Bora nirudi kwa wazazi wangu wanifunze upya

Bora nirudi kwa wazazi wangu wanifunze upya

ephen_

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2022
Posts
14,949
Reaction score
54,485
"Based on a True Story "

SEHEMU YA 1


"Tina! twende baba yangu amekuja" Haya ni maneno ya rafiki yangu Emmy mchana ya Siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi.
"Mmh! Wewe nenda ukirudi utanikuta" nikamjibu
" Twende nikakutambulishe baba yangu hana shida, lazima ameniletea chakula na huku bwenini vyakula haviruhusiwi, twende Tina tukale"
Mimi ni nani nikatae kwenda kula ukizingatia wazazi wangu wapo mkoani huku hawawezi kuja.
..........................................................

Imepita miaka 12 tokea nilipoanza kuharibu maisha yangu, nimejaribu njia nyingi za kujitoa uhai lakini nimegonga mwamba. Sina jinsi zaidi ya kuchukua ushauri wa rafiki yangu kua nianze upya.

Nina miaka 27 kwasasa ila sio mbaya nikirudi nyumbani kwa baba na mama, nikiwa kwetu nitajihisi amani na utulivu zaidi. Bora nirudi ili mama na baba wanilee upya, safari hii nitasikiliza kila watakachoniambia.

Mama yangu alizoea sana kuniita 'mtukutu' yeye huniambia "Hivi Tina kwa tabia zako hizi wadogo zako unataka wajifunze nini? Kwanini hutaki kubadilika"
Haya maneno yananiudhi sana naona bora shule zifunguliwe niondoke nyumbani.

Nipo kidato cha pili shule ya bweni lakini kila ijumaa ya mwisho wa mwezi wenzangu wakienda usiku kujisomea Mimi natoroka narudi nyumbani mpaka jumapili ndio narudi shule.
Natoroka Siku hiyo kwasababu ni ngumu walimu kugundua sababu jumamosi ya kila mwisho wa mwezi ni visiting day.

MAMA: Leo tena umerudi nyumbani! Sasa kuna faida gani ya baba yako kulipa mamilioni wewe usome bweni, walimu wako wakigundua utafukuzwa shule. Baba yako ndiye anakudekeza wewe!
TINA: Hakuna madhara yoyote, kesho wazazi wanakuja kuwaona watoto wao hakuna kusoma, sasa Mimi nikija nyumbani kuna shida gani?
MAMA: Mimi hayo hayanihusu, muhimu ukifukuzwa shule ni kosa LA baba yako, yeye ndiye amekuza huo mchezo wako.

Baba yangu ni dereva wa malori ya mikoani, hana shida kuhusu Mimi kurudi nyumbani, huwa ananiambia anachotaka yeye ni kuniona nafaulu vizuri.

Nikijiangalia naona kabisa sina akili za darasani, nimeitwa sana mbele ya umati wa wanafunzi wenzangu kama 'best loser' kwenye mitihani ya mwisho wa mwezi, ni kawaida yangu kutofikisha wastani wa 50.

Nimemaliza mitihani ya kidato cha pili nipo nyumbani.
TINA: Hivi mama sina ndugu Dar es salaam niende kukaa kwake hii likizo?
MAMA: Kukaa kwenu hutaki? Nani ataweza kuishi na wewe na utukutu wako huo?

Mama yangu ananiona mtukutu kisa sipendi kutumwa, napenda kukaa kwenye TV tu, nikiwa nyumbani wadogo zangu wanakasirika nawatuma mpaka kazi zangu.

MAMA: Dar es Salaam utakaa mpaka utachoka mwenyewe, kidato cha tatu unaenda bweni huko, sababu ukiwa hapa karibu kila Siku unataka utoroke shule.
..........................................................

MATRON: Umesema unaitwa Tina! Basi subiri wenzako watoke darasani nikupe Emmy awe rafiki yako ana akili atakufaa na wewe ufaulu vizuri.
Sio ishara nzuri kidato cha pili kupata division 3.

Huyu ni matron kwenye shule yangu mpya niliyoamishiwa Dar as salaam.

Safari yangu ya urafiki na Emmy ilianza kwa kuunganishwa na Matron.
.........................

Basi Mimi na Emmy tukaongozana mpaka kwenye bustani waliopo wazazi.
Nikatambulishwa na Emmy kwa baba yake, nashkuru Mungu baba wa watu hakuonesha kutofurahishwa na uwepo wangu pale.

