Boriska: Binadamu anayedai kuwahi kuishi sayari ya Mars

Boriska: Binadamu anayedai kuwahi kuishi sayari ya Mars

Boriska is said to have disappeared along with his mother and a number of attempts by Western Journalists to track him down has failed. One journalist had been informed by one of Russian associate that Boriska is now in a remote village under the protection of Russian Government and an attempt to reach him would be futile.

A several psychics have claimed that they have been able to communicate with Boriska through their minds and that they have been replied by Boriska with a similar saying that he is in a remote place with his mother but he is doing okay and that the Russian Government has something to do with it.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1043226

Utakaposikia stori ya kijana Boriska Kipriyanovich anayeishi eneo liitwalo Volvograd nchini Urusi, unaweza usiamini hata kidogo, sanasana utamuona dogo huyu kama amechanganyikiwa.

Hebu sikia stori hii; Boriska anadai kwamba kabla ya kuzaliwa hapa duniani, amewahi kuishi kwenye Sayari ya Mars kwa miaka kibao na alikuwa rubani. Anaeleza kwamba kwa kipindi hicho, alikuwa anakuja duniani mara kwa mara, akiwa anaendesha ndege zinazotumika huko, ambazo kitaalamu huitwa spaceships.

Nikufafanulie kidogo hapo, spaceships, zimekuwa zikitajwa sana kuwa ni ndege zinazotumiwa na aliens, viumbe kutoka sayari nyingine kuja duniani.

Muundo wake siyo kama ndege hizi unazozijua, zinakuwa na mfano kama wa meli kubwa, zikiwa na vifaa vingi na mitambo ya nguvu, zikiwa na uwezo mkubwa wa kusafiri kutoka sayari moja hadi nyingine, ndani ya muda mfupi.

Tuendelee; Boriska anaeleza kwamba wakati fulani katika sayari hiyo ambayo wakazi wake wana miili mikubwa na wanavuta hewa ya Carbondioxide, kulitokea vita ya nyuklia kati ya pande mbili zilizokuwa zinakinzana, vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Ni vita hiyo ndiyo iliyoharibu kila kitu kwenye sayari hiyo, wakazi karibu wote wa Mars ambao huitwa ‘martians’ walikufa kwenye vita hiyo, wachache walionusurika, wakakimbilia kwenye sayari nyingine ikiwemo duniani.

Anafafanua zaidi kwamba, wapo ‘martians’ wachache ambao walijificha kwenye mahandaki wakati wa vita hiyo, wao walisalimika na kwamba baadaye, walianzisha upya maisha ambayo yanaendelea hadi leo, lakini siyo kwa kiwango kama kile kilichokuwepo kabla ya vita hiyo.

Ilikuwaje mpaka akafika duniani? Boriska anaeleza kwamba baada ya mabomu ya nyuklia kupigwa kwa wingi, hakuelewa tena kilichoendelea, hajui kama alikufa au ilikuwaje, lakini baadaye kumbukumbu zake zilipoanza kumjia, alijikuta akiwa duniani, tena mtoto mdogo.

Sasa sikia hii; Boriska alizaliwa nchini Urusi mwaka 1997 na mama yake ni daktari. Mwanamke huyo anaeleza kwamba mwanaye akiwa na umri wa siku 15 tu, alianza kuonesha mambo yasiyo ya kawaida, kwanza aliweza kunyanyua kichwa chake mwenyewe bila msaada wa mtu yeyote, jambo ambalo haliwezekani kwa watoto wenye umri huo.

Baadaye, alianza kuonesha mambo mengine makubwa kuliko umri wake na alipofikisha umri wa mwaka mmoja na nusu, tayari alikuwa anaweza kuzungumza maneno yote, alikuwa anaweza kusoma, kuhesabu na kuchora!

“Tulipompeleka chekechekea, siku chache baadaye walimu wake walituambia kwamba ‘ha-fit’ kusoma chekechea kwa sababu anajua mambo mengi mno,” alinukuliwa mama yake.View attachment 1043228

Ilibidi wamrudishe nyumbani na kusubiri aongezeke kidogo kimo kwa sababu umri wake ulikuwa mdogo sana kumpeleka shule za wakubwa. Akiwa nyumbani, alianza kuonesha kuvutiwa sana na elimu ya anga za mbali, baadaye alipelekwa shule za kawaida ambako nako walimu walimuelezea kwamba ni ‘super intelligent’.

