafrika ndivyo vitu vuilivyopanda mbegu ya awali ya Ujamaa ndani ya mwanafunzi Nyerere.

Ukisoma kitabu cha "Nyerere: The Early Years" cha Dr. Thomas Molony, profesa wa The University of Edinburgh aliposoma Nyerere, utaona hayo na mengine mengi kuhusu historia ya awali kabisa ya Nyerere imeandikwa.

Hiki nacho ni kitabu kizuri sana nilichopata kufurahia kusoma.

Ulivyomtaja John Stuart Mill umenikumbusha hii habari ya Julius K. Nyerere na siku zake za Edinburgh.
 
I see, we jamaa, duuu!
 
Wewe nakufananisha na JS Mills, nasikia kabla hujafikisha miaka 17,

ulikuwa ushasoma vitabu vyote karibu mia vya JH Bond, series zote za Harry Potter, umeshameza Oxford dictionary na kumaliza kitabu chote cha Philosophy of religion, an anthology, na umeshashinda na tuzo ya pulizer prize(not sure the name of the prize)
 
Pole kwa kumpoteza mama mpenzi... May her soul Rest in Peace

Sasa tusiojua kiinglishi tunacomment wapi vitabu vyetu?
 
Kila ulichoandika hapa nazidi kudhibitisha umri ni kigezo.
Nimetoka kapa, sijui haya maneno magumu mnachukua miaka mingapi kuyasoma.
 
Sio kweli bibie. Au kuna kitu nimekosea katika hayo niliyo yaandika ? Kama nimekosea nisahihishe kisha nitakiri kosa.

Kwa hakika sijawahi kuwa mbishi kwa ile maana ya dhati kabisa ya tamko "Ubishi" ila huwa naitwa mbishi kwa dhulma.
Ili uwe mbishi si lazima uwe haupo sahihi kwa unachokiandika. Kitendo tuu cha kuargue uwe right or wrong ni ubishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…