Bora kumchangia mtu Mahari au harusi?

Bora kumchangia mtu Mahari au harusi?

musicarlito

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2020
Posts
368
Reaction score
556
Sio vizuri kuomba omba kwa mambo uliyoyapanga mwenyewe tena na tarehe unaijua ya tukio

Ni wajibu kuchangia matatizo kama misiba, magonjwa ajali nk...kwa sababu hakuna mtu anapanga au hujiombea hayo japo yapo kwa kujitakia

Lakini kawaida watu husema huwa sheria...tuna desturi ya kuchangia mambo ya kushereheka kama harusi...Send off nk

Je si muhimu kumchangia mtu alie au anae hiari kwenda katika hatua nyingine ya kuwajibika kwa maana ya kuwa na familia...nikimaanisha MAHARI/MAHALI halafu hayo mengine tukamuachia yeye mwenyewe?
 
Mimi kwangu cha muhimu kuchangia ni msiba. Harusi na mahari sijawahi kuvipa kipaumbele.

Ikitokea nimekuja kuoa nadhani harusi yangu haitokua na michango, itakua simple tu. Ndugu na jamaa wachache wa kufurahi nao kwa masaa kadhaa basi. Bajeti ya 2-3mil from my pocket imeisha hiyo.

Kuna jamaa yangu mpaka sasa hatusemeshani. Tulikua marafiki chuoni. Yeye kaoa mwezi wa tano, bahati mbaya alifanya siri sikujua mapema kua anaoa. Kaja kunipa kadi ya mchango imebaki wiki moja afunge ndoa, tena kaweka na kiwango kabisa nichangie laki. Sikuchangia kwavile nilikua nimetingwa na majukumu mengine. Hivi sasa akiniona njiani anabadilisha njia. Dah!
 
Vyote hazifai kuchangiwa.
Kama hata mahari mwanaume atachangiwa, nini maana ya yeye kwenda kuoa hapo?
Kama harusi ni mbwembwe za muoaji, kwanini anichangishe mimi pesa?

Kijamii watu sahihi wa kuchangiwa ni wagonjwa tu, tusisubiri wafe ili twende kuchangia msiba.
 
Mimi kwangu cha muhimu kuchangia ni msiba. Harusi na mahari sijawahi kuvipa kipaumbele.

Ikitokea nimekuja kuoa nadhani harusi yangu haitokua na michango, itakua simple tu. Ndugu na jamaa wachache wa kufurahi nao kwa masaa kadhaa basi. Bajeti ya 2-3mil from my pocket imeisha hiyo.

Kuna jamaa yangu mpaka sasa hatusemeshani. Tulikua marafiki chuoni. Yeye kaoa mwezi wa tano, bahati mbaya alifanya siri sikujua mapema kua anaoa. Kaja kunipa kadi ya mchango imebaki wiki moja afunge ndoa, tena kaweka na kiwango kabisa nichangie laki. Sikuchangia kwavile nilikua nimetingwa na majukumu mengine. Hivi sasa akiniona njiani anabadilisha njia. Dah!
Sasa msiba unachangia kwanini wakati mtu keshakufa? Tena wakati mwingine kwa kukosa hela ya matibabu!
Yaani mi nachangia matibabu ya mtu mwenye uhitaji wa kutibiwa na hana uwezo!

Ila habari za sherehe, harusi nk watanisamehe bure. Tena kwenye msiba ndio kuna maswali mengi khs hiyo michango. Kwani wakienda kuzika na kuondoka bila kula kuna tatizo?
 
Inategemeana na uhusiano mlionao Mzazi anastahili kumchangia mahari mwanae. Ndugu, jamaa na marafiki wa karibu wachangie harusi!
 
Wengine wanakosa aibu wanaweka mpaka kima cha chini wakati ni marafiki tu usipotoa au ukimpa pungufu mnanuniana na mawasiliano yanakata.
 
