Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
Kama unachukua mkopo wa 1,000,000 maana yake zaidi ya 200,000 utazitumbukiza bank kwa mfumo wa riba za Tanzania, na kwa tathmini ya haraka hiyo ndio net profit anayotazamia mfanyabiasha kuipata katika mkopo huo. Kwa mtindo huu mfanyabiashara asipokuwa na biashara yenye kuweka pesa yake kwenye mzunguko wa haraka kupata faida ya haraka ataishia kurudisha mkop huku bado hajajenga capital ya kutosha kuendeleza biashara yake, kisha ataendelea na biashara za mabanki kupata mkopo mwingine kuwanufaisha.
Ni sawa kwa wenye nafasi hizo ambao ni wachache sana, Vipi mwalimu aliyeko Tunduru ambaye hata kufika Songea mjini ni issue huo unafuu wa mkopo wa majuu ataupataje? tuiombe serikali iwaombe wenye mabenki washushe riba ili sote tunufaike.
taratibu gani zinahitajika kufungua akaunti katika mabenki ya huko nje ukiwa huku bongo, nchi zipi ni nzuri kuweka akiba? challenges? wana taratibu gani za mikopo?
Mikopo kwenye mabank ya Tanzania riba kubwa mno kiasi cha mfanya biashara kuzalishia bank badala ya kutia pesa mfukoni. Bank za Tanzania riba zinatisha kufikia hadi zaidi ya 15% wakati majuu mkopo wenye secured acoount ni free for short term kwa baadhi mabank na ni 3% - 4% for long term loam. Hapa nimegundua sababu ya wafanya biashara wengi kuwa na acoount nje ambako wanafanya ndio mabank ya kukopa pesa badala ya mabank nchini. Wasio na access ya kuwa uwezo wa kufungua account majuu kwa sababu ya mashari ndio wanaoumia katika mikopo ya mabenk yetu.
...Yaani riba ambayo sasa hivi inatozwa na bank za nchi za magharibi ingekuwa riba kama hii inapatikana nchini basi wengi wangeweza kukopa na kufanya shughuli za maendeleo za aina mbali mbali ili kuinua viwango vyao vya maisha na hivyo kuinua uchumi wa nchi. Sasa hivi variable rates katika baadhi ya nchi ni 2.75% na fixed rates ni 3.3% (5 years), lakini nchini bank zinatoza 15% huu ni wizi wa hali ya juu.
Hivi tufanyeje kuwasumbua hao jamaa wenye hizo bank? Tuandamane? Au tifungue vyama vya watumiaji mabenki ili tuwe na msemo mmoja?