Emmy akafungua mifuko iliyoletwa, jicho langu likatua kwenye chakula ninachokipenda 'Chips kuku' japo kulikua na mazagazaga mengine
Nilikula nikafurahi.

Kitu kilichonishangaza ni baba Emmy wakati anaondoka akanipa elfu 30.
Nikapokea huku siamini macho yangu
"Jamani huyu baba ana roho nzuri sana" nikajisemea

"Sinilikuambia Tina! Baba yangu hana neno"
Elfu 30 nilipewa mbele ya kila Mtu aliyekuwepo pale, Tina nae alipewa kibunda ambacho baadae nilijua ilikua ni laki 1.


Baada ya Mimi kupewa ile hela, mapenzi yangu kwa Emmy yaliongezeka urafiki ulinoga sana ukizingatia baba alitupa nasaha wakati anaondoka "Watoto wangu msome kwa bidii" hivyo tulikua tunasoma kwa kushirikiana na Emmy wangu.

Nikapata utamaduni mpya kila mwisho wa mwezi baba Emmy akija na Mimi nipo! Chips kuku zikaanza kuletwa mbili, shower gel 2, dawa za mswaki 2 kila kitu kinaletwa kwa pair.
Yote Tisa, kumi nililetewa mpaka dictionary bila kusahau kila mwisho wa mwezi elfu 30 yangu ipo palepale.

Ila nina siri ambayo naona nimfiche Emmy JINSI BABA YAKE ANAVYONIANGALIA..!

Sehemu ya 2: Bora nirudi kwa wazazi wangu wanifunze upya

Sehemu ya 3: Bora nirudi kwa wazazi wangu wanifunze upya

Sehemu ya 4: Bora nirudi kwa wazazi wangu wanifunze upya

Sehemu ya 5: Bora nirudi kwa wazazi wangu wanifunze upya

Sehemu ya 6: Bora nirudi kwa wazazi wangu wanifunze upya

Sehemu ya 7: Bora nirudi kwa wazazi wangu wanifunze upya

Sehemu ya 8: Bora nirudi kwa wazazi wangu wanifunze upya

Sehemu ya mwisho: Bora nirudi kwa wazazi wangu wanifunze upya
 
SEHEMU YA 2
Utukutu wangu wote ila Mimi simjui mwanaume.
Nikikaa naona sura ya baba Emmy jinsi ambavyo huwa ananiangalia naona navutiwa lakini huyu ni mtu mzima nazuia hisia za kusema ananipenda au Mimi nampenda.

" Emmy baba yako ana miaka mingapi kwani?" Nikamuuliza rafiki yangu, imekua kawaida Mimi kumuuliza vitu kuhusu baba yake, naona tukimuongelea napata furaha.

" Baba yangu ni mkubwa, mama alishawahi kuniambia baba kazaliwa 71, ebu! 2013 ukitoa 1971 ni 42, baba yangu ana miaka 42" akajibu

Nikaguna kimoyomoyo, Tina mie ndio kwanza Nina miaka 16.

Kama kawaida ikafika visiting day nyingine hapo tayari nipo kidato cha 4, naona aibu kwenda kwa baba Emmy nahisi anavyoniangalia ni kama mtu na mpenzi wake siwezi kusema nahisi kumpenda lakini navutiwa na anavyonitazama.

"Tina unaitwa na baba" rafiki yangu Emmy alinifata kuniita ni baada ya kumtoroka ili kukimbia kumuona baba yake.

Nikakubali wito, kama kawaida nikamsalimia "Shikamoo baba" hakuitikia ila akaniuliza "vipi unaumwa? Nikamjibu "hapana"

Akasema "Leo inabidi niwaachie hela ya kutosha sababu tumeambiwa hatutoruhusiwa tena kuja kuwaona kidato cha nne miezi iliyobaki muwe busy na kujisomea"

Nikashtuka kimoyo nikajiambia "hela ya kutosha ndio kiasi gani hicho! Mimi nishazoea elfu 15, elfu 20 za wazazi wangu"

Macho ya baba Emmy bado yananitizama na Mimi imekua kawaida nikimuangalia kwa aibu, rafiki yangu yeye nimemsoma haoni macho ya baba yake.