Sasa msiba unachangia kwanini wakati mtu keshakufa? Tena wakati mwingine kwa kukosa hela ya matibabu!
Yaani mi nachangia matibabu ya mtu mwenye uhitaji wa kutibiwa na hana uwezo!
Ila habari za sherehe, harusi nk watanisamehe bure. Tena kwenye msiba ndio kuna maswali mengi khs hiyo michango. Kwani wakienda kuzika na kuondoka bila kula kuna tatizo?
Yote kwa yote ni muhimu kumchangia mtu hasa mgonjwa au yoyote ambae yupo ktk matatizo. Lakini kuna misiba inatokea bila kuuguza, jirani anafiwa na mtu wake wa karibu kifo cha ghalfa kwa ajali au kuna wanaougua asubuhi mchana amefariki (hapo ndio point yangu ilipo).

Au chukulia una rafiki au workmate kafiwa na mzazi huko kijijini anatakiwa asafiri haraka na vitu kama hivyo. Hiyo kwangu ndio michango ya lazima. Kinyume na hapo ni bora nilaumiwe tu.
 
Sio vizuri kuomba omba kwa mambo uliyoyapanga mwenyewe tena na tarehe unaijua ya tukio

Ni wajibu kuchangia matatizo kama misiba,magonjwa ajali nk...kwa sababu hakuna mtu anapanga au hujiombea hayo japo yapo kwa kujitakia

Lakini kawaida watu husema huwa sheria...tuna desturi ya kuchangia mambo ya kushereheka kama harusi...Send off nk

Je si muhimu kumchangia mtu alie au anae hiari kwenda katika hatua nyingine ya kuwajibika kwa maana ya kuwa na familia...nikimaanisha MAHARI/MAHALI halafu hayo mengine tukamuachia yeye mwenyewe?
Kila mtu apambane na hali yake
 
Karibu Tanzania
Nchi ambayo wakazi wake wanachanga zaidi ya million 15 watumie kwa siku moja

Bibi na bwana harusi wanapanda kwenye Hummer baada ya siku mbili unakutana nao wanagombania dala dala

Bola kumchangia harusi wanandoa watakuwa anasemwa sana
 
Hii mambo ya michango ya maharusi tumeitaka wenyewe watz unajua wabongo tunapenda sifa sana mtu anajikuta anapenda kutoa michango mikubwa kwenye masherehe kwa sababu ya misifa aonekane kuwa ana fedha sasa kimbembe apo aombwe mchango wa mgonjwa unaweza ata asitoe
 
Kibiblia neno kuchanga au kutoa msada haina kiwango ni vile moyo wako unajisikia ila leo kuchanga au kusaidia imekuwa deni tena deni lenye kiwango jambo ambalo halima uhalisia.....'Ukiwa na shughuli yako jipange ili usiwape watu lawama"
 
Mimi kwangu cha muhimu kuchangia ni msiba. Harusi na mahari sijawahi kuvipa kipaumbele.

Ikitokea nimekuja kuoa nadhani harusi yangu haitokua na michango, itakua simple tu. Ndugu na jamaa wachache wa kufurahi nao kwa masaa kadhaa basi. Bajeti ya 2-3mil from my pocket imeisha hiyo.

Kuna jamaa yangu mpaka sasa hatusemeshani. Tulikua marafiki chuoni. Yeye kaoa mwezi wa tano, bahati mbaya alifanya siri sikujua mapema kua anaoa. Kaja kunipa kadi ya mchango imebaki wiki moja afunge ndoa, tena kaweka na kiwango kabisa nichangie laki. Sikuchangia kwavile nilikua nimetingwa na majukumu mengine. Hivi sasa akiniona njiani anabadilisha njia. Dah!
imagine mtu anakununia kisa kabajeti pesa yako ya mfukoni
 
Sasa msiba unachangia kwanini wakati mtu keshakufa? Tena wakati mwingine kwa kukosa hela ya matibabu!
Yaani mi nachangia matibabu ya mtu mwenye uhitaji wa kutibiwa na hana uwezo!
Ila habari za sherehe, harusi nk watanisamehe bure. Tena kwenye msiba ndio kuna maswali mengi khs hiyo michango. Kwani wakienda kuzika na kuondoka bila kula kuna tatizo?
Kabisa waje wamekula...tena wengine wanatoka jirani kabisa[emoji23]
 
Back
Top Bottom