Bosi alinisimamisha kazi bila sababu yoyote. Leo anamwambia mwenye kampuni kwamba nina matatizo ya kifamilia

Bosi alinisimamisha kazi bila sababu yoyote. Leo anamwambia mwenye kampuni kwamba nina matatizo ya kifamilia

Jemima Mrembo

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
2,864
Reaction score
8,328
Huyu boss nahisi ana pepo wachafu. Issue ilikiwa hivi, tarehe 19 aliniita ofisini kwake, akasema anataka tufanye mahesabu ya madai yangu yote.

Tulipomaliza kufanya mahesabu, akanipa mshahara wangu na kuniambia akinihitaji ataniita. Kwa kuwa nililetwa hapo na mwenye kampuni, naye alikuwa ameniajiri na kunikabidhi kwa HR ili waniandalie mkataba.

Ni zaidi ya miezi sita sasa, HR hawajanipa mkataba wangu, wanasingizia hadi aje owner ambaye muda mwingi yuko kwao Sweden.

Basi nilipopewa mazaga yangu nikarudi home kukaa, juzi nikaona nimjulishe owner kwamba nimeondolewa kazini bila sababu yoyote.

Leo owner kampigia simu boss kumuuliza kwanini kaniondoa?/boss akajibu eti mimi nina matatizo ya kifamilia tena makubwa ila yakipungua atanirudisha.

Owner aliponieleza hayo nikashangaa sana kwani mimi familia yangu ina amani sana.

Owner kuniambia kwamba nimjulishe boss kwamba nimesha maliza mtatizo jumatatu nipo tayari kwa kazi.

boss kamaindi sana.
Kakasirika haswa ila atafanyeje!
 
Hapo sasa upafom, na ujitume sifa zitamfikia tu boss hata wakikuwekea kauzibe, sio tena kwa sababu utaogopwa uanze kuvimba na kujisahau....
Umemaliza, afike kazini mapema, kazi anazopewa afanye Kwa ufanisi, ajitahidi kutokua na kiburi hata Kwa aliowashinda cheo aheshimu watu wote kwenye taasis atafika mbali
 
Back
Top Bottom