Baba Emmy akamtuma mwanae akamuite Matron, Emmy alivyoondoka nikapewa hela kiuficho halafu akaniambia "Siku ya graduation yenu nikija kuna kitu nitakuambia"

Emmy alivyorudi baba yake akaaga ila akanipa tena hela na Emmy akapewa
Emmy akaniuliza "amekupa bei gani? Nikafungua mkono kuhesabu ni elfu 70 nilipigwa na butwaa!
Emmy nae akahesabu akakuta ni laki 2

Muda wote nimekaa na Emmy nawashwa kwenda ufichoni kuhesabu hela nilizopewa mwanzo nilizificha ndani ya mfuko wa sketi.
" Emmy nakuja naenda chooni"
Nikawa natembea harakaharaka, nilipofika nahesabu ni elfu 50, jumla nimepewa laki na ishirini.

............................................................
Ulikua unadhani nataka kukuambia nini? Msg imeingia kwenye simu yangu kutoka kwa baba Emmy

Nikamjibu "Mimi sijui"

BABA EMMY: Nilivyotegemea ilikua tofauti sana siku ya graduation yako, ulikua busy na wazazi wako na Mimi ndugu zake Emmy walikua wengi nisingeweza kukuita kukuambia nilichotaka.

TINA: Unaweza kuniambia hata hapa kwenye simu.

Muda huo nishajua baba Emmy amenielewa na Mimi akinitongoza siwezi kumkataa, sijali umri wake hats hivyo bado analipa.

BABA EMMY: Ungekua unaishi Dar es Salaam ingependeza zaidi, huko mkoani halafu bado wewe ni katoto itakuaje nikitaka tuanzishe urafiki.

Huzuni mpya ikaniingia moyoni, kumbe naweza kumpoteza baba Emmy kisa tupo mikoa tofauti.
Nifanye nini nikaishi zangu Dar es Salaam?
Nina shangazi yangu kule lakini ni wa mbali kidogo, nikimuomba baba nikaishi huko wakati nasubiri majibu lazima atakubali lakini vipi kuhusu mama ambaye ana gubu sana, ananiudhi anavyonibanabana.

TINA: Mama eeh!
MAMA: Nini?
TINA: Pre form five nataka nikasome dar kuna kitu kizuri wenzangu tuliomaliza nao wote wanaenda kusoma hapo.

MAMA: Ni bweni au?
TINA: Hapana
MAMA: Basi kitulize! Utatafuta hapahapa usome, kwanza hata majibu hayajatoka

TINA: Kwamba unadhani nitafeli sio!
MAMA: Hapana! Wasiwasi wangu utakaa wapo huko? Kwa tabia zako mbaya huwezi kuishi kwa watu tofauti na hapo ungeenda kwa shangazi yako.

TINA: Niruhusu mama! Nitaenda kuishi nao vizuri.
MAMA: Wewe nakujua, una kiburi, mvivu, m'babe. Msubiri baba yako akirudi Mimi sitaki lawama.

Nilikasirika sana, wasiwasi wangu ni baba Emmy kua nae mbali naona sitoweza kabisa.
.......................................................
Hizi ni nyakati ambazo nazikumbuka sana! Natamani ingekua ni ndoto au nipewe nafasi ya pili nirudi kua Tina mwenye miaka kabla ya 16 au wazazi wasingenipeleka kusoma Dar es Salaam.

Kila nikifikiria naona Nina wengi wa kuwalaumu baba asingekua ananipa Uhuru kiasi kile au mama angeongea na Mimi kwa kina kila tendo baya na madhara yake lakini najiona Mimi ndo mkosaji zaidi.

'Haya uliyonifanyia Mimi, vipi mwanao Emmy akifanyiwa hivyohivyo' haya ni maneno niliyomwambia baba Emmy huku nikitoa machozi.

"Muhimu kila mtu atabeba mzigo wake" alinijibu huku macho yake yakiwa kwenye TV.

Nisikilize nikuambie "nalipua hii nyumba moto wote tufie ndani, siwezi kuishi kwa mateso kiasi hiki" nikamwambia Mzee wangu

Baba Emmy mapenzi yetu yalivyonoga nikaacha kumuita baba nikambatiza jina 'Mzee' Basi namuita kwa manjonjo "Mzee wangu karibu kula, Mzee wangu twende tukalale"

Sasa mapenzi yetu hayapo tena ananijibu "Ukilipua hii nyumba Mimi sina hasara, watoto wangu ni wakubwa wanaweza kujitegemea, Mimi pia nishakula chumvi nyingi na miaka yangu hii 50, vipi wewe binti hata miaka 25 bado hujafika?