“Miaka kadhaa baadaye, ndipo alipoanza kueleza kwamba eti amewahi kuishi Mars na kusimulia haya anayoyasimulia leo. Hatujawahi kumfundisha chochote kuhusu Mars na hata walimu wake wanasema hawajawahi kumfundisha chochote kuhusu elimu ya anga,” aliongeza mama yake.

Kubwa kuliko; Boriska akiwa amefikisha umri wa miaka 11, amewahi kuelezea kuhusu mapiramidi ya Misri akililenga zaidi lile la The Great Sphinx of Giza. Katika maelezo yake, alinukuliwa akisema kwamba sanamu hilo kubwa zaidi duniani kuwahi kuchongwa kwa jiwe moja, lina siri kubwa ndani yake ambayo siku ikigunduliwa, itabadilisha kabisa maisha ya binadamu wote waliopo duniani.

Akaongeza kwamba ili kulifungua, kuna alama maalum chini ya moja ya sikio la sanamu hilo na kwamba Wamisri walikuwa na uhusiano mzuri kwa miaka mingi na alliens. Miaka michache baadaye, wanasayansi waligundua kwamba ni kweli chini ya sikio moja la sanamu hiyo, kuna kitu kisicho cha kawaida kinachoweza kufananishwa na ufunguo.

Mpaka hapo unaamini Boriska amechanganyikiwa au anasema kweli? Majibu bado hayajapatikana. Kwa sasa ana umri wa miaka 22.




Huyo Boriska alivuta bangi ya Njombe.😁😁
 
Boriska is said to have disappeared along with his mother and a number of attempts by Western Journalists to track him down has failed. One journalist had been informed by one of Russian associate that Boriska is now in a remote village under the protection of Russian Government and an attempt to reach him would be futile.

A several psychics have claimed that they have been able to communicate with Boriska through their minds and that they have been replied by Boriska with a similar saying that he is in a remote place with his mother but he is doing okay and that the Russian Government has something to do with it.

Sent using Jamii Forums mobile app


That boy must be suffering from a sort of mental ailment. Hallucination or derangement of brain---- how can some one live in any form in the Planet Mars and under any means happen to be living on the Earth??, a very unspeakable ridiculous.😁😁😁
 
Tatizo letu sisi bina-adamu tuna amini na kuiishi ile mifumo ya duniani ya maisha tuliyo ikuta ambayo mingi yake hutufanya kuwa na mitazamo sawa .

Mitazamo iliyofanana fanana,maisha yaliyo fanana fanana kila kitu kufanana fanana.

Hii "Mungu " !.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazungu wanatabia ya kuanda feature ya watoto wao huyo mtoto anaandaliwa awe maarufu na wameanza kufanikiwa

Haiwezekani aishi Mars kama alien alafu aje kuzaliwa duniani kama binaadam kutokana na nature ya binaadam
Na hata hivyo viumbe vinavyoitwa aliens pia ni vya kufikilika tu lkn kiukweli havipo
Wapo wanasayansi wameenda sayari ya Mars hawakuona dalili ya kiumbe chocho kuishi Kyle

Kuhusu huyo dogo kuyajua mambo ya anga sio ishu maana kila kitu kipo katika published documents anaweza akasoma au akahadithiwa akavijua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Science yenyewe imethibitisha kuwa hakuna kiumbe ktk sayari ya Mars maana tayari sayari ile ilishafikiwa. Inamaana kuna tafiti zingine ktk sayari hiyo? Pia demonic people huongea vitu visivyojulikana ktk ulimwengu wako na wangu na kuchanganya watu. Science pia zina fiction kama unataka kujua angali sayansi ya hollywood . Sina haja sana kutoamini kuwa hiyo story ni spiritual maana ni imani ya budha kuwa unaweza kuwa paka leo ukafa ukaja kuzaliwa kama binadamu miaka mingi baadae i.e The law of karma. Hiyo ndio kusema allein wa Mars amezaliwa kama binadamu huko Urusi kama umeamini amini pia budhism.
Natoroka kidogo
THERE MORE EVIDENCES FOR LIVE UNDER MARS. BADALA YA KUANGALIA SERIES JIBURUDISHE NA RESEARCH FINDINGS ZA MAMBO YA KALE.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom