Nadhani tatizo ni serikali na viongozi wenye dhamana.
Nchi hii haishindwi kutoa chakula kwenye shule zake.
Tuna bahari, mito na maziwa makubwa yenye samaki wa kutosha.
Tuna mbuga za wanyama na wanyama wa kila aina.
Uwekwe utaratibu mzuri wa kuvuna hao wanyama na samaki kisha wanakuwa wanasambazwa kwenye shule za serikali watoto wapate chakula.