Boom kupandishwa kutoka sh.7500/= mpaka 9750/=

Achoki

Senior Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
151
Reaction score
60
je ni kweli boom litapandishwa mwakani kutoka sh 7500 mpaka sh 9750/= napenda kujua tafadhali
 
Ni vigumu kupandishwa haraka haraka kiasi hicho. Kumbuka Tsh. 5000 imedumu tokea mwaka 2005. Ikizingatiwa ya kwamba gharama za maisha hazijapanda sana tokea wapandishe. Kuna mchakato mkubwa kidogo hata kufikia kubadili nalipo kama boom, per diem n.k.
 
Someni vijana hiyo ela inatosha sana. Hamlipii maji wala umeme. Hivi kima cha chini cha serikali kwa muhitimu wa chuo kikuu mnakijua?

Wengi wakifika mtaani na kuanza shughuli ya kutafuta kazi ukumbuka maisha ya chuo. Tieni bidii katika elimu kwani bumu la uhakika liko mtaani iwapo utaonyesha jitihada pia.
 
ni kweli ndugu,iyo bado inatosha kwasasa by thn hizo fedha mtazirudisha
 
je ni kweli boom litapandishwa mwakani kutoka sh 7500 mpaka sh 9750/= napenda kujua tafadhali

Daah...!! watoto mnapeta sana siku hizi, bumu 7500/=..!? First year Mabibo hostel si ndo watanunua sub woofer, tv na computer hadi zikome.... sijui na mimi nirudi chuo tena!?? lakini nikikumbuka dash na pasi ndefu sitamani.....
 
Vijana wa sasa hivi wa chuo hamjitambui kabisa.
Mnatiana moyo tu na story za Facebook tu.

Serikali haiwezi kuongeza hata senti tano mpaka muandamane, mgome na vyuo vifungwe.
Kama mnataka mkwanja uongezwe anzisheni 'kunji' haraka haraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…