Bora kunywa gongo na viroba kuliko ushabiki wa mpira madhara ni makubwa zaidi

Bora kunywa gongo na viroba kuliko ushabiki wa mpira madhara ni makubwa zaidi

moghaka

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Posts
252
Reaction score
143
Madhara ya ushabiki wa mpira unaoendelea kutamalaki Tanzania ni makubwa sana kuliko ulevi mwingine katika jamii(NAONGELEA “USHABIKI” SIO MAPENZI YA MICHEZO YA KAWAIDA)
  • Umesababisha uvivu uliokithiri hasa mikoa ya pwani na baadhi ya miji ya mikoani
  • Umesababisha wanafunzi, watoto wadogo kuanzia chekechea hadi std 7 KUSHINDWA KUSOMA kabisa kisa kukariri ushabuki wa mpira
  • Umeleta uzembe makazini na majungu
  • Umesababisha upotevu wa heshima na nidhamu aidha kifamilia , jamii, na makazini pia
  • Maeneo ya Pwani na Morogoro kwa kuanzia Tanga , Mtwara, Zanzibar na Daressalaam ndio kitovu chenyewe ni moja ya chanzo cha watoto wa kiume kufeli madarasani na watoto wa kipe kufanya vizuri zaidi ya wenzao wa kiume zaidi ya nusu darasa wanakuwa nyuma
  • Jamii hasa vijana kuharibika kwa maadili hasa badala kuwa wachapakazi na watendaji kwa vitendo na kuwa wapiga DEBE, wapiga DOMO, WABISHI, hodari kwa UBUNIFU WA MAJUNGU, KUKOMAZA UJINGA, mbaya zaidi HAKUNA MALIPO WALA FIDIA HATA YA MUDA N.K
Ebu tujiongeze kuangalia faida za mpira KIFAMILY, KIJAMII, KIUCHUMI N.K
  • Ajira zitokanazo na mpira
  • Mapato yatokanyayo na mpira kwa level ya mtu mmoja mmoja na kiwango gani
Watoto wa pwani wa primary na mitaani wanazijua timu na wachezaji wote wa timu za ulaya kuliko wanachofundiswa shuleni na wote hasa wavulana wanaishia KUFELI masomo mbaya zaidi wanabishana na wazazi wao kutwa kucha family nzima ni mpira hakuna wa kumkosoa mwenzake,

Huyo mtoto atasoma kweli, kuna maadili hapo kweli, ajira , kipato fidia ?

Vijana na wazee wanashindia vijiweni kutwa nzima wakibishana ushabiki wengine wanashinda njaa kwa kutafuna kashata na kahawa, pesa mfukoni hakuna, badala ya kufanya kazi wanabishania wenzao wako kazini wanapokea mamilion ya pesa wao wanatoka patupu...

Hivi vilabu hasa yanga na simba na kwa ushabiki walionao na muda tangu vianzishwe vilipaswa kuwa na asset nyingi sana hata Tanzania kama vile viwanda, majengo hapo kariakoo angalau gorofa 25 kila moja na viwanda angalau vitano kila kilabu,

JAMII yetu kwa ujinga wetu tunawachangia kila kukicha wao wakula tu more than 60yrs ? ?
 
Naona wazembe, wavivu na wengine kama hao mmepata kisingizio kingine!
 
Hivi ulishawahi kuionja hiyo Gongo!
Enewei unaweza kuwa mnywa Gongo na ukaanza kushabikia mpira tena! Unapigwa na vitu viwili vizito kwenye utosi..

KichWa bOX
 
Minaona ingependeza sana kama ushauri wako ungepeleka pale kwenye kilabu cha gongo na nturu mnaposhindaga mchana kutwa nayule jirani yako bwana ntangala.
 
Achana kabisa na tabia ya kuwapangia watu maisha. Ishi maisha yako!!

Wewe kama kilevi chako ni hiyo pombe ya gongo, basi kuna wenzako ulevi wao ni kushabikia mpira.
 
Back
Top Bottom