Nililia sana nilidhani nikimwambia habari za moto ataogopa, atarudisha mapenzi kwangu lakini kumbe yeye hajali.
............................................................

TINA: Shikamoo baba! Baba naomba niende kusoma pre form five Dar es Salaam
BABA: Umeshindwa kusubiri hata nipumzike? Kwani matokeo yameshatoka?
TINA: Hapana baba
BABA: Basi subiri yakitoka utaenda, kuna shangazi yako kule hana shida.

Sikufurahi lakini kidogo nilipata ahueni nikijua matokeo yakitoka nitaenda Dar es Salaam, nitakua namuona baba Emmy ambae Nina uhakika kabisa tunapendana.
 
SEHEMU YA 3
Hii taarifa nilimpa baba Emmy akaniambia ni sawa nitulie mpaka matokeo yakitoka.

Matokeo yalipotoka niliambulia division 3 haikua mbaya na safari ya Dar ikawadia.
Nilikua nina furaha sana,nilipofika kwa shangazi nikamjulisha baba Emmy nae akaniambia itabidi kesho yake tuonane ana maongezi na Mimi.
Akasema itabidi niende Bar X Saa 1 usiku, umri wangu haitofaa kua nae maeneo hayo mchana.

Kwa kusoma mazingira ya nyumbani kwa shangazi nisingeruhusiwa kutoka usiku na haya nilimuambia baba Emmy akanijibu hamna shida.
Ila aliniambia ana safari nje ya nchi kwa muda wa miaka miwili.

BABA EMMY: Vipi nikikupa smartphone ili iwe rahisi sisi kuwasiliana, nikiwa nje.
TINA: Sijui itakuwaje nyumbani wakigundua.
BABA EMMY: Basi waambie una hela uliweka kipindi upo sekondari unataka ununue simu.

Nilimwambia baba, baba akasema hamna shida, ninunue tu simu.

Baba Emmy aliniaga kisha akaniambia kuna mtu atanipigia nikafate simu. Na kweli simu kadhaa nilipigiwa simu nikamuelekeza Huyo mtu akaniletea simu.
Nilifurahi sana kumiliki smartphone simu yangu ya kwanza Tecno W5.

Miezi ilienda nikiwa nawasiliana na baba Emmy Mara nyingi alikua akinitumia video chafu za watu mpaka nikazoea.
Hakuwahi kunitongoza lakini ule ukaribu wa kuwasiliana tukajikuta tayari ni kama wapenzi.

Kuna siku aliniambia kama nina mahusiano nikamjibu Hapana na wala sijawahi kufanya mapenzi. Alishangaa inawezekanaje kumbe hakujua tokea nimfahamu nimetokea kumpenda sana hata wavulana wa agemate nawaona kama ni mashoga zangu tu.

Hakukuwa na cha maana kwenye hiyo miaka miwili ambayo mpenzi wangu alikua nje, Ndio ni mpenzi wangu kwasasa nimezoea kumuita hivyo huko WhatsApp ukiangalia msg zetu hutoamini kama ni binti wa 10's na mwanaume wa 40's.

Utajiuliza vipi kuhusu urafiki wangu na Emmy, urafiki wangu na Emmy ulipungua ukizingatia advance kila mtu shule yake lakini tulikua tunawasiliana na hajawahi kujua kama siku zingine huwa namwambia baba yake "Mpenzi natamani ungekuwepo karibu ili uwe mwanaume wangu wa kwanza"

Sijui kwanini nampenda baba Emmy au ni zile pesa zake alizokua ananipatia? Au ni vile alizoea kuniangalia? Au ni jinsi alivyo mwanaume wa makamu mtanashati?

...........................................................
"Niambie nikufanyie usahili vyuo vipi?" Mzee wangu ananiuliza nikiwa kifuani kwake.
Ndio! Baba Emmy namuita Mzee wangu mapenzi yetu yamekolea sana tokea arudi Tanzania na Mimi nimefaulu kwenda chuo.

"Hapo nataka vyuo vya Dar" Nilimjibu
Na kweli selection zilivyotoka nilichaguliwa chuo kimojawapo Dar.

