Outlier, nimekushauri kuwa hizo facts ziweke kivyako acha kuchangia mchango wangu, changia thread!, fact gani unazitaka zaidi ya hiyo link niliyoitoa, nawewe bandika literature inayoonyesha kuwa good diabetic care ELIMINATES long term complications, na hapa tuanazungumzia majority ya diabetics, ambao hata mlo mmoja ni shida kuupata,. Ninaposema thread ni philosophical hata huelewi maana yake, we unataka madesa ya ki-technical unayoyaita facts, tell the forum your OWN VIEWS on the subject!
umeni-address three times; nashangaa unaposema "tell the forum" wakati wewe wani-tell mimi.
kifupi ni kuwa;
1. HIV/AIDS ni uniformly fatal - yaani even after how many years/treatment bado itakuondoa wakati diabetes with good control ya blood sugar waweza ku-survive
2. Dawa za HIV/AIDS ni lazima kunywa aina 3 ama zaidi, na mara nyingi frequency ni mara 3 au zaidi kwa siku wakati kwa kisukari either dawa moja ama at most 2 na possibly mara moja ama mbili tu kwa siku.
3. Dawa za HIV/AIDS zina side effects nyingi zaidi ya dawa za kisukari, partly kwa sababu unakunywa dawa nyingi
4. Complications za kisukari (ambazo ni chache uki-control sukari vizuri) zaidi zaidi ni macho, figo, mishipa ya fahamu na moyo wakati complications za HIV/AIDS ni systems zote za mwili (zilizotajwa na zingine zote zinazobaki eg GIT nk), tena HIV/AIDS inasababisha mpaka kuongezeka risks za cancer kama kaposis sarcoma na nyingine nyingi.
5. HIV/AIDS kuna hatari ya kuambukiza wengine wakati diabetes huwezi kuwaambukiza wengine
6. HIV/AIDS ukipata watu wanakunyanyapaa na kukusuta (tatizo kubwa) kwa hiyo inakuathiri sana ki-psychologia wakati kisukari watu hawakunyanyapai na mara nyingi wanakuonea huruma hivyo ki-psychologia unakuwa better off
7. Mwisho, katika perspective ya community, HIV/AIDS ni tatizo kubwa kuliko kisukari shauri ya kuathiri watu wengi na matatizo kede kede yanayohusiana nayo.
Ni hayo tu kwa sasa;
waweza kujikumbusha hapa
HIV/AIDS Symptoms, Transmission, Diagnosis, Treatment and Prevention on eMedicineHealth.com
kwa wenye kisukari;
punguza ama acha kunywa pombe
fanya mazoezi regularly
kula vyakula vyenye fiber kwa wingi, na proteins - matunda, mboga mboga, maharage, usiache wanga ila punguza, pia mafuta mazuri ni yale yatokanayo na mimea eg alizeti
kama umeanza dawa tumia kama inavyoshauriwa
usivute sigara
pima mara kwa mara sukari yako