Chuo wanaume wengi walinitaka lakini Mimi niliwakataa, kwenye moyo wangu yupo Mzee wangu tu! Nampenda sana.

Haikua rahisi kujigawa muda wa chuo na muda wa kua na mpenzi wangu sababu Mara kwa Mara nilikua napenda nionane nae na yeye hupenda kunipeleka Bar huko nilijifunza kunywa nikawa mzoefu.
Matokeo ya mwaka wa kwanza yalipotoka nilipata GPA ya 2.4 ilinishtua sana.

Nikakumbuka maneno ya lecturers kwamba "Yaani mwaka wa kwanza ukikosa first class sahau kuipata miaka inayofuata"
...........................................................

TINA: Hallow!
BABA EMMY: Niambie huko hospital wamesemaje?
TINA: Unajua siamini! Eti daktari kasema nimeathirika.
BABA EMMY: Ebu! Toka hapo hospital njoo nyumbani kwangu.

Mzee akanielekeza kwake, ni baada ya miaka mingi kupita tokea nimfahamu Leo kwa Mara ya kwanza ananielekeza niende kwake.

Nikapanda daladala kuelekea huko.
Niliamua kwenda hospital baada ya kutojisikia vizuri kwa muda mrefu nilipomshirikisha Mzee aliniambia niende hospital labda Nina UTI na kweli UTI nilikutwa nayo ila daktari alinishauri nipime na damu pia.

DAKTARI: Una mahusiano? Nakuuliza japo naona una miaka 20 hapa.
TINA: Ninayo
DAKTARI: Ushawahi kupima kipimo cha HIV hapo kabla?
TINA: Ndiyo! Ila zamani huko kipindi nipo sekondari
DAKTARI: Umekuja na nani hapa hospital?
TINA: Peke yangu.
DAKTARI: Naomba unifate nikupeleke kwa watu wanaohusika na kitengo hiki.

Moyo wangu ulishtuka, nikajiuliza anipeleke kitengo gani tena? Niliendelea kukaa nikimuangalia wakati huo daktari amesimama ilibidi na yeye akae tena chini.

DAKTARI: Tina! Majibu yako ya damu sio mazuri inaonesha una virusi vya ukimwi lakini sio mwisho wa maisha. Nifate nikupeleke kwenye jengo LA ushauri nasaha wana maelezo zaidi.

Nilitabasamu! Maelezo yake hayakunihuzunisha sababu najijua sina mazoea ya kuchangia vitu vyenye ncha Kali na wenzangu pia nimetulia tokea nizaliwe namjua mwanaume mmoja tu, na Mzee wangu hana virusi jinsi alivyo mtanashati, mtaratibu, mpole na mwenye afya njema hivyo Mimi sina virusi.

Nilipotoka wakati daktari yupo mbele ameniacha hatua kadhaa ndio nikampigia mzee simu, simu ilipokata nikageuza huyooo! Harakaharaka hadi nje ya hospital kutafuta kituo cha daladala.
........................

"Mpe boda simu nimuelekeze, atakapokushusha wewe sukuma tu geti Mimi nipo ndani" Mzee wangu aliniambia akiwa upande wa pili wa simu na Mimi nikatii.

Boda akachukua simu alipomaliza kuongea safari ikaanza kutoka mwenye kituo nilichoshuka mpaka nje ya geti la kijivu.
Kwa Mara ya kwanza nimeona nyumba ya mzee wangu sio mbaya ni nzuri wastani.
TINA: Daktari amesema nina virusi vya ukimwi.
BABA EMMY: Itabidi nikuunganishe na bima ya kazini kwangu ili uanze kwenda kuchukua dawa hospital X ya private.

Nilishtuka kusikia hayo maelezo yake, nikabaki namshangaa.

BABA EMMY: Tena uanze dawa mapema na uzingatie matunda, asali kwa wingi. Wewe kinga yako ya mwili inaonekana haiko imara yaani virusi kidogo tu ushaanza kuumwa na vidonda vya mdomo juu.

Baada ya yeye kuniambia hivyo ndio akili yangu ikazinduka kua hapa nimeingia choo cha kiume nikaangua kilio.

TINA: Unamaanisha Mimi nina ukimwi?
BABA EMMY: Unaniuliza Mimi tena? Wewe sindiye umeniambia?
TINA: Ndivyo daktari alivyosema lakini sijamuamini na mbona wewe huonyeshi kushtuka?
BABA EMMY: Nishtuke nini wakati Mimi nimekubaliana na hali yangu.
TINA: Kwamba na wewe una virus?
Niliuliza huku natoa macho nikimuomba Mungu jibu liwe 'Hapana'
BABA EMMY: Ndio

Nilihisi kuanguka huku nimekaa, niliwakumbuka wazazi wangu ghafla! Nikamkumbuka rafiki yangu Emmy ambae hajui mahusiano yangu Mimi na baba yake.

TINA: kwanini sasa umenifanyia hivi? Kwanini umeniambukiza?
BABA EMMY: Aisee! Sikujua kama utapata kama ambavyo hujapata mimba.

Nililia sana kwa uchungu, nilifikiria mengi sikujua kama kweli watu wanapata virusi, sikujua kama na Mimi nitakuja kua mmojawapo.
Mzee wangu ilibidi anibembeleze na alikua anasisitiza nipunguze mayowe majirani wasisikie.
Akaniambia "Tina nakupenda! Wewe usijali nitakua na wewe bega kwa began muhimu usimwambie yeyote kuhusu hili"

Niliendelea kulia lakini moyoni nilipata unafuu baada ya kusikia Mzee wangu ananipenda sababu na Mimi nampenda pia.

Chuoni kati ya wadada wanaoishi maisha mazuri na Mimi ni mmojawapo, boom ninalo na mzee wangu ananipa pesa kila nikimuomba hapa nalia lakini namiliki Samsung yenye edge ambayo Ndiyo kwanza imetoka nikiwa darasani wenzangu macho yote kwenye simu yangu.

Nilikaa kwa mzee wiki nzima mapenzi motomoto mpaka nikasahau kama hospital walisema nina virusi.
Hiyo siku alirudi akanikuta nimejilaza akanipa bahasha nilipofungua nikaona bima ya afya akaniambia nitaitumia kwenye hospital 5 za private na akanitajia ila akasema kesho nijiandae niende hospital A ndio rahisi zaidi hamnaga foleni.

Nilihisi huzuni upya, nikakumbuka kumbe ni kweli nina ngoma ila sikujali sana nikamuuliza "Lini ulipata virusi?
Akanijibu " Muda sana zaidi ya miaka 10 mwanzoni niliona tabu ila sasa hivi nadunda tu" akaongezea "Ukienda kesho mwambie daktari kwenye kadi yako ya dawa aandike jina lingine" akimaanisha nitumie jina fake kwenye kadi ya kuchukulia dozi.
...........................

Kuna hali mpya nahisi, nikiwa natembea sanasana mazingira ya chuo naona kama watu wanajua hali yangu, najishtukia.
Ukweli usiofichika tokea nichukue dawa nakosa amani sana muda mwingine nikikaa peke yangu nalia lakini bado nahisi kumpenda mzee wangu.
.......................

Mimi nina akili bhana! Nilijiambia, hata kama nilikua sisomi vya kutosha sio rahisi Mimi kudisco yaani wale wengine waliofeli form 4 wakaambulia division 4 wakaenda kuanza certificate, diploma sasa degree wamefaulu ila Mimi niliyefaulu form 4, form 6 Leo naambulia GPA ya 1.4! Nilihisi nina mikosi na ndoto za kununuliwa gari na mzee wangu kama alivyonihaidi imeyeyuka.

"Siku ya graduation yako nitakupa zawadi ya gari" mpenzi wangu aliniambia kipindi nipo mwaka wa kwanza.

"Sasa inakuaje unadisco kizembe hivyo na course yako ni nyepesi? Watoto wa sikuhizi bhana" Mzee wangu aliniambia

"Imetokea bahati mbaya tu, na Mimi kuanza upya mwaka wa kwanza sitaki"

"Unataka nini?" Nilifurahia swali hili LA mzee wangu

"Nataka biashara hata ya saloon na spa" nilimjibu

"Hiyo biashara inahitaji mtaji wa kutosha, subiri mpaka Emmy amalize chuo sababu yeye anakula hela zangu nyingi kama unavyojua hana mkopo na course yake ada ni nyingi" aliniambia Uso ukiwa mkavu.

Kwa Mara ya kwanza naomba kitu kwa mpenzi wangu na yeye ananinyima.
 
Back
Top